Kabla ya kupiga kelele zozote ilikuwa ni vyema kutafuta toleo zima la utafiti na kulisoma, kuliko kulishwa maneno na kuruka nayo. Hata biblia inaweza kutumiwa na mchawi atakavyo.
1: Utafiti uliofanyika ni in-vitro/kwenye maabara na pia ni pre-clinical. Kwa kutumia ini Huh7. Haijafika hata clinical stage.
2: Dose iliyotumika kwa seli za ini husika ni kubwa ukilinganisha na dose ya kawaida ya chanjo. Ambayo wao pia wanasema itahitaji kunyambulishwa zaidi/kutolewa maelezo sahihi.
3: Imesharipotiwa na Pfizer na BioNTech kuwa asilimia 18 (18%) ya dose ya chanjo/dawa inaenda kwenye ini. Hilo linajulikana.
4: Tafiti zimeshaonyesha kuwa virusi vya SARS-Cov2 RNA vinaweza kuingilia mfumo wa DNA ya seli kwa mtindo wa Reverse-transcriptase. Nasisitiza VIRUSI na SI CHANJO ya mRNA.
5: Chanjo ya BNT162b2 ni sehemu ya SARS-Cov2 inaweza pia kujishikiza kwenye DNA kwa mtindo uleule.
MALENGO YA UTAFITI
1: Kuangalia/demonstrate kama BNT162b2/chanjo ina uwezo wa kuingia kwenye seli za ini na kwa njia ipi kwa kiasi gani?
2: Athari/demonstrate ya BNT162b2/chanjo kwenye Reverse Transcriptase Long Interspersed Nuclear Element-1 (LINE-1) na kiasi cha protein husika.
3: Kutafuta/demonstrate Reverse BNT162b2 DNA kwenye seli za Huh7/ini husika.
Majibu hapo juu yote yamepatikana ni kweli. Kinachofuata/unachohutaji kujua kabla ya kelele ni:
1: Je mabadiliko haya ni ya kudumu na kwa kiasi gani?
2: Mabadiliko haya yana-athiri ufanyaji kazi wa seli husika?
3: Mabadiliko haya yanaweza kusababisha vitu kama KANSA na au kuzaliana na kugeuka sumu kwa DNA ya seli za mwanadamu?
4: Swali pia litakuja kuwa kati ya aliyepata half impact ya Covi (chanjo) na ku-control multiplication na aliyepata Covid full range impact nani atapata athari zaidi kutokana na athari ya kila kimoja?
NB: Haya yanayozungumzwa hapa yanahusu pia walioambukizwa Covid, na kwa tafiti za mwanzo ililenga kujua kwa nini wagonjwa wa Covid waliendelea kuwa na majibu positive kwa kipimi cha PCR kwa muda mrefu kidogo baada ya maambukizi/kuumwa.
Kwenye utafiti huu, hakuna sehemu wamesema mtu atageuka ZOMBI au HATAZAA nk.
Tujisomee haya mambo.