cnx
Member
- Apr 26, 2021
- 6
- 6
Hili ni swali linalohitaji ufafanuzi: kwa nini vijana waliyoitwa kwenye usaili wa Zimamoto kuanzia tarehe 15 Disemba 2025 hadi tarehe 20 Disemba 2025 hawakupata nafasi ya kwenda kwenye mafunzo, ilhali baadhi ya waliokuwa hawakuitwa kwenye usaili wamepata nafasi hiyo?
Mtu anajituma na kusafiri kwa siku mbili kutoka Lindi hadi Dodoma kwa ajili ya usaili, anazingatia vigezo vyote vinavyotakiwa, lakini PDF ya majina ya waliochaguliwa inapotoka jina lake halipo. Cha kushangaza zaidi, ukiangalia kwa makini orodha ya waliopata nafasi ya kwenda kwenye mafunzo, unaona majina ya watu wengine tu ambayo hata hayakuonekana kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.
Hali hii inanifanya nijiulize: je, watu hawa walifanya usaili wapi, au walitumia vigezo gani kupita na kuchaguliwa?
Nimejaribu kuweka PDF zote mbili (ya walioitwa kwenye usaili na ya waliochaguliwa kwenda mafunzo) ili kila mmoja ajaribu kuzipitia na kufanya ulinganisho wa majina.