Walioiangusha Bongo Movies sasa wanaipigia debe Taifa stars...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
WALIOHARIBU BONGO MOVIE NDIO WANAHAMASISHA TAIFA STARS ISHINDE...

Kwa masikitiko makubwa jana nimeona kamati ya kuhamasisha timu ya taifa kushinda ikiongea na wandishi wa habari.

Nikajaribu kusikiliza walicho kuwa wakikiongea lakini sikuambulia kitu chochote cha maana kwa kuwa hakukuwa na lolote la msingi lenye kuhimiza na kuhamasisha timu hio kushinda zaidi ya kuomba watu wajitokeze kuujaza uwanja.

Niliwaona wasanii wa Bongo movies sambamba na waimbaji na machekbobu na watu wa kujikombakomba wakiwa kwenye meza za wageni watao zungumza na waandishi wa habari.

Hakukuwa na nguli yeyote wa Soka ambae aliwahi kuwika na kulitumikia taifa hili kwa nguvu zake zote, hakukuwa na mwamba yeyote wa Soka ambae angeweza kusimama na kuongea kitu cha soka na kueleweka.

Matokeo yake uhamasishwaji ukaongozwa na wababaishaji ambao wamefeli kwenye tasnia zao, wababaishaji ambao huyatumia matukio kuwa kama kick ya kuwarudisha kwenye chat.

Hili suala si la kulifumbia macho, ufike wakati sasa Soka liongozwe na kupigiwa debe na watu wa Soka, na muziki uongozwe na kupigiwa debe na watu wa muziki, kadhalika sinema zisimamiwe na watu wa sinema.

Hivi kweli kamati ya kuhamasisha wanamuita Sheta na kumuacha Sekilojo Chambua?
Kamati inamuita Le Mutuz na kumuacha Zamoyoni Mogella?
Kamati inamuita Steve Nyerere na kumuacha John Mwansasu?
Je Wema Sepetu ni nani katika soka, kiasi cha kumuita aje azungumze na kumuacha Muhamed Mwameja?

Kwanini wakina Salvatory Edward, Keneth Mkapa, Seleman Matola, Edibily Lunyamila wasije kuhamasisha mchezo ambao wameutumikia kama ofisi zao kwenye maisha yao mpaka waje hao watu wa tasnia nyingine?

Hivi kweli Wema akiulizwa ataje kocha msaidizi wa Stars anamjuwa?
Hivi Le Mutuz akiambiwa ataje kikosi cha Stars anakijuwa?
Watu wa soka hili ni tusi kubwa sana tunatukanwa.

Imekuwa ni wimbo sasa kuhamasishana watu kujitokeza na kujazana uwanjani, lakini hatuhamasishi wachezaji kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha timu inashinda na kufudhu.

Watu wa Soka Tufike kipindi tusiruhusu wahuni waongoze wala wasisimamie suala lolote linalo husu Soka.
Kila Mtu akaongoze tasnia yake na kuhakikisha inafanya vyema.

Naitakia kila la heri Taifa stars na naimani wachezaji watapambana kuhakikisha nafasi ya kucheza AFCON tunaipata.

Wachezaji wetu nyie ndio wokozi wetu, sisi hata tuujaze uwanja mpaka nje, kama nyinyi hamtokaza na kutumia mbinu sahihi za kuwafunga waganda basi ni kazi bure tu.
 
Ni upuuzi kumpa nafasi Wema na kuongea hapo na kuahidi yeye ya team yake watakuwepo Taifa, je hii itasaidia Stars kushinda?

Ni uzezeta kumleta Steve Nyerere hapo na kuleta masihara yake na maigizo yake wakati wachezaji wanataka kusikia nini wameahidiwa ili kupambana kufa na kupona.

upuuzi mdogo mdogo sasa umekuwa mwingi. unawaahidi washabiki ambao hawachezi kutakuwa na pati na vinywaji nusu bei je itasaidia kujenga morali ya wachezaji?

