Waliomaliza form iv mwaka 2007 kushuka v/s waliomaliza form four 2008-2013.

Waliomaliza form iv mwaka 2007 kushuka v/s waliomaliza form four 2008-2013.

Wanafunzi waliomaliza mwaka 2000 ndo hao peke yao ambo walikumbana na changamoto za mabadiliko Necta na wizara ya elimu kwa ujumla . Namaanisha hata style ya utunzi ilibadilishwa pamoja na usahihishaji.
 
nakataa kwani mitihani ya 2010 kushuka maswali yalikuwa yanarudiwa sana hata wewe shahidi hivyo aliye solve past papers ndiye aliefaulu,,1.7 zilikuwa za kumwaga na vijana wengi wa govn walikuwa wanakariri sana almaarufu kumeza,,,hivi sasa mtaala sio content based bali competence ka hujui kaulize necta,,na hii ndo ilifanya 2011 na 12 wafeli kwani waliikuta wakiwa form 3 na 4,,,vitabu vya sasa (kuanzia 2012) ni bora na competence based,,,masuala ya kukariri hayahitajikini tena bali uelewa wako wa mambo,,,

Hilo la vitabu silikubali
Kuanzia 2008 hadi leo kumekuwa na utitiri wa vitabu vya kiada na ziada ambavyo havikidhi viwango kwa vile vimeandikwa na watu binafsi wenye lengo la kupata maslahi
Hata vile vilivyoandikwa na taasisi havina content inayojitisheleza
Vile vile hakuna taasisi inayodhibiti ubora wa vitabu
Kila shule hutumia vitabu vyake kwa vile hakuna mwongozo wa vitabu vipi vitumiwe
Hali hii bado inaendelea hata sasa
 
Mpambano ni mkali kwelikweli!Sasa mi nadhan ipo siku tutakutana kwenye 'INTERVIEW'
 
Mtakaa mtabishana na kila mmoja kuvutia mwaka wake alofanya mitihani akijisifia ndio bora... Mpango mzima katika kumake money tu, tunasoma tutemgeze hela ya kuendelea na maisha, sasa kaeni mjisifie magamba mloyatia lamination kisha mfukoni ndururu huna, utakuwa mjing.a kichizi.
 
Napeperusha bendera ya 2007 kushuka chini enzi hizo unaambiwa u-define mpaka kwenye mathematics, aiseee shule ilikuwa zaman, kikwetism imewapoteza sana vijana
 
Mwaka 2007 ulikuwa ni highest peak kwa ufaulu na baada ya hapo mambo yalianza kuvurugika sana, mambo mengi yanachangia.

1. Walio maliza 2008 kama mnakumbuka walivurugwa na Mungai (hawa ni watu wa physics with chemistry.
2. Watu wa 2009 hawa hawakuwa na mtihani wa form two, wasiojiweza wengi walifika form four.
3. 2010 kulikuwa na uchaguzi wa kitaifa, kila mtu alikuwa bize na siasa, kama mnakumbuka mwaka huu nia halisi ya mgomo wa walimu ili wapandishiwe mshahara ilionekana.
4. Mwaka 2010 pia watoto walilipiwa ada ya mtihani na serikali, kwa hiyo ni lazima serikali ifanye kila linalo wezekana.
5. Mwaka 2011 hawa watoto pia hawakuwa na mtihani wa form two, na mgomo baridi wa walim uliendelea kushika kasi.
6. Mwaka 2012 mgomo wa walimu uliingia hadi vijijini na kuanza kuingia mioyoni mwa walimu na mwaka huo huo kulikuwa na mgomo dhahili wa walimu japokuwa ulikatizwa.
7. 2012 huu mwaka licha ya kuwa na mgomo dhahili wa walimu, pia mwaka huu kulikuwa na sensa iliyo chukua mwezi mzima, what do you expect from these two?
8. Mwaka 2013 up to date mgomo wa walimu (mgomo baridi) umeingia uvunguni mwa mioyo ya walimu, na hivi sasa nao wamefunga EFD/LUKU kwenye ufundishaji siku hizi walimu wanasema FUNDISHA KADRI UNAVYO LIPWA (FUKU).
9. Kuna sababu zingine nyingi, kama miundombinu mibovu, mazingira yasiyo rafiki katika ufundishaji, na nyingine nyingi.

10. Slogani mpya ya serikali ya "SIASA KWANZA ELIMU BAADAE" nayo imechangia kwa kiasi kikubwa, kusema kweli wakuu wa shule wanapata tabu sana na hawa watu waitwao madiwani.

Mie ni hayo tu wandugu, i stdand to be corrected.

mkuu hapo kwenye namba.1 na 2 umedanganya
mm nimemaliza mwaka 2009,cc ndo 2likuwa wahanga wa physics with chemistry na 2lixoma hl somo 2kiwa form one mwaka 2006
darasa le2 ndo lilikuwa la mwisho kufanya mtihan wa form two mwaka 2007 na waliofel walikarr darasa
waliomaliza mwaka 2008,ndo wa kutiliwa mashaka kwan mitihan yao yote ilivuja na mingine kuokotwa masokon na stend,hisabat iliahirishwa lakn still ilivuja
mwaka 2009 wazir wa elim kipind icho j4 maghembe aliapa kutembea uchi kama mitihan ingevuja tena na kwel cha moto 2likiona kwan 2lifaulu kwa nguvu zetu wenyewe
mwisho madarasa yaliyopitishwa form two bila mtihan n kuanzia 2010 mpaka 2013
 
Mi nawashauri waliomaliza form iv kuanzia mwaka 2008 wawe wanaomba tuwafundshe TUISHENI baadhi ya masuala ya shule! Kuna vitu vingi sana hawajui! N.B- DIV IV.31 -2007,ni sawa na DIV III.31-2013.
 
mkuu hapo kwenye namba.1 na 2 umedanganya
mm nimemaliza mwaka 2009,cc ndo 2likuwa wahanga wa physics with chemistry na 2lixoma hl somo 2kiwa form one mwaka 2006
darasa le2 ndo lilikuwa la mwisho kufanya mtihan wa form two mwaka 2007 na waliofel walikarr darasa
waliomaliza mwaka 2008,ndo wa kutiliwa mashaka kwan mitihan yao yote ilivuja na mingine kuokotwa masokon na stend,hisabat iliahirishwa lakn still ilivuja
mwaka 2009 wazir wa elim kipind icho j4 maghembe aliapa kutembea uchi kama mitihan ingevuja tena na kwel cha moto 2likiona kwan 2lifaulu kwa nguvu zetu wenyewe
mwisho madarasa yaliyopitishwa form two bila mtihan n kuanzia 2010 mpaka 2013

wewe kweli wa 2008 ->
ndio nyinyi mlioanza kuandika 'X' badala ya 'S'
shame on you
 
Kama ni kelele tumepiga sana
Kelele zetu kama MAJI YA MOTO hayakawii kupoa
Serikali yetu kama pakacha bovu ukiziba huku kule kunavuja
Siku,miezi mwaka ,miaka inapita
Kelele, kelele , elimu duni,waalimu hawatoshi malipo kidogo,wanafunzi wanakaa chini madawati hakuna na sasa matokeo du???

Huduma za afya hoi ukiandikiwa asprin ukanunue dukani,Kina mama wanajifungulia chini hosptalini vitanda hakuna

Umeme mgao au unakatika katika bila sababu na bei juu

Polisi Mahakamani bila chochote file halionekani au kesi itapigwa tarehe hadi mashahidi wako watakuchoka kesi dismiss

Wimbo mmoja kila siku kelele hadi watawala wetu wametuchoka wanasema sisi watanzania mazuzu tutawachagua tu kwani
kama maji ya moto hatukawii kupoa
Ni kweli ngoma ya watoto haikeshi

Hebu na tukue mwakani uchaguzi tucheze ngoma ya watu wazima mpaka kuche giza limezidi
 
Nimegundua ubora wa elimu hapa TZ,ulianza kushuka miaka ya 2008, kama tunakumbuka kipndi hiki(kikwetism) mitihani ya taifa form 2 na form 4 ilivuja mno, Madogo wengi walitusua kwa kwenda shule za vipaji maalum. Miaka ya hapa kati 2009,2010,....,...2012 elimu yetu bado ilikuwa ikilegalega. Matokeo ya mtihani form iv 2013,SERIKALI imeamua kuwabeba wanafunzi na kujiriDHIsha kuwa inatekeleza sera ya BRN. Kwa maelezo haya mi naona msomi wa mwisho kumaliza form IV nchini TANZANIA ni yule aliyemaliza miaka ya 2007,2006,2005....... Hawa wa miaka ya 2008,2009,........ ni wasomi wa kupewa maksi na serikali! Au ninyi mnaonaje wakuu?

.
Kaka hebu tujaribu kuangalia na utungaji wa mitihani wenyewe!

.
Miaka ya hapo nyuma mtu unakutana kabisa na
define ..-------
.
Lakini hali ya sasa ina tisha mtu aliyesoma miaka ya 2005 serious kabisa mtihani wa miaka hii ya sasa utamsumbua tena sio kidogo...
.
Midomo yetu isiwe miepesi tu kusema siku hizi watoto wanabebwa.....
Angalieni na hali harisi mitihani ya siku hizi si ya kitoto!
.
Over
 
shule ya nyumbani kwenu ndo haikuwa na mtihani wa kidato cha pili kwa wale waliohitimu 2009,na je wewe ulipata div ya ajabu kuliko hao walionzia necta 2008 na kuendelea?kama ndivyo una nini na uko wapi ndo kitu kinachoangaliwa,au wewe div yako ilikuwa below dv 1 and above div 0?
 
Lecture mmoja wa Udsm nanukuu,endapo serikali itaendelea kuleta wanafunzi kama hawa mimi mwakani naacha kazi mana kujibu mitihani hawajui licha ya mafunzo na maelezo
 
watu wengne humu wanafki tu wanaongea vitu bila data,mim nmemalza 2009 na sis ndo tulikua watu wa mwisho kufanya mtihani wa 4m2,pia cc 4m1 physics with chemistry,alaf kufika mwez wa sita wakazigawanya tena,na pia mitihani yasasa hv inahitaji maarifa zaid kulko kukulil km mitihan ya zamani ilivyokua
 
compitence. v/s content!
hope ni rahisi sana ku-define kitu ikiwa umesoma na kukikariri, but ni ngumu sana kukielezea kitu endapo umekisoma na kukikariri tuu bila kukielewaa...!
Over .....!
 
Nimegundua ubora wa elimu hapa TZ,ulianza kushuka miaka ya 2008, kama tunakumbuka kipndi hiki(kikwetism) mitihani ya taifa form 2 na form 4 ilivuja mno, Madogo wengi walitusua kwa kwenda shule za vipaji maalum. Miaka ya hapa kati 2009,2010,....,...2012 elimu yetu bado ilikuwa ikilegalega. Matokeo ya mtihani form iv 2013,SERIKALI imeamua kuwabeba wanafunzi na kujiriDHIsha kuwa inatekeleza sera ya BRN. Kwa maelezo haya mi naona msomi wa mwisho kumaliza form IV nchini TANZANIA ni yule aliyemaliza miaka ya 2007,2006,2005....... Hawa wa miaka ya 2008,2009,........ ni wasomi wa kupewa maksi na serikali! Au ninyi mnaonaje wakuu?
kweli kabsa,form wa mwisho ni wale wa 2007 tu,kuanzia 2008 hapo majanga
 
Back
Top Bottom