Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Nadhani wote tunawakumbuka wale wabunge 19 walioingizwa bungeni kinyemela kwa tiketi ya CHADEMA huku chama kikiwa hakitambui uwakili wao.
Yaliongelewa mengi sana, kesi ikaenda mahakamani, danadana mpaka sasa, wakakingiwa kifua na Spika na mifumo mingine ya maamuzi, kumbe ilikuwa ajenga tu.
Sasa mwaka wa uchaguzi umefika, chamani hawatakiwi na chama kimetoa msimamo hakishiriki uchaguzi, tamaa zao za madaraka wakajikuta wanahamia CCM dakika za lala salama maana wasingeweza kufanya hivyo wakiwa bungeni.
Ngoma ishakuwa ngumu, CCM kuna makada pia wanaomezea mate ubunge, haiwezekani uhamie chamani halafu upewe ridhaa kirahisi hivyo, badamu batamwagika.
Yangu macho tu.