Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fafanuatatizo kila mtu anavutia kwake
nakataa kwani mitihani ya 2010 kushuka maswali yalikuwa yanarudiwa sana hata wewe shahidi hivyo aliye solve past papers ndiye aliefaulu,,1.7 zilikuwa za kumwaga na vijana wengi wa govn walikuwa wanakariri sana almaarufu kumeza,,,hivi sasa mtaala sio content based bali competence ka hujui kaulize necta,,na hii ndo ilifanya 2011 na 12 wafeli kwani waliikuta wakiwa form 3 na 4,,,vitabu vya sasa (kuanzia 2012) ni bora na competence based,,,masuala ya kukariri hayahitajikini tena bali uelewa wako wa mambo,,,
Bravo!Mi ni msomi,niliyemaliza form four miaka ya 2007,2006,2005.........
Mwaka 2007 ulikuwa ni highest peak kwa ufaulu na baada ya hapo mambo yalianza kuvurugika sana, mambo mengi yanachangia.
1. Walio maliza 2008 kama mnakumbuka walivurugwa na Mungai (hawa ni watu wa physics with chemistry.
2. Watu wa 2009 hawa hawakuwa na mtihani wa form two, wasiojiweza wengi walifika form four.
3. 2010 kulikuwa na uchaguzi wa kitaifa, kila mtu alikuwa bize na siasa, kama mnakumbuka mwaka huu nia halisi ya mgomo wa walimu ili wapandishiwe mshahara ilionekana.
4. Mwaka 2010 pia watoto walilipiwa ada ya mtihani na serikali, kwa hiyo ni lazima serikali ifanye kila linalo wezekana.
5. Mwaka 2011 hawa watoto pia hawakuwa na mtihani wa form two, na mgomo baridi wa walim uliendelea kushika kasi.
6. Mwaka 2012 mgomo wa walimu uliingia hadi vijijini na kuanza kuingia mioyoni mwa walimu na mwaka huo huo kulikuwa na mgomo dhahili wa walimu japokuwa ulikatizwa.
7. 2012 huu mwaka licha ya kuwa na mgomo dhahili wa walimu, pia mwaka huu kulikuwa na sensa iliyo chukua mwezi mzima, what do you expect from these two?
8. Mwaka 2013 up to date mgomo wa walimu (mgomo baridi) umeingia uvunguni mwa mioyo ya walimu, na hivi sasa nao wamefunga EFD/LUKU kwenye ufundishaji siku hizi walimu wanasema FUNDISHA KADRI UNAVYO LIPWA (FUKU).
9. Kuna sababu zingine nyingi, kama miundombinu mibovu, mazingira yasiyo rafiki katika ufundishaji, na nyingine nyingi.
10. Slogani mpya ya serikali ya "SIASA KWANZA ELIMU BAADAE" nayo imechangia kwa kiasi kikubwa, kusema kweli wakuu wa shule wanapata tabu sana na hawa watu waitwao madiwani.
Mie ni hayo tu wandugu, i stdand to be corrected.
mkuu hapo kwenye namba.1 na 2 umedanganya
mm nimemaliza mwaka 2009,cc ndo 2likuwa wahanga wa physics with chemistry na 2lixoma hl somo 2kiwa form one mwaka 2006
darasa le2 ndo lilikuwa la mwisho kufanya mtihan wa form two mwaka 2007 na waliofel walikarr darasa
waliomaliza mwaka 2008,ndo wa kutiliwa mashaka kwan mitihan yao yote ilivuja na mingine kuokotwa masokon na stend,hisabat iliahirishwa lakn still ilivuja
mwaka 2009 wazir wa elim kipind icho j4 maghembe aliapa kutembea uchi kama mitihan ingevuja tena na kwel cha moto 2likiona kwan 2lifaulu kwa nguvu zetu wenyewe
mwisho madarasa yaliyopitishwa form two bila mtihan n kuanzia 2010 mpaka 2013
Nimegundua ubora wa elimu hapa TZ,ulianza kushuka miaka ya 2008, kama tunakumbuka kipndi hiki(kikwetism) mitihani ya taifa form 2 na form 4 ilivuja mno, Madogo wengi walitusua kwa kwenda shule za vipaji maalum. Miaka ya hapa kati 2009,2010,....,...2012 elimu yetu bado ilikuwa ikilegalega. Matokeo ya mtihani form iv 2013,SERIKALI imeamua kuwabeba wanafunzi na kujiriDHIsha kuwa inatekeleza sera ya BRN. Kwa maelezo haya mi naona msomi wa mwisho kumaliza form IV nchini TANZANIA ni yule aliyemaliza miaka ya 2007,2006,2005....... Hawa wa miaka ya 2008,2009,........ ni wasomi wa kupewa maksi na serikali! Au ninyi mnaonaje wakuu?
kweli kabsa,form wa mwisho ni wale wa 2007 tu,kuanzia 2008 hapo majangaNimegundua ubora wa elimu hapa TZ,ulianza kushuka miaka ya 2008, kama tunakumbuka kipndi hiki(kikwetism) mitihani ya taifa form 2 na form 4 ilivuja mno, Madogo wengi walitusua kwa kwenda shule za vipaji maalum. Miaka ya hapa kati 2009,2010,....,...2012 elimu yetu bado ilikuwa ikilegalega. Matokeo ya mtihani form iv 2013,SERIKALI imeamua kuwabeba wanafunzi na kujiriDHIsha kuwa inatekeleza sera ya BRN. Kwa maelezo haya mi naona msomi wa mwisho kumaliza form IV nchini TANZANIA ni yule aliyemaliza miaka ya 2007,2006,2005....... Hawa wa miaka ya 2008,2009,........ ni wasomi wa kupewa maksi na serikali! Au ninyi mnaonaje wakuu?