Tetesi: Waliokuwa wapangaji wa NIC Mikocheni na Masaki wafukuzwa bila kupewa notice

Tetesi: Waliokuwa wapangaji wa NIC Mikocheni na Masaki wafukuzwa bila kupewa notice

wanabodi.

Shirika la Bima la Taifa limewafurusha bila hata kuwapa notice wapangaji wake huko masaki na mikocheni siku ya alhamisi wiki hii.

Tukio hili lilitokea siku ya alhamisi mchana kuanzia saa 8:00 mchana.
ilivyokuwa.

Shirika la Bima liliuza nyumba zake kwa PPF huko nyuma. PPF wakawa wanahitaji nyumba zao wapangaji hawa walikuwa wanaenda mahakaman kuweka zuio la kuhamishwa hapo.

Shirika la bima likawa halipati pesa toka kwao kutokana na kuwepo kwa kesi ya msingi.

Rais Magufuli aliitisha kikao cha siri na mkurugenzi wa shirika na kuwataarifu wafanyakazi wa bima kuwa uhamishwaji ufanyike kwa dharura bila notice wala kuandikwa popote.

Walivamiwa na askari wenye silaha za kivita hapo Alhamisi na ni muda ambao mahakama ilikuwa imemaliza shughuli zake.So ilikuwa vigumu kuweka zuio.
wapangaji hawa wakiwemo majaji, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watoto wa vigogo wameisoma namba.

Polisi walikuwa 46 na Yono walikuja na mabaounsa pale.

My take: Uvunjifu huu wa haki za kiraia ni mpaka lini jamani?
Wajenge za kwao,hata wewe kwenye nyumba yako una haki ya kumtimua mpangaji wako anayeshindwa kutimiza masharti,kwanini ung'ang'anie nyumba isio yako?au sababu ni nyumba za shirika la umma?
 
" Waambie mjini shule wasitamani vyote vimelipiwa,
Kama wapenda vya bure leta sahani na utapakuliwa "
Ray vanny in pre hook -
( fresh remix )
 
Hii kelele uliopiga humu hailingani na kilio cha uchungu wa wale maskini waliovunjiwa nyumba zao morogoro road.

Unalalamika nini na wakazi wa masaki na mikocheni. Hebu wakati mwingine uwe muelewa wa kutofautisha matukio ya kugusa hisia. Hawajaonewa kama unavyohisi hao wameharakishwa kuondoka. Judge mzima awe alikuwa hajui kama hili litamtokea basi huyo siyo judge ni mlinzi tu wa kampuni binafsi katika hizo mahakama zetu.

Wakome
 
Huyu ndugu arudishwe darasani. Huenda hafahamu kuwa alipoapa KUILINDA na KUITETEA KATIBA haikuwa katiba ya CCM.
 
Mpelekee yule askofu awatetee hawa wanaotaka kuishi bure
Unahitajika tena kwenye kipindi cha XXL ukatoe pumba tena.
Maana toka kianzishwe wewe ulivunja rekodi kwa kubwabwaja nje ya mada
 
Sasa wangekaa bure mpaka lini kwa kisingizio cha mahakama?Acha watimuliwe bwana
 
Hadi majaji wametolewa vitu ?

Duh ! Yule aliedhani "hagusiki" wala "hashikiki" leo kashikwa. Tena pabaya kweli kweli
 
utaolewa dadangu usipende vya bure
Ningekuwa KE kuolewa ni heshima kama ulivyowahi kuolewa wewe. Ila ni fedheha kuachika na kuwa chakula cha wengi mjengoni kama ulivyo.
Rekebisha tabia hujachelewa bado na umri unakuruhusu ku change behavior
 
Rais Magufuli aliitisha kikao cha siri na Mkurugenzi wa shirika na kuwataarifu wafanyakazi wa bima kuwa uhamishwaji ufanyike kwa dharura bila notice wala kuandikwa popote.
Na wewe ulikuwa mjumbe kwenye hicho kikao? sasa kilikuwa cha siri, hizi taarifa umezipataje?
 
Wakati mwingine watu wanatumia mahakama kama kichaka cha kujificha hasa kwenye kesi za nyumba....ukitaka kumtoa mtu anawahi kuchukua court order hadi shauri likamilike....sitetei hiki kitendo ila kuna nyakati ni bora kupiga hii short cut
 
Hawa serikali sina hamu nao....kila nikikumbuka hasira zinapanda though imepita miaka 7 tokea watupige tukio kwenye nyumba
 
Ungesema tu silaha ingetosha/ ulivotumia silaha za kivita umeonesha aina flani ya chuki na uchochezi alafu kama ulifanikiwa kugundua kikao basi hakikua cha siri,
 
Back
Top Bottom