La msingi hapa kamati ilitakiwa iende kambini iongee na wachezaji iwawekee dau mezani kama 10 milioni kwa kila mchezaji endapo timu itashinda na kufudhu, uone watu watavyopiga kazi, waambie wachezaji kuwa mnakatiwa viwanja Chanika hapo heka kadhaa kwa kila mmoja endapo mkishinda hii gem, waambie wachezaji familia zao zinapewa medical and life insurance endapo tutatoboa na kuingia AFCON.

Sio unakuja tueleza upuuzi wa kufunga mitaa na kufanya pati....pati tunaeza fanya tu wenyewe hata tusipofuzu
 
WALIOHARIBU BONGO MOVIE NDIO WANAHAMASISHA TAIFA STARS ISHINDE...

Kwa masikitiko makubwa jana nimeona kamati ya kuhamasisha timu ya taifa kushinda ikiongea na wandishi wa habari.

Nikajaribu kusikiliza walicho kuwa wakikiongea lakini sikuambulia kitu chochote cha maana kwa kuwa hakukuwa na lolote la msingi lenye kuhimiza na kuhamasisha timu hio kushinda zaidi ya kuomba watu wajitokeze kuujaza uwanja.

Niliwaona wasanii wa Bongo movies sambamba na waimbaji na machekbobu na watu wa kujikombakomba wakiwa kwenye meza za wageni watao zungumza na waandishi wa habari.

Hakukuwa na nguli yeyote wa Soka ambae aliwahi kuwika na kulitumikia taifa hili kwa nguvu zake zote, hakukuwa na mwamba yeyote wa Soka ambae angeweza kusimama na kuongea kitu cha soka na kueleweka.

Matokeo yake uhamasishwaji ukaongozwa na wababaishaji ambao wamefeli kwenye tasnia zao, wababaishaji ambao huyatumia matukio kuwa kama kick ya kuwarudisha kwenye chat.

Hili suala si la kulifumbia macho, ufike wakati sasa Soka liongozwe na kupigiwa debe na watu wa Soka, na muziki uongozwe na kupigiwa debe na watu wa muziki, kadhalika sinema zisimamiwe na watu wa sinema.

Hivi kweli kamati ya kuhamasisha wanamuita Sheta na kumuacha Sekilojo Chambua?
Kamati inamuita Le Mutuz na kumuacha Zamoyoni Mogella?
Kamati inamuita Steve Nyerere na kumuacha John Mwansasu?
Je Wema Sepetu ni nani katika soka, kiasi cha kumuita aje azungumze na kumuacha Muhamed Mwameja?

Kwanini wakina Salvatory Edward, Keneth Mkapa, Seleman Matola, Edibily Lunyamila wasije kuhamasisha mchezo ambao wameutumikia kama ofisi zao kwenye maisha yao mpaka waje hao watu wa tasnia nyingine?

Hivi kweli Wema akiulizwa ataje kocha msaidizi wa Stars anamjuwa?
Hivi Le Mutuz akiambiwa ataje kikosi cha Stars anakijuwa?
Watu wa soka hili ni tusi kubwa sana tunatukanwa.

Imekuwa ni wimbo sasa kuhamasishana watu kujitokeza na kujazana uwanjani, lakini hatuhamasishi wachezaji kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha timu inashinda na kufudhu.

Watu wa Soka Tufike kipindi tusiruhusu wahuni waongoze wala wasisimamie suala lolote linalo husu Soka.
Kila Mtu akaongoze tasnia yake na kuhakikisha inafanya vyema.

Naitakia kila la heri Taifa stars na naimani wachezaji watapambana kuhakikisha nafasi ya kucheza AFCON tunaipata.

Wachezaji wetu nyie ndio wokozi wetu, sisi hata tuujaze uwanja mpaka nje, kama nyinyi hamtokaza na kutumia mbinu sahihi za kuwafunga waganda basi ni kazi bure tu.

