Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Habarini wakuu, mukihitaji ramani nzuri msisite kututafuta kwa 0715477041, pia mwaweza tembelea link hii kujionea baadhi ya kazi zetu

1: kuset msingi..hii hutegemea na ukubwa wa nyumba..
2: tofali za chini huwa ni 250 japo wapo makauzu wanalipa 200
3: tofali za juu 300
4: zege mnaelewana kulingana na ukubwa wa nyumba
Asante, naomba makadirio tu ya kuchimba na kuseti msingi kwa nyumba ya vyumba 3 ya kawaida
 
Hongera sana mkuu. Naomba kuuliza, tofali za kulala kabla ya mkanda wa chini ( za msingi zilikua nnchi ngpapi na ziliteketetea ngapi?

Mkanda na linter zote umetumia nondo tatu au nne?

Naona kama umefanikiwa sana kupata vitu bei rahisi.

Ardhi yetu mfinyanzi 10 iliteketea kwenye msingi tu, ikijumuisha kifusi cha kuweka sawa.
Mimi pia nashangaa watu wamejenga 10 M hadi lenta wakati mimi yangu 10M imeteketea kwenye msingi pekee ambao umejazwa kifusi, nothing more. Msingi una kozi saba. Mimi boma bila kupaua imekula 20M, nyumba ina kozi 12 baada ya msingi kabla ya lenta na ina kozi nne baada ya lenta.
Mwisho wa siku nakubali, kuna vigezo vingi vinasababisha nyumba zenye idadi sawa ya vyumba kutofautiana gharama, mojawapo ikiwa ukubwa wa nyumba husika, nyumba kuwa na kona nyingi n.k
 
Dahh msingi wa kibabe sana huo . mkuu unaweza kutupia kapicha
 
Hiyo hapo mkuu
886936981.jpg
 
Mimi pia nashangaa watu wamejenga 10 M hadi lenta wakati mimi yangu 10M imeteketea kwenye msingi pekee ambao umejazwa kifusi, nothing more. Msingi una kozi saba. Mimi boma bila kupaua imekula 20M, nyumba ina kozi 12 baada ya msingi kabla ya lenta na ina kozi nne baada ya lenta.
Mwisho wa siku nakubali, kuna vigezo vingi vinasababisha nyumba zenye idadi sawa ya vyumba kutofautiana gharama, mojawapo ikiwa ukubwa wa nyumba husika, nyumba kuwa na kona nyingi n.k
Wee kozi nne baada ya linta why? Tatu hazitoshi?
 
Heshima sana wakuu,

Tumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kutupatia uhai mpaka sasa tunapoelekea kuukamilisha mwaka 2021. Najua kwamba wapo wengi walitamani.

kuanza ujenzi wa nyumba zao na ni ukweli usiopingika kwamba baadhi yao wameweza kuanza ujenzi, wapo walioishia katikati, wengine wamemaliza na huku wengine wakiwa hawajaanza kabisa.

Vilevile mwaka huu ume-trend zidi kwenye sekta ya ujenzi hasa kutokana na ukweli kwamba bei ya vifaa vya ujenzi mfano cement na bati ilipanda maradufu.

Kutokana na hayo naomba tupeane uzoefu kwa wale wote walioanza ujnzi wa nyumba zao mwaka 2021 ulifanikiwa vipi kuanza ujenzi na ni kwa namna.

gani ulipambana mpaka kufikia hapo.

Itapendeza zaidi kama utaweka specification za nyumba yako mfano vyumba viwili na sebule na gharama yake mfano milioni 30.

kwani mchanganuo huo utachagiza ari na morali ya wanabodi lakini pia utatuongezea mwanga na kutupa funzo kubwa la kusonga mbele na kutokukata tamaa.

kama sio kuahirisha ahirisha ujenzi wa makazi yetu tarajiwa.

Kwa heshima yenu nawasilisha
Huwa na utaratibu wa kila mwaka kuweka lengo moja tu la kutimiza,,ilipoingua 2021 lengo kuu ilikuwa ni nipate kiwanja na nijenge boma likamilike,,mwezi feb nilianza kwa kutafuta mafundi na kuwaelezea aina ya nyumba nayotaka ili wao wanipe ramani na gharama zao na wanipe hesabu ya ujenzi kuanzia msingi hadi boma likamilike....wapo mafundi waliokuja na makadirio ya juu ila nikafanikiwa kupata fundi ambae bajeti yake aliyinipa niliona itanifaa
Nyumba ya vyumba vinne(kimoja master)choo na bafu,jiko dining,sebule na baraza mbili...gharama zake za kujenga zilikuwa nitamlipa 1.5 M akaniandikia material ya kununua yote,,basi kuanzia mwezi wa tatu nikaanza nunua matofali Elfu 3(nchi 6 ya msingi mia tano na ya boma 2500) nikakamilisha tofali mwezi wa tano...mwezi wa sita nikaanza nunua nondo,mawe,kokoto,mchanga,tank la maji,na sementi mifuko 100 hili nikakamilisha mwezi wa saba nikaanza jichanga sasa kupata 1.5 ya fundi ambapo ndani ya mwezi nilikuwa nimeikamata nikasema nitafute balance ya 1M kwaajili ya lolote la ziada litakalotokea kufika sept 1 kila kitu kilikuwa na tayari na nikamuita fundi akaanza ujenzi kwa kasi hadi boma likakamilika....
Lengo la mwaka huu ni kupaua na kufanya finishing nihamie,,tathmini ya fundi katika upauzi ni 4.5 M ila kwa mimi nimeamua niweke 5 M ndo naichanga hapa najua nikishapau haya mengine yataendelea mdogo mdogo hadi desemba nitaleta mrejesho tena hapa..

INSHALAAH
 
Nyumba ya vyumba vinne kupaua 4.5 M tu? Au hiyo ni gharama ya ufundi tu sijaelewa.

Sent from my vivo 1938 using JamiiForums mobile app
 
Karibu. Ntakachokushauri uongeze kidogo ukubwa wa vyumba vile viwili.

Pia kwenye jiko nilifanya marekebisho.
Store niliisogeza isiguse ukuta ili kuwe na mwanga jikoni.

Pia niliweka mlango wa mbao wenye vile vioo vinapitisha mwanga hafifu ili sehem ya maliwato na kuelekea vyumbani pasionekane mtu anapokua sebuleni.

Blue ndio eneo la jiko
Nyekundu eneo la store
Mstaro wa kijani badala ya kuwa wazi, nikaweka mlango wenye kupitisha mwanga
View attachment 2078110

View attachment 2078111
Mkuu The Monk naomba msaada wapi naweza pata hiyo mikanda ya gypsum kwa ajili ya kuweka papi kwenye flash za milango kama ulivyo weka wewe

Msaada wako tafadhali
IMG_20220118_214315.jpeg
 
Back
Top Bottom