Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Ama kweli la kuvunda halina ubani. Yamesikika mengi kuhusu ugaidi na ufwedhuli wa wapalestina na HAMAS.
Kwamba HAMAS ni wauaji, wabakaji, magaidi, wenye kutumia mahospitali kama vituo vya kijeshi, wanyama wasiostahili kuishi duniani na eti kuwa walaumiwe wao kwa vita hivi huko Gaza.
Kwenye mkutano wao na baraza la vita ambao amekuwa akiukimbia kwa muda mrefu, waliokuwa mateka Gaza wamemjia juu waziri mkuu huyu mwongo mwongo sana. Ya kuwa kumbe ni jongo, lisilokuwa na huruma wala kuyajali yakiwamo madhila ya mateka wanaobakia Gaza.
Kwamba jongo jongo hili halifai hata kuwepo madarakani. Liondoke, nchi iendeshwe na wenye kujali ustawi wa watu wakiwamo hata wasiokubaliana nao.
View attachment 2834459
Barua za shukurani toka kwa waliokuwa mateka kwenda HAMAS zimeonekana. Afya ya miili ya mateka miezi 2 wakiwa kifungoni wengine na vijibwa vyao zimeonekana. Shuhuda za mateka kuwahusu HAMAS zimesikika.
Natenyahu na tuhuma zake mpya kuwa HAMAS walibaka, ila waliobakwa walikufa, hizo labda kama ni za kuwaambia mbuzi.
Kwa hakika waliokuwa mateka na wasikilizwe!
Wapalestina Gaza wagaragazwa wenzao wanaangalia tu. Huu ni unyama
Inashangaza sana kuwa binadamu sasa wamekuwa na roho za kinyama sana kwa sababu wanyama ndio ambao mwenzao akiliwa wanakuwa na msaada mdogo sana japokuwa kwa umoja wao wangeamua wangeweza kumuokoa. Kinachotokea Gaza kinalingana sana na unyama.Kiwango cha vifo vya wapalestina na kujeruhiwa ni...