Dah...Tangu mwaka huu uanze sijasoma andiko zuri kama hili...ni andiko lililojaa hisia...ni andiko linalofikirisha...soka ni mchezo unaopendwa duniani...lakini hapa kwetu inaelekea soka imeingiliwa...TFF hii kwa hakika imekosea mno kuteua kamati ya hovyo kabisa ambayo haijawahi kutokea...Yaani wanaojikombakomba na wababaishaji ndio eti wanahamasisha ushindi wa Taifa Stars...dah...Eee Mungu wee...
 
Tulia Wewe Hata Wasanii Wana Haki Ya Kuisapoti Timu Ya Taifa Kazi Ya Kuhamasisha Wachezaji Ni Ya Kocha Wasanii Wanahamasisha Mashabiki
 
John Mwansasu ana followers wangapi na Steve Nyerere ana followers wangapi?ikitumwa video ya kuhamasisha ya John Mwansasu wangapi watamtambua??Mmeanza lini kujipa haki miliki ya kundi flani tu kuhamasisha na kushangilia Stars kana kwamba Stars ni ya kundi hilo tu?

Anyway kitaalam kuna kitu kinaitwa Target Market,yaani soko au wateja walengwa!!Mnajuaje kama hiyo kamati imeamua kuwalenga wafuasi wa hao wasanii ambao wengi wao hawana habari na mpira???Watu wa mpira ambao wanamjua John Mwansasu na wengineo ni dhahiri watakuwa wafuatiliaji wa soka na wanajua wajibu siku ya jumapili.

Mwisho tusipende sana kukosoa kila jambo bila tafakari lakini pia tujenge utamaduni wa kuthamini mawazo ya wengine na kuyakubali mawazo mbadala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mkubwa huu kupitiliza...
WALIOHARIBU BONGO MOVIE NDIO WANAHAMASISHA TAIFA STARS ISHINDE...

Kwa masikitiko makubwa jana nimeona kamati ya kuhamasisha timu ya taifa kushinda ikiongea na wandishi wa habari.

Nikajaribu kusikiliza walicho kuwa wakikiongea lakini sikuambulia kitu chochote cha maana kwa kuwa hakukuwa na lolote la msingi lenye kuhimiza na kuhamasisha timu hio kushinda zaidi ya kuomba watu wajitokeze kuujaza uwanja.

Niliwaona wasanii wa Bongo movies sambamba na waimbaji na machekbobu na watu wa kujikombakomba wakiwa kwenye meza za wageni watao zungumza na waandishi wa habari.

Hakukuwa na nguli yeyote wa Soka ambae aliwahi kuwika na kulitumikia taifa hili kwa nguvu zake zote, hakukuwa na mwamba yeyote wa Soka ambae angeweza kusimama na kuongea kitu cha soka na kueleweka.

Matokeo yake uhamasishwaji ukaongozwa na wababaishaji ambao wamefeli kwenye tasnia zao, wababaishaji ambao huyatumia matukio kuwa kama kick ya kuwarudisha kwenye chat.

Hili suala si la kulifumbia macho, ufike wakati sasa Soka liongozwe na kupigiwa debe na watu wa Soka, na muziki uongozwe na kupigiwa debe na watu wa muziki, kadhalika sinema zisimamiwe na watu wa sinema.

Hivi kweli kamati ya kuhamasisha wanamuita Sheta na kumuacha Sekilojo Chambua?
Kamati inamuita Le Mutuz na kumuacha Zamoyoni Mogella?
Kamati inamuita Steve Nyerere na kumuacha John Mwansasu?
Je Wema Sepetu ni nani katika soka, kiasi cha kumuita aje azungumze na kumuacha Muhamed Mwameja?

Kwanini wakina Salvatory Edward, Keneth Mkapa, Seleman Matola, Edibily Lunyamila wasije kuhamasisha mchezo ambao wameutumikia kama ofisi zao kwenye maisha yao mpaka waje hao watu wa tasnia nyingine?

Hivi kweli Wema akiulizwa ataje kocha msaidizi wa Stars anamjuwa?
Hivi Le Mutuz akiambiwa ataje kikosi cha Stars anakijuwa?
Watu wa soka hili ni tusi kubwa sana tunatukanwa.

