Waliokuwa na bidii na elimu lakini wapo mtaani wanadharaulika kwakuwa jamii iliweka matarajio makubwa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ni lile kundi la watu ambao tulisoma nao shuleni na vyuoni, walikuwa serious sana na elimu na waliweza kuwa na matokeo mazuri sana, wengi walisifika kwa kuitwa majina maarufu kama vipanga.

Katika fikra za wengi hawa walikuwa wanaonekana tayari wana future nzuri maana wakimaliza tu elimu zao basi wana maisha

Kiukweli yalikuwa ni matarajio makubwa sana lakini kwa uhalisia mambo yapo tofauti kabisa na ndio maana wapo ambao wapo mitaani kwa kukosa ajira au kukosa mitaji.

Changamoto kubwa wanayoipata ni kwamba tayari walijizolea umaarufu wa kuwa na uwezo mkubwa darasani hivyo kila anaekutana nae anajua ana bonge la kazi au cheo shirika flan na lazma aulize ili kuthibitisha. wengine masnich tu anajua kila kitu lakini anauliza makusud ili tu amtibue.

Basi baada ya hapo kinachofuata anaweza kudharaulika sana ama kuonewa huruma sana kama mtu mgonjwa asiejiweza maana alitarajiwa afike mbali sana kwa juhudi zake ila hakuna alichoambulia, mbaya zaidi katika kundi la waliomdharau hilo kunaweza kuwa na wenye ajira au biashara zao basi wanasambaza sumu kwamba elimu si kitu kwa kumfanya mwenzao awe mfano.
 
Mhubiri 9:11

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
Elimu ya darasani sio elimu ya mtaani.
Darasani unafundishwa kukariri, mtaani ni elimu kwa vitendo
Uongo inattegemea ulichosoma. masomo ya sayansi hakuna kukariri lazima uelewe ulichosoma
Degree za Arts zifutwe

Misomo ya Arts ni aibu kwa nchi ndio inazalisha watu wa kukariri huwezi soma digriii ya engineering au udaktari ukafaulu kwa kukariri

Na huwezi soma combination za sayansi kama PCB, PCM ukafaulu kwa kukariri
 
Tunahitaji wakalimani, wanasheria, HR’s nk hawa wote hawasomi sayansi.
 
hizo degree, zifundishwe level ya masters kwa anayetaka sababu Hata sasa hivi mwenye degree ya sayansi huwa ruksa kuzisoma level ya masters degree au postgraduate Diploma Digriii za Kwanza ziwe sayansi tu ila anayetaka kwa hiari yake ruksa ila asibwate baadaye kuwa kasomeshwa masomo ya kukaririshwa digriii ya kwanza
 
Uongo inattegemea ulichosoma. masomo ya sayansi hakuna kukariri lazima uelewe ulichosoma
Degree za Arts zifutwe

Misomo ya Arts ni aibu kwa nchi ndio inazalisha watu wa kukariri huwezi soma digriii ya engineering au udaktari ukafaulu kwa kukariri

Na huwezi soma combination za sayansi kama PCB, PCM ukafaulu kwa kukariri
mkuu yale ma arrhenious law yanaeleweka kweli?? Mfumo wa elimu ya kibongo n wa kukaririshwa mkuu, hakuna kuelewa jambo.

Hata huko udaktarini pia n ukaririshwaji wenye ahueni. Kama ulisoma huo udaktari bila shaka ulipitia ishu kama drancuculus medinences.... Hawa microorganisms ulikaririshwa na si kuwaelewa.
 
Percent ya kukariri ni ndogo huwezi linganisha na mtu aliyesoma digriii ya history au sheria au administration au uhasibu nk
Sehemu kubwa lazima uelewe kwenye digriii ya udaktari
 
Uongo inattegemea ulichosoma. masomo ya sayansi hakuna kukariri lazima uelewe ulichosoma
Degree za Arts zifutwe

Misomo ya Arts ni aibu kwa nchi ndio inazalisha watu wa kukariri huwezi soma digriii ya engineering au udaktari ukafaulu kwa kukariri

Na huwezi soma combination za sayansi kama PCB, PCM ukafaulu kwa kukariri
narcissist arrogant
 
Mhubiri 9:11
[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
AMINA
 
suala ni kukariri. Hio percent unaipimaje??
inapigana na soko la ajira mtaaani. Waende mtaaani mtu kasomea digriii ya engineering ya umeme, ujjenzi nk Halafu linganisha na huyo aliyesoma masomo arts uone demand ya jamii inamhitaji soko la ajira yupi kwa wingi huyo aliyekariri digriii ya sheria au administration na masomo ya Arts ?

Ndipo utajua jamii mtaani hawahitaji degree za kukariri!!! ! Digriii za kukariri Hata uswahilini hawazihitaji
 
hizo degree, zifundishwe level ya masters kwa anayetaka sababu Hata sasa hivi mwenye degree ya sayansi huwa ruksa kuzisoma level ya masters degree au postgraduate Diploma Digriii za Kwanza ziwe sayansi tu ila anayetaka kwa hiari yake ruksa ila asibwate baadaye kuwa kasomeshwa masomo ya kukaririshwa digriii ya kwanza
Hivi aliyesoma civil engineering anaweza kusoma masters ya sheria😟😟
 
Ndio anaanza na postgraduate Diploma ya law Halafu anaingia masters Degree.
yeyote mwenye digriii aweza soma masters ya law kupitia njia ya postgraduate Diploma na akawa hadi wakili

Pia law degree Hata mwenye PCM au PCB aweza jiunga na digriii ya kwanza ya Law mbona wako kibao
 
Ila bwana inategemea unasoma kitu gani? Kuna dogo kasoma marine huko kamaliza novemba, februari kala shavu huko umangani. Pesa aliyokusanya miye nikichukua mkopo nalipa miaka mitatu au mitano.
 
Back
Top Bottom