Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
WALIOHARIBU BONGO MOVIE NDIO WANAHAMASISHA TAIFA STARS ISHINDE...
Kwa masikitiko makubwa jana nimeona kamati ya kuhamasisha timu ya taifa kushinda ikiongea na wandishi wa habari.
Nikajaribu kusikiliza walicho kuwa wakikiongea lakini sikuambulia kitu chochote cha maana kwa kuwa hakukuwa na lolote la msingi lenye kuhimiza na kuhamasisha timu hio kushinda zaidi ya kuomba watu wajitokeze kuujaza uwanja.
Niliwaona wasanii wa Bongo movies sambamba na waimbaji na machekbobu na watu wa kujikombakomba wakiwa kwenye meza za wageni watao zungumza na waandishi wa habari.
Hakukuwa na nguli yeyote wa Soka ambae aliwahi kuwika na kulitumikia taifa hili kwa nguvu zake zote, hakukuwa na mwamba yeyote wa Soka ambae angeweza kusimama na kuongea kitu cha soka na kueleweka.
Matokeo yake uhamasishwaji ukaongozwa na wababaishaji ambao wamefeli kwenye tasnia zao, wababaishaji ambao huyatumia matukio kuwa kama kick ya kuwarudisha kwenye chat.
Hili suala si la kulifumbia macho, ufike wakati sasa Soka liongozwe na kupigiwa debe na watu wa Soka, na muziki uongozwe na kupigiwa debe na watu wa muziki, kadhalika sinema zisimamiwe na watu wa sinema.
Hivi kweli kamati ya kuhamasisha wanamuita Sheta na kumuacha Sekilojo Chambua?
Kamati inamuita Le Mutuz na kumuacha Zamoyoni Mogella?
Kamati inamuita Steve Nyerere na kumuacha John Mwansasu?
Je Wema Sepetu ni nani katika soka, kiasi cha kumuita aje azungumze na kumuacha Muhamed Mwameja?
Kwanini wakina Salvatory Edward, Keneth Mkapa, Seleman Matola, Edibily Lunyamila wasije kuhamasisha mchezo ambao wameutumikia kama ofisi zao kwenye maisha yao mpaka waje hao watu wa tasnia nyingine?
Hivi kweli Wema akiulizwa ataje kocha msaidizi wa Stars anamjuwa?
Hivi Le Mutuz akiambiwa ataje kikosi cha Stars anakijuwa?
Watu wa soka hili ni tusi kubwa sana tunatukanwa.
Imekuwa ni wimbo sasa kuhamasishana watu kujitokeza na kujazana uwanjani, lakini hatuhamasishi wachezaji kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha timu inashinda na kufudhu.
Watu wa Soka Tufike kipindi tusiruhusu wahuni waongoze wala wasisimamie suala lolote linalo husu Soka.
Kila Mtu akaongoze tasnia yake na kuhakikisha inafanya vyema.
Naitakia kila la heri Taifa stars na naimani wachezaji watapambana kuhakikisha nafasi ya kucheza AFCON tunaipata.
Wachezaji wetu nyie ndio wokozi wetu, sisi hata tuujaze uwanja mpaka nje, kama nyinyi hamtokaza na kutumia mbinu sahihi za kuwafunga waganda basi ni kazi bure tu.