Unaongelea kusafiri kwako wewe unamaanisha Nini? Ajali inaweza tokea popote mkuu...unaweza toka kimara kwenda Ubungo pia ukapata ajali..sasa kuzuia familia zisikae kwenye usafiri mmoja ni wazo ambalo halina mashiko kutokana na ugumu wake katika utekelezaji...Kuna watu wanaishi maeneo ambayo barabara zinapita nao utawazuia wasipande chombo kimoja Cha usafiri..coz na wao pia wapo kwenye risk kubwa ya kupata ajali...wanaweza pata hizo ajali kutokana na highway kupita maeneo Yao..mfano watu wanaoishi pembezoni kwa morogoro road..
Pia Kuna maeneo yanachangamoto ya usafiri gari Moja asubuhi gari Moja jioni..sasa hapo utazuiaje marufuku wanafamilia kupanda Hilo gari Moja...haya Kuna wengine wanasindikiza wagonjwa, misiba au wanashughuli za kifamilia sasa utawambiaje ni marufuku kusafiri pamoja..kinachotakiwa hapo ni kuboresha miundombinu..Hilo eneo linasifika kwa ajali za mara kwa mara kutokana na ufinyu wa barabara na si kwa kuwa familia zinapanda usafiri mmoja.