Nawasalimu wote wakubwa kwa wadogo,
Ni usiku wa kuamkia leo nimepokea taarifa kutoka kwa watu wangu wa karibu kua kuna daktari ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga katika mji wa Nyamongo wilaya ya Tarime.
Daktari huyo kijana mdogo kabisa aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Afya Nyamongo(Nyamongo HC) amekutwa na umauti huo wakati akiwa anaendesha pikipiki yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika mji huo.
Bado chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana, na wala sina taarifa yoyote kuhusiana na kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.
Ni aibu kubwa Kwa mji huo kumuua mtumishi tena kwa kumkata kata kwa mapanga wakati huu ambao kumekua na uhaba wa watumishi hasa kada ya afya katika maeneo ya pembezoni ya nchi. Je, ni nani atakubali kwenda kufanya kazi katika eneo kama hilo ambalo linaonekana si salama tena kwa watumishi na ukizingatia ajira za TAMISEMI zimetangazwa juzi.
Haijalishi sababu ya kifo itakuwa nini lakini huu ni ukatili wa hali ya juu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Dr Isack Sima Mahala pema peponi, Amina.