Wafahamu zamani mtu bosi wa shirika la umma akifukuzwa kazi na ikitangazwa redioni ni lazima watasema "amefukuzwa kwa manufaa ya umma".
Yaani yule mtu akiendelea kuwepo pale basi taasisi, shirika au kampuni hiyo itaanguka maana ameitumia vibaya kiofisi, matumizi mabaya ya fedha na kutojali au "carelessness".
Hivyo hili neno kwa manufaa ya umma ni neno muhimu sana kwa kizazi cha sasa kufunzwa.
Kisha kuna neno Kwa Maslahi ya Taifa au "national Interests".
Hili neno Kwa Maslahi ya Taifa bado wengi wanalipuuzia kwa makusudi yaani "ignorance" na waendekeza uhuni ambao ndo auzungumzia bwana Polepole.
Kizazi cha sasa chapaswa kujifunza kwa moyo wote maneno haya mawili Maslahi ya Taifa na Kwa manufaa ya Taifa.
Kitu chochote kinohusiana na maneno haya mawili kinawahusu wananchi wa taifa husika na si kikundi fulani.
Leo hii Iran akitishiwa au Korea Kaskazini akitishiwa a nchi za magharibi, wao husema sisi tutalipua sehemu zote tunazofahamu ninyi mna maslahi yaweza kuwa ndani au nje ya nchi hizo.
Na wakisema hivyo nchi za magharibi hukaa kimya na maisha yaendelea.
Sasa hoja zozote zinazohusu maslahi ya taifa, Nishati, madini, miundombinu, mifumo ya afya, Chakula, kilimo ni sehemu ya maslahi ya taifa.
Yaani wananchi wa Tanzania wanastahiki kufahamu mtakabali wa maslahi ya taifa lao.
Wakijitokeza watu kuzungumzia masuala hayo wasibezwe waachwe na hio ndo demokrasia.
Bwana Polepole hayupo peke yake kuna kundi kubwa sana nyuma yake ambalo bado lina dukuduku la moyoni.
Ipo siku si mbali dukuduku hilo litatolewa.