Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Kwahiyo umetumia miezi 36 kwenye ujenzi,
Na ambapo kila mwezi ulikuwa unatumia 2000000 ambayo ni asilimia 30% ya mshahara wako, hivyo mshahara wako utakuwa ni 7000000...
(sijui kama nipo sahihi)
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Hahahahahahaha
 
Kama ni rahisi sasa mkuu mbona hujajenga?Anyway,mimi nimejenga nyumba wala sio moja na kiukweli nataka ujenge.Ila siwezi kukuficha.Ujenzi unahitaji kujinyima,uvumilivu na fedha,labda kama wewe ni mzee wa shortcuts(ngada,madili au fisadi).
 
Sio kweli, mbona mimi huwatia moyo sana?
Ujenzi ni rahisi mno hasa ukiwa na kiwanja. Ukiwa hata na 300,000 inafanya kazi, unajenga kwa awamu sawa na nguvu yako hatimaye unaingia kwako.
Watu wasiogope kujenga
 

Hiyo ni gharama ya msingi na ukuta tu mkuu
 
Hahaha sio kilamtu awe na nyumba wengine tubaki kuwa wapangaji
 
Siyo nyumba peke yake, chochote binadamu anachofanya hupenda kujikweza nacho, na kuwakatisha wengine tamaa...



cc: mahondaw
 

Ushauri wako huu ndio ambao nimekuwa naufanyia kazi. Sasa mimi nafanya tu survey ya maeneo yanayofaa kwa mimi kujenga, huku nikifuatilia gharama ya ujenzi na alternatives.

Mfano kuna jamaa mmoja aliniambia yeye amejenga nyumba yake kwa kutumia mafundi aliowatoa kijijini, hii yote ilikuwa ni kuepuka mafundi wa mjini ambao ujanja ni mwingi ukichanganyikana na wizi. Nyumba imejengwa vizuri utadhani hao mafundi wana degree za ujenzi kutoka Holland.
 
Jenga tu mjengo wako mkuu, hakuna anayekuzuia
 
Nimekusoma mkuu hapo sasa kikubwa nilichokiona ni kila mtu ajenge kutokana na uwezo wake na si kulalamika kuwa ujenzi si gharama au ujenzi ni gharama.
Mkuu hapo sio tu kujenga kutokana na uwezo, ameonyesha pia kwa sababu fulanifulani, mfano kutokuwa na taarifa sahihi na kutokufanya uchunguzi wa kina, unaweza kutumia mil 100 kujenga nyumba ambayo mtu mwingine ameijenga katika eneo hilohilo ulipojenga wewe na factors zingine kubaki constant kwa mil 50 tu.
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Eti? Wapi huko tuhamie? Vyumba vya size gani? Kwa materials gani? Weka BoQ mezani.
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Never on earth!
 
Hongera sana mkuu!

Mimi naamini sana katika kuwa mvumilivu, kusaka taarifa sahihi ikiwemo kuwasikiliza watu wote haijalishi wanakufurahisha ama lah! Kwani kwa kila mmoja kuna kitu utapata kujifunza.
 
Wajenzi wengi wanapenda kupandisha gharama
 
duh hizi hesabu zako sijui
 
Weka pamba masikio, halafu cheza muziki...usiogope maneno ya watu.
Utageuka KIBWEKA...[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kucheza Muziki usio sikiliza sauti na ALA...

Umekwisha weka PAMBA Masikioni..

Unategemea nini...!!?
Unamaanisha hutaki kusikia hata USHAURI wa Mafundi...!!
 
Ina maana mpaka unaogopa maana yake hujachukua uamuzi wa kujenga hivyo unapokwenda kuuliza kwa jirani akakuambia kujenga nyumba ni gharama unachukulia kama anakutisha kumbe anakueleza ukweli ili sasa wewe mwenyewe unatakiwa uumuulize alifanyaje mpaka akajenga ndipo na yeye atakuambia njia alizopitia ikiwepo na kununua vifaa duka moja kuanzia msingi mpaka kufikia hatua ya kujenga urafiki na kuanza kuchukua vifaa na kulipa mwisho wa mwezi pamoja na kuchagua fundi mzuri.

Lakini kingine pia ujenzi ni hatua hasa kwetu wenye maisha ya kuunga unga maana kuna wengine anataka akinunua kiwanja na ajenge palepale (ndo pale unapokuta mtu anasubiri zifike 20million ndo anunue kiwanja kumbe hata kama huna mpango wa kujenga kiwanja kununua iwe ni lazima ili siku ukiona wakati umefika au ela zimekutembelea ni kufanya utekelezaji

Kwa ujumla hakuna anaetishwa ila ni kuelezana ukweli though ni ngumu mtu kukupa figure zote hasa kama sio rafiki maana kuna wengine sio wajenzi zaidi ya kupekuapekua mambo ya watu......mtu mwenye nia ya kujenga huwa haulizi gharama ya kujenga nyumba ni kiasi gani bali huuliza idadi ya vifaa vinavyohitajika kujenga nyumba pamoja na ufundi ili mwenyewe sasa akapige hesabu kulingana na aina ya material anayotaka maana kuna bati la 12,000 mpaka 50,000 na yote ni mazuri na size ni moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…