#COVID19 Waliofunga shule kwa corona, maslahi ya walimu yatakuwepo? Je, wazazi hawatalazimishwa kulipa tena ada?

#COVID19 Waliofunga shule kwa corona, maslahi ya walimu yatakuwepo? Je, wazazi hawatalazimishwa kulipa tena ada?

Joined
Jul 11, 2020
Posts
66
Reaction score
145
Kabla sijaenda kwenye maswali zaidi niweke wazi kuwa, I have never bought any Conspiracy lakini najua attention ya dunia dhidi ya corona is greater than the real problem.

Corona kuwepo ni jambo moja, impact yake ni suala jingine, Idadi ya wanaopona ukilinganisha na wanaokufa inaoesha haja ya kufanya tafiti ya impact ya gonjwa hili kabla ya kutangaza kwamba ni janga la dunia.

Moja kati ya vitu vya kupima ni statistical significance ya tofauti ya miaka kabla ya corona na baada ya corona. Yaani tujue watu walikuwa wanakufa wangapi kwa mwaka, kwa miaka kumi iliyopita ili kuangalia trends zake, ambapo tutafananisha na vifo vilivyotokea kwa muda huu ambao corona ipo, kama mwaka unaweza kuwa shida tunaweza kuchukua vya miezi 15 kabla ya corona na 15 wakati wa corona.

Moja kati ya error ambayo ipo kwenye reporting ni kwamba inawezekana tumeongeza kuripoti vifo vya watu na kuvihusianisha na corona huku uhalisia ukiwa vifo havijaongezeka significantly.

So nasimama kusema, corona inaweza kuwepo lakini impact yake inalazimishwa kuwa kubwa ili kutisha watu, namna pekee ni kupima idadi ya vifo kwa miaka iliyotangulia.

TURUDI KWENYE SHULE
Shule moja jana imetangaza kufungwa kwa kuwa na mtoto mwenye corona, nimeangalia picha zake shule ina watoto wa kizungu, labda ni wazungu wameweka shinikizo hilo. Anyways, concept inakuja hapa

Miezi kadhaa iliyopita kipindi corona ipo juu, walimu wa shule binafsi waliumizwa kutokana na kutolipwa mishahara na hata shule ziliporudi wazazi walilazimishwa kulipa ada upya japo awali watoto hawakusoma kwa takribani nusu muhula.

Kwa wale waliofunga shule wamefanya jambo la maana sana, lakini je wamejipangaje kwenye maslahi ya walimu na wafanyakazi wa shule husika, na je wazazi hawatasumbuliwa kulipa ada, maana kama ni Corona ipo duniani kwa zaidi ya mwaka sasa, na kama shule zingefungwa maana yake ni hata sasa watoto wangekuwa nyumbani.

I prefer kujadili mambo kiuchumi zaidi.

Naenda kusolve another Mathematical Equation
 
Corona ipo wapi wewe.

Fanya mambo yako achana na hayo ma vitu ya kusadikika ambayo hayaonekani.
 
Corona ipo wapi wewe.

Fanya mambo yako achana na hayo ma vitu ya kusadikika ambayo hayaonekan
Acha ubishi mkuu! Ukianza kukosa uwezo wa kupumua uwahi mapema kuja kutuaga humu jukwaani.

Corona imerudi kwa kishindo. Na kwa Nchi yetu, hii ndiyo miezi yake!! Tahadhari ni muhimu kuchukua.
 
Back
Top Bottom