Tetesi: Waliofukuzwa uanachama CHADEMA waanza kugawanyika

Huyu dada nilikuwa namkubali sana aisee... Lakini kaniangusha sana leo Halima wakuiogopa chadema kwamba katishwa hawezi kuhudhuria muito alioitwa na wenzake?? Yani kwamba chadema wanaweza kumdhuru Halima na wenzio?
Hii ni kama binti aliyewakosea wazazi na anaogopa kurudi nyumbani kuomba kwa wazazi
 
Ulitaka wazubae mgogoro ukue uwe km ule wa cuf? Walichofanya ndo kukomaa kisiasa... Hatuwezi fuga mapapa kwenye chama wanaojiamulia wanavyotaka! Hata ccm hawawezi kuendekeza huo ujinga!
 
HIVI wee ndio mshauri wao?
Kwa taarifa tu, lugha kama yako kuhusu upinzani/wapinzani haikuanza leo wala kwako.
Majisifu yako ya kitoto, hayana mvuto wowote kwa CHADEMA usipoteze muda wako kurudia rudia ulivyokaririshwa.
CHADEMA weshafanya uamuzi, nyie huko mtajuana mwende wapi kusini au mashariki au kokote kama kaa ni yenu hakuna haja kelele.
Wasalimie
 
Huyu dada amepambana sana
Leo watu wanajidai hawaoni effort zake.
Hata Mimi natamani mkulu ampe cheo.
 
Unachukua Miaka 15 kuijenga sifa yako na unachukua dakika 5 kuivunja

Noma sana
 
Kwani CCM wamekomaa nini sasa kisiasa wakati msaada wao mkubwa ni mbeleko ya Polisi, TISS na NEC
 
Hakuna Catch-22 hapo. Its sweet Covid-19, pure corona with all the trimmings. Kuna magumashi mengi mno. A failed, botched up, half-baked Amateur operation , at best.

Kuapisha kinyume na katiba, operesheni Nusrat inanuka mno. Haya mawili wala serikali , wala Bunge haijajibu.

Wanaongea juu juu tu. Ila kwa kuonesha msimamo imara, CHADEMA ime-retain heshima yake.
Unasema upinzani hawajakomaa. CCM ya 1977 na yenye mizizi ya TANU ya 1954, kwa chaguzi mbili, ule wa serikali za mitaa na huu mkuu wa 2020, imejionesha wazi kuwa ishakufa kama chama cha siasa, ila ni genge la Mafia. Imeaibisha kabisa historia nzuri ya TANU na ASP.

CHADEMA ndio wakomavu na wastaarabu. Kwa ccm hii ya Magufuli, genge la mafisi wa Serengeti lina afadhali
 
Mbona waraka ni wa mwandiko wa Pole Pole.
 
Halima Mdee anasema na nishukuru mwenyekiti wangu wa chama kwa kuturuhusu,... Aisee..!
Inawezekana alimaanisha kuwaruhusu kuondoka kwenye chama, maana m/kiti ndiye aliyesoma tamka la maamuzi ya kamati kuu kuwafuta uanachama. Na Bi Mdee alishafahamu kwamba kwa kitendo chao hicho lazima wataondoka tu.
 
Act au ccm kunawafaa
 
Nadhani katika hilo kundi kuna mmoja ama wachache sana kutaka kutumia umaarufu ama nafasi zao ndani ya chama kuendesha uasi, kwa lengo la kuungwa mkono na wengine wengi nyuma yao, lakini baada ya BAWACHA ambao ndio lengo kuu la kuwaingiza kwenye uasi huo kuonyesha msimamo tofauti, imeharibu mpango mzima na baadhi kutoka hao 19 kuona wameingizwa kwenye matope maana hata ukijinasua kwenye tope ukitoka bado itakuwa umesha chafuka.
 
Hii karata hata CCM hawaelewi waipindue vipi ionekane haina kona kona mingi
Wapanga mikakati ndani ya Ccm hawatumii akili. Hii issue ilikuwa very simple
Walitakiwa waongee na wabunge walio shiriki uchaguzi wakashindwa waende mahakamani. Hapo kwa vile mahakama zetu hivi sasa wana fanya kazi kwa maelekezo na sio kufuata sheri, basi mahakimu wangeelekezwa kuwapa ushindi walio fungua kesi asap. Hilo linge pita bila maswali. Lakini jili la kuigiza saini za watu hata mimi nalipinga..
 
Kukomaa katika lipi,kama chama kwa pamoja kila siku kinatoa tamko hawatambui uchaguz wala matokeo ma hawajachagua wabunge wa viti maalum tena wanaongea hadharani ,alaf wanatokea watu wanaenda tofaut na msimamo wa chama apo wa kulaumiwa hao waliofanya ilo jambo na wengine walikua wabunge karibu vipind vitatu wakomae nin tena
 
Ulitaka mimi nifanye nini kwa niaba yenu?
Ya kwako tu yamekushinda kuyafanya, itakuwa ya wengine? Huna unaloliweza zaidi ya kula na kulala kwa shemejio!
Bora unyamaze tu ili shemeji asimwache dadako ukakosa pa kumbonji! Mjini na kitaa pagumu ati!
 
Ushshangae Rais akateua baadhi yao kuwa wabunge. Na uwaziri wakapata.
Ila wapo wataoumia jumla.
 
Hata bila kwenda Mahakamani. NEC wangesema tu kuwa baada ya malalamiko mengi, wanahesabu upya kura zilizopigwa. Halima, Bulaya, Matiko, Ruge, Heche, Mbowe, Msigwa, Zitto, Ado na wengine wanatangazwa washindi na wasimamizi waliosimamia uchaguzi katika maeneo yao wanatumbuliwa ( lakini wanapewa kazi nyingine). Chadema kutokana ns kura zao kuongezeka wanapata viti zaidi vya wakina mama. ACT-WAZALENDO nao wanapata viti maalum. CCM wananaki kuwa na absolute majority lakini si huu upuuzi wa 90%.
Aidha, kura za mgombea wa urais zinapunguzwa mpaka anashinda kwa asilimia 66. Kazi inakuwa imekwisha.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…