DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mahakama imeelezwa kuwa Said Issa Mohamed na wenzake wamewasilisha mapingamizi hayo wakipinga kuhusishwa kwa Lissu katika shauri hilo.
Awali, kabla ya kusikilizwa kwa hoja hiyo ya pingamizi, Jaji Hamidu Mwanga alitupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na CHADEMA, yaliyodai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Jaji Mwanga alibainisha kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa CHADEMA hazikuwa na msingi wa kisheria, akieleza kuwa Mahakama ilizingatia marejeo mbalimbali ya sheria kabla ya kufikia uamuzi huo.
Kutokana na mwenendo huo, Mahakama imepanga kutaja shauri hilo Februari 17, 2026, saa 2:30 asubuhi, ambapo itasikiliza mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya kuingizwa kwa Lissu na kuendelea na usikilizaji wa shauri kuu.