Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Mimi
Mnaojua hesabu hongereni sana, binafsi sikumbuki chochote nilichosoma kuhusu hesabu zaidi ya magazijuto.
Mimi hilo somo lilinikata kabisa kila nikijipendekeza wapi nikaona cha kuumwa kichwa nini
 
Mihesabu kama ya Trigonometric ratios (Tan, Cos na Sin), Calculus n.k. na mihesabu migumumigumu ya chuo kikuu iligunduliwaje?

View attachment 1963923

Yani mtu unasolve page nne ndio unapata jibu jamani!!! Sasa walifikiajefikiaje muafaka kwamba ukifanya hivi hivi ukaja hivi na hivi mpaka mwisho ndio mjibu huo umetiki?

View attachment 1963924

Kwakweli hesabu ni jambo la kushangaza sana. Hebu tupeni historia ya kugunduliwa hesabu mpaka leo. Na je, hakuna hesabu mpya zilizogunduliwa miaka ya karibuni?
Unaujua uchawi wewe
Ukichukua kitu hiki na kile na kile na hiki unapata hiki......uchawi ndio ulivyo

Kwangu mimi hisabati ni uchawi maana unapita mule mule kwenye kufanya hivi na hivi unapata jibu hili....
 
Namkumbuka mzee Pythagora ambaye Maaskari walimuua kwa sababu alikuwa amechora pembetatu mraba(Right-angled Triangle) barabarani na ameinamia kutaka kujua uhusiano kati ya mistari yake (urefu ) na kwa bahati mbaya hao majamaa(Askari) walikuwa wanapitisha Gwaride lao hapo. Pythagora aliwataka wasiukanyage mchoro wake bali wapite pembeni kidogo. Alipokataa kuwapisha na akawa mbishi wakamwua bila kujua alikuwa anasolve a2 + b2 = c2.
Hiki kisa nakijua leo, ngoja nikifuatilie. Asante mkuu.
====
Updates

Nimefuatilia kwenye vyanzo vyangu vya habari, nakukuta kumbe kila habari iliyokuwa na muhusu Pythagoras ilikuwa inatiliwa mashaka. Vivo hivyo, na habari ya kifo chake. Habari nyingi zinasema alichomwa moto akiwa kwenye nyumba na wenzake, kutokana na mtafaruku wa kisiasa, habari nyingine zinasema alitoroka janga hilo.

Mkuu, naomba chanzo chako cha habari hii, ya mtaalamu huyu kuuawa na askari.
 
form six nilikuwa natembea nimejaza Yale makaratasi ya kufungashia magazeti utazani muuza chumvi,kisa mihesabu ya kusolve mpaka page 3,daah.waligundua mihesabu migumu ambayo baadhi yake huenda kwa b8nadamu wa ss matumz yake hatujafka hata 10%, kumbuka waliogundua walikuwa na mipango mikubwa na hiyo mihesabu migumu ya 6 by 6 ,na ndo walishakufa kitambo na ndo maana hatuoni ugunduzi mwingine wa mihesabu migumu ,au mwendelezo wa kugundua au kukosoa !!!,wale watu sijui walitoka sayari nyngne tofauti na hii tunayoijua!!!!!!
 
Apply log mtu wangu. Utaielewa.... au tumia Chi square table of distributions😂😂😂
Mpe ushauri kwamba kama ikishindikana hapo, basi atumie Duncan Multiple Range Test.🙄🤣🤣
Hiki kisa nakijua leo, ngoja nikifuatilie. Asante mkuu.
====
Updates

Nimefuatilia kwenye vyanzo vyangu vya habari, nakukuta kumbe kila habari iliyokuwa na muhusu Pythagoras ilikuwa inatiliwa mashaka. Vivo hivyo, na habari ya kifo chake. Habari nyingi zinasema alichomwa moto akiwa kwenye nyumba na wenzake, kutokana na mtafaruku wa kisiasa, habari nyingine zinasema alitoroka janga hilo.

Mkuu, naomba chanzo chako cha habari hii, ya mtaalamu huyu kuuawa na askari.
Mkuu; Haiko wazi sana(ni ya kusadikika- myth) ; tulisikia kwa Teacher shuleni, lakini uki-Google kama swali " Was Pythagoras killed by a soldier?" utakutana na hiyo kitu japo wanaeleza kukataa kwake kukanyaga shamba la maharage!
 
Kila kitu kina kazi yake kama huna kazi nacho basi lazima ujiulize why unasoma na utaona tabu kujifunza. ni ajabu kuona watu wanamuachia mungu kuhusu kujua umuhimu wa math na kazi zake wakati simply unaweza google.

Mathematics ni njia moja wapo na labda tuseme njia kuu ya kusolve problems za physical world kwa njia yenye uhakika bila vibabaishi.
Ni mfumo wa logic na critical thinking.

So huu ni mfano mwepesi wa kuelewa lengo zima la hesabu na kutatua tatizo hadi kupata solution na nitaonesha nini kinatokea pale unapokosa uwepo wa hesabu.

Rafiki yako anapiga simu anakwambia tukutane mbagala rangi tatu! then anakata simu.
Je wewe utafikiria nini na utafanya nini? unaona kinachotokea unapokosa uwepo wa hesabu?
Mkutane mbagala rangi tatu saa ngapi au muda gani?
Mkutane mbagala rangi tatu lini?

Now hicho ndicho kinachotokea pale unapokosa hesabu ndani ya physical world.
Hayo maswali mawili ndio problems zinazohitaji solution na ukiweza tatua ndio utapata jibu sahihi la nini unatakiwa kufanya.

Lakini kama rafiki yako angetumia hesabu (exactness, kwa uhakika) basi wewe ungejua kwa uhakika nini cha kufanya. tuone nini kinatokea pale rafiki yako anapotumia hesabu.

Rafiki yako anakupigia simu then anakwambia tukutane mbagala rangi tatu, mwaka 2021, mwezi wa 10, alhamisi asubuhi, saa 3 na dk 45 sekunde 36.
Hapo wewe utajua kwa uhakika nini cha kufanya sababu ametumia hesabu na jibu kwako litakuwa clear bila vibabaishi vyovyote, labda uwe mvivu.

Sasa huo mfano ni wa problem ndogo ambayo haiitaji calculations nyingi. ndio maana wakasema hesabu ni mfumo wa logic na critical thinking.
Now kila formula ya hesabu inakuwa na kazi yake maalum ya kusolve tatizo fulani kwenye physical world na kupata jibu lenye uhakika.

Let say unataka kurusha rocket ipeleke satellite kwenye orbit.
huwezi ukafanya fanya tu then utegemee mambo yaende kama unavyotaka.
first itabidi ujue umbali wa kutoka hapa mpaka kwenye orbit?
ujue kiasi gani cha fuel utumie mpaka kwenye orbit?
ujue uzito wa satellite na uzito wa rocket?
ujue ni kiasi gani cha uzito rocket inaweza kubeba mpaka kwenye orbit?
ujue ni angle gani dunia inazunguka na angle gani unataka satellite yako ielekee?
ujue ni speed gani satellite inatakiwa iende ili isiangukie duniani?
ujue gravity ya dunia ina nguvu kiasi gani?
ujue ni speed gani inayotakiwa ili rocket iweze kutoka duniani (escape velocity)
ujue speed limit ya rocket yako?
ujue speed ya upepo na mambo yote kuhusu hali ya hewa?
ujue jinsi gani utaweza kucontrol air flow kwa kiasi gani ili rocket isizunguke au kupinduka juu chini?

Kule juu hakuna pita kulia alafu nyoosha kushoto geuka kulia tena fanya kama unarudi nyuma nk sababu kule juu ni empty space, hivyo hesabu ndio kiongozi wako especially spaceships zinapofanya docking.

Now hayo maswali yote yanahitaji majibu ili operation yako ikamilike lasivyo hakuna kitakachofanikiwa.
kizuri hayo maswali yote tayari yana formulas ambazo zinaeleza nini cha kufanya ili upate majibu sababu hayo maswali siyo ya leo watu walijiuliza hayo maswali miaka mia iliyopita na kupata majibu.
kizuri kila unapojibu swali moja unakutana na errors au maswali mengine mengi zaidi but hey! watu walishajaribu yote hayo miaka hiyo na kupata majibu sahihi, hivyo actually hesabu za leo ni rahisi sababu watu walishafanya na kupata majibu sahihi.
Kama unaona ni ngumu basi sababu hujui unachokitafuta na kwanini unakitafuta?

Watu au tuseme watu wote ukiondoa waafrika wavivu wa kufiri, walikuwa wakikutana na changamoto nyingi zinazohitaji solutions hivyo wakawa wanatumia mathematics au numbers kutatua chanagamoto hizo kwa uhakika na kila changamoto inakuwa ni ya kipekee hivyo wakawa wanatengeneza formula tofauti'tofauti kutatua aina fulani ya changamoto.
Na kila walivyozidi kuendelea wakawa wanazidi kugundua mengi zaidi.

Kwa Africans ni sahihi kuuliza hesabu za nini sababu hawazitumii popote zaidi ya kupatia vyeti na kuajiriwa lakini wenzetu wanazitumia kufanya ya kuitwa maajabu why? sababu wao wanatumia akili kufikiria na africans ni wavivu wa kufiri simple. wao walikuwa wanatumia vichwa vyao na akili zao kutafuta solutions na huku africans wakimuachia mungu au unataka sema mungu alishusha vitabu na formulas za rocket science?

Hivyo hakuna cha mungu kushusha hesabu wala fairy tales nyingine za aina yake ni uwezo tu wa akili za binadamu wenye uthubutu wa kufikiri. plain, short and simple.

So hilo ndio jibu sahihi.
 
Hesabu ni kipimo sahihi cha kupima uwezo wa mtu kufikiri, pia ukirejea mashuleni wanafunzi wanaolimudu vizuri somo la Hisabati( Mathematics) wengi wao hata matokeo yao ya mitihani ya NECTA huwa ni mazuri kuliko wazembe wa hesabu, ndo hao husoma combination za PCM, PMC,PGM,PCB,EGM,CBG,CBN ambao hulisaidia taifa ktk kazi za Uhandisi, Urubani ,Udaktari, Unahodha nk.

Hata kazi ya ufundi selemala na ushonaji nguo Kama mtu hajui hesabu atatumia materials nyingi kuliko yule anayezimudu vizuri, nenda kwenye biashara yule anayejua hesabu vizuri ni rahisi kuendesha biashara kwa faida.

Kwahiyo tuwahimize watoto wetu kupenda Hisabati.

Mathematics is our own language, let's speak it!!!
No, lengo la mathematics sio kupima uwezo wa mtu kufikiri.
Inavyoonesha hata wewe mweyewe hujui umuhimu, kazi wala lengo la mathematics.
 
africans ni wavivu wa kufiri simple.
Usi generalise kirahisi hivyo, Africans wanafikira za hali ya juu sana. Nakuhakikishia wamehusika kikamilifu katika mission nyingi za anga za mbali.
===
Unazo nondo lakini kukebehi wafrika halikubaliki.
 
Sioni matumizi ya hesabu kama trigono ratio au logarithim ktk maisha ya kawaida. Yaan zinatumika wapi?
Siku mkiwa mnabishana jengo gani refu kati ya PPF TOWER au Benki Kuu
Chukua kipima pembe (protractor) kwenye kompasi yako ya shule ya msingi
Nenda karibu na hilo jengo, simama na weka alama uliposimama
Piga hatua miguu kadhaa mpaka ulifikie jengo, (akisia kila hatua ni mita moja)
Rudi ulipoweka alama, na chukua kipima pembe na uweke kwenye jicho huku ukiangalia juu mpaka urefu wa jengo, nikuu ni nyuzi ngapi ukiwa unaagalia urefu wa jengo inawiana na kipima pembe.
Hapo tumia hiyo Trigonometry kama unaijua kutafuta urefu wa jengo,
Ubishi kwisha.....

1633560875832.png

1633560997154.png
 
Usiseme HUONI UMUHIMU, sema HUJUI UMUHIMU. Kila hesabu ina umuhimu wake hapa duniani, ukiona haina umuhimu ujuwe hukufikia level ya matumizi yake
 
Dah ila maisha hayako fair. nakumbuka A level natoka kwenye paper ya bam nawaambia washkaji sijaona swali ya kukosa. wakawa wananinanga ile pepa ilisukwa kiasi kwamba unampelekea mtu wa pcm anasanda ila huwezi amini nilipata 100% akati napiga pcb.
ajabu saivi natukanwa na waindi.
 
mkuu, michoro na maumbo mbali mbali katika nguo ulizo vaa ni Application ya TRIG kwa msaada wa matlab
 
Kila kitu kipo na kinatumika mahala pake,
Huko ulaya mathematics inatumika kwingi Sana

Sasa we umeajiriwa na Mo dewji kwenye kiwanda Cha sabuni Tena ni casual labour, ya duniani utayajuaje
 
Back
Top Bottom