Imekuwa ni wimbo sasa kuhamasishana watu kujitokeza na kujazana uwanjani, lakini hatuhamasishi wachezaji kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha timu inashinda na kufudhu.

Watu wa Soka Tufike kipindi tusiruhusu wahuni waongoze wala wasisimamie suala lolote linalo husu Soka.
Kila Mtu akaongoze tasnia yake na kuhakikisha inafanya vyema.

Naitakia kila la heri Taifa stars na naimani wachezaji watapambana kuhakikisha nafasi ya kucheza AFCON tunaipata.

Wachezaji wetu nyie ndio wokozi wetu, sisi hata tuujaze uwanja mpaka nje, kama nyinyi hamtokaza na kutumia mbinu sahihi za kuwafunga waganda basi ni kazi bure tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali muhimu, hii kamati ni ya kuhamasisha timu au kuhamasisha mashabiki?

Nafikiri nikiipata jibu la hili swali basi nitafaham uelekeo wa hoja zenu!

- KANA -
 
Upo sawa mtoa mada eti shilole name alikuwepo na wamewaacha Watusi kama hamis kinye,Abdullah kibaden king
 
John Mwansasu ana followers wangapi na Steve Nyerere ana followers wangapi?ikitumwa video ya kuhamasisha ya John Mwansasu wangapi watamtambua??Mmeanza lini kujipa haki miliki ya kundi flani tu kuhamasisha na kushangilia Stars kana kwamba Stars ni ya kundi hilo tu?

Anyway kitaalam kuna kitu kinaitwa Target Market,yaani soko au wateja walengwa!!Mnajuaje kama hiyo kamati imeamua kuwalenga wafuasi wa hao wasanii ambao wengi wao hawana habari na mpira???Watu wa mpira ambao wanamjua John Mwansasu na wengineo ni dhahiri watakuwa wafuatiliaji wa soka na wanajua wajibu siku ya jumapili.

Mwisho tusipende sana kukosoa kila jambo bila tafakari lakini pia tujenge utamaduni wa kuthamini mawazo ya wengine na kuyakubali mawazo mbadala

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkongwe leo umeniangusha sana...
Hapa tulipofika hatuhitaji followers bali tunahitaji hamasa kwa wachezaji wakapigane kufa na kupona ili taifa letu likapate kufudhu AFCON.

Kama followers wangekuwa na umuhimu katika timu basi wamarekani wangekuwa mabingwa wa Dunia kila msimu kwa kuwa wana watu ambao wana followers weengi katika social media.
 
Swali muhimu, hii kamati ni ya kuhamasisha timu au kuhamasisha mashabiki?

Nafikiri nikiipata jibu la hili swali basi nitafaham uelekeo wa hoja zenu!

- KANA -

Kamati ya kusaidia Taifa Stars ifudhu...
 
Hii kamati inaitwaje?

Malengo yake ni yepi?

- Kama malengo ni kuhamasisha ushangiliaji siku ya mechi, sioni shida ya hiyo kamati.

- Kama ni kamati ya kuhamasisha wachezaji wacheze kwa jitihada na watupatie matokeo mazuri, hapo kuna walakini.
 
Kama ishu ni kujaza uwanja mm naimani waTz tunavyopenda mpira tungeujaza uwanja bila hata kutegemea ushawishi wa wasanii au mtu yoyote yule.
Cha msingi ni TFF kuchukua majukumu tu watengeneze mfumo mzuri na mipango ya muda mrefu katika. Mfano ndio tumeshinda hiyo jumapili upande wa pili kule Lesotho akampiga Cape verde ushindi unakua hauna maana yeyeote tena
 
Tanzania yangu

Wema awepo tu ,tukifungwa anajua cha kuwapa kwani anacho na wanakipenda saaana ,

Ila nimuhimu kuwakumbuka walio itumikia soka hata kama wawe wamechoka wangetoa maneno yao na kuwapa hamasa wachezaji wetu mana wanajua kazi ya uwanjani ilivyo ,lakini walishasahauliwa ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom