Waliombeza RC Makonda leo mmeumbuka

Waliombeza RC Makonda leo mmeumbuka

Fikira finyu kuwaza kwamba makonda kuna kitu amefanya kuwezesha ushindi huu? Labda tu kama kuna kitu amekifanya ni kwenda kuwabembeleza Uganda au kwa chochote kuwaomba walegeze. Kwa mawazo yako Uganda isingekuwa bado haija-qualify unafikiri wangekubali kufungwa kirahisi hivyo? Gool 3 uwafunge Uganda kirahisi hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mtu mzima na akili yake anataka eti Tanzania ishindwe kwenda Misri kushiriki AFCON kwa sababu kamati ya stars inaongozwa na Makonda!!.

Makonda asingezaliwa Tanzania isingekuwepo!!. Tanzania ni zaidi ya mtu mmoja mmoja. Unapoitakia mabaya maana yake wewe huna tofauti na mnafiki.

Na siku zote zawadi ya mnafiki huwa ni kutandikwa risasi, zamani enzi za Yesu na Mohamed mnafiki alikuwa anapigwa mawe mpaka anakufa.
 
Tff siku za nyuma walitangaza kamati wezeshi ya kuhakikisha tunashiriki michuano ya Afcon kule Misri mwaka huu,Kamati hii ya ushindi ilikuwa inaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Baada tu ya Makonda kutangazwa tu kuongoza kamati tumeshuhudia baadhi ya wadau humu kwenye mitandao ya kijamii wakibeza hili na kuingiza mada za kisiasa ilimradi tu kumkatisha tamaa Makonda..

Wengine walienda mbali zaidi kwamba kwanini asitumie wachezaji wa zamani kama chachu ya ushindi na si kuwatumia wasanii kama alivyofanya?

Leo wale wote mliokuwa mnambeza Makonda na kamati yake mmeumbuka na hatimaye Taifa stars imefuzu michuano ya AFCON.

Mwisho Baniani mbaya kiatu chake dawa..Hongera sana RC Makonda na kamati yako kwa ushindi wa leo

Sent using Jamii Forums mobile app
ina maana alicheza... wachezaji wasifiwe kwa kujitoa kupambana.....vitu vingine tujaribu kutumia akili.....jamii forum is for great thinkers
 
Hivi kwa akili yenu Uganda wangekuwa hawaqualify leo wangekubali kufungwa?
Mkuu kwa akili yako ile mechi ya kwao tuliyopata sare (droo) walikuwa wamesha-qualify?
Mbona waliponea chupuchupu kufungwa kwao na stars hii hii?
 
Hongera serikali ya sisiemu ya wanyonge kwa kuivusha sitaz kwenda Afukoni! Maendeleo hayana vyama.
 
Kumbuka uwanjani huwa kuna wachezaji 12!
Kama ni hivyo, kwanini sifa zinaenda kwa DAB pekee na si kwa mashabiki wote?! Ukweli ni kuwa hata PM alikuwa pale lakini DAB tu anaonekana ndiye aliyeleta ushindi. Hii sio sawa hata kidogo. Huyu mtu anatukuzwa kuliko uhalisia wake.
 
Things were obvious. Wapumbavu wanataka kuchukulia hapo points.
Waache wajichukulie points kwani hzo points hazidumu na wala haina nafasi kama historia iliyowekwa na Vijana wetu Taifa Stars hiyo itabaki milele na milele kukumbukwa sasa kwa nini niendelee kuteseka?
 
Yaani mtu mzima na akili yake anataka eti Tanzania ishindwe kwenda Misri kushiriki AFCON kwa sababu kamati ya stars inaongozwa na Makonda!!.

Makonda asingezaliwa Tanzania isingekuwepo!!. Tanzania ni zaidi ya mtu mmoja mmoja. Unapoitakia mabaya maana yake wewe huna tofauti na mnafiki.

Na siku zote zawadi ya mnafiki huwa ni kutandikwa risasi, zamani enzi za Yesu na Mohamed mnafiki alikuwa anapigwa mawe mpaka anakufa.
Kwa hili limenifanya nichukie siasa yaani kisa mtu au kikundi kimoja mtu uchukie mafanikio ya taifa lako ? ,kuwa mfiachama ni shida tupu yaani anaweza jitikeza hata mfadhili kujenga hospitali kijijini kwenu lakini ukaombea hata mradi huo usiwepo na ufe kisa mtu atachukulia points yaani bora watu wafe kwa kukosa huduma
 
Back
Top Bottom