Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Wachimbaji wawili wa dhahabu Mpina Shukuru (29) mkazi wa Muganza Chato mkoani Geita na Renatus Nyanga (35) Mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza wameokolewa wakiwa hai baada ya kukaa kwa muda wa siku 8 ndani ya shimo walilofukiwa na kifusi wakitafuta dhahabu katika mgodi wa Igalula uliopo wilayani Nyang’wale mkoani Geita.
Wakizungumza na EATV katika eneo la tukio mashuhuda waliohusika kuwaokoa watu hao wanaipongeza serikali pamoja na uongozi wa mgodi huo kwa jitihada walizozionesha mpaka kuwaokoa watu hao wakiwa hai.
Hussen Makubi Mwananyanzala ambaye ni Mmiliki wa leseni katika eneo hilo amesema eneo hilo la machimbo palipotokea ajali hiyo lilikuwa limezuiliwa kwa muda kutumika
"Walikuwa wanachimba eneo ambalo limezuiliwa kufanyia kazi na waliingia kinyemela, walikuwa watatu, wawili wakafukiwa mmoja akatoka akaja akatoa taarifa ofisini na sisi tukaenda tukaanza kuwaokoa tumetumia siku nane tukawa tumewaokoa na kwa sasa wako hospitali wanaendelea vizuri," amesema mmiliki huyo.