Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Gharama ya chini shilingi ngapi?
Nguvu zako tuu. Unakata miti unafyatua tofali bila cement, unachoma, unakata nyasi unajenga mwenyewe chumba na sebule unaezeka nyasi unakaa shambani. Ndo gharama ya chini. Ya juu haijulikani.
 
Kweli mkuu
 
Labda niombe mwenye uzoefu anipigie hesabu rough, nyumba ya vyumba 4, sebule na jiko inakula tofali za kuchoma ngapi, bati za kawaida ngapi na simenti+ ufundi
 
dahhh!! nikiona hayo mamilioni mnayosema eti ndo gharama ya chini navurugwa tumbo, ama hakika ujenzi noma, ila kufikia mwaka 2020 lazima niwe kwenye mjengo wangu mzuuuri!!
Mkuu vipi tayari una mjengo wako mzuriiii???
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Sasa mln 20 sio gharama kubwa?
 
Hakuna quality yoyote kwa 16 mln,sema nyumba hiyo Ina ukubwa gani na weka quantities na quality ya materials hapa tuone ,au kiwanda Cha kila kitu anachoyeye?
 
Na huku ndo kwenye gharama sio kule kwenye kupanga tofari, mi nilinunua vifaa vya umeme 2m nikavibeba kwa bodaboda yaani vyepesiiii
[emoji23] ulitaka viwe vizito kulingana na hela mkuu
 
Sasa wewe kwa gharama hiyo afu kwa nyumba ya bedroom 2 huoni umeingiliwa,kwamba with the same cost ungeweza kujenga ya vyumba 3 ,unit cost ingekuwa ndogo
 
Sasa wewe kwa gharama hiyo afu kwa nyumba ya bedroom 2 huoni umeingiliwa,kwamba with the same cost ungeweza kujenga ya vyumba 3 ,unit cost ingekuwa ndogo
Huwa simuelewi mtu anaejenga nyumba ya kuishi ya two bedrooms kwa kigezo cha kukwepa gharama. Gharama ya kuongeza hiyo room moja haipishani sana kwenye grand total ya ujenzi unapokamilika.
 
mi nimejenga vyumba 3 kwa m6 na msouz kabisa na mageti [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
we umenena,mi nimejenga hata m7 haijafika na nikitaka kuhamia nahamiaaa nnitamalizia nikiwa humuhumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…