Waliofilisiwa biashara zao kwa mgao wa umeme 2022 watafidiwa na nani?

Waliofilisiwa biashara zao kwa mgao wa umeme 2022 watafidiwa na nani?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mwaka 2022 unaelekea kufikia mwisho ni mwaka ambao watanzania wengi wamefilisika na biashara zao nyingi zimekufa na kupoteza wateja hasa zile biashara zilizokuwa zinategemea nishati ya umeme chini ya uongozi wa Waziri Januari Makamba(MNEC).

Watu wa biashara za saluni za kike na za kiume, biashara za stationary, biashara za uchomeleaji vyuma, biashara za kufyatua matofali, biashara za kuuza nyimbo kwenye flash, biashara za studio za muziki, biashara za bucha za samaki na nyama, wauza juice,.

Watengenezaji wa barafu, wauzaji wa ice cream na biashara mbalimbali zinazotegemea umeme hawatausahau mwaka 2022 jinsi walivyopoteza mapato mengi kutokana na kadhia ya kukosekana kwa umeme.

Wenye viwanda nao hawatausahau mwaka 2022 kwa kupunguza shift za uzalishaji kutokana na mgao wa umeme.

Lakini na sisi wananchi wa mwisho hatutasahau jinsi bidhaa zilivyopanda bei mara dufu vikiwemo vifaa vya ujenzi kama mabati, saruji, nondo, vigae na bidhaa mbalimbali za viwandani kutokana na tatizo la umeme.

Pamoja na matatizo makubwa hayo ya kiuchumi yako mengi mazuri yamefanywa na Serikali ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari.

Je wananchi wote walioanguka kibiashara kutokana na tatizo la mgao wa kutengenezwa na MNEC Januari Makamba kwa mwaka mzima wa 2022 watanzania hawa masikini watalipwa fidia na nani?
 

Attachments

  • 241826586_4573559236041368_8194241424205200694_n.jpg
    241826586_4573559236041368_8194241424205200694_n.jpg
    72.1 KB · Views: 6
Mimi nadhani jukumu hili wapewe wenyeviti wa vitongoji na mitaa nchi nzima wafanye tathmini ya hasara iiyopatikana kwa wananchi wao kutokana na mgao feki alioutengeneza Makamba alafu wakabidhi madai hayo kwa wabunge wajende nayo bungeni ili Makamba aweze kulipa fidia aliyoisababisha kwa mwaka mzima 2022
 
Back
Top Bottom