Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Asante sana Ushimen wewe unaishi tu huko, ama ni mwenyeji wa huko? Usinicheke lakini, Nyamongo nimewahi kwenda, mara moja tu ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
Napatikana kwa wingi sana kuanzia Kemakorere, Nyamwaga, Kerende, Nyamongo, Matongo hadi muambata wa mto Tigite mura...๐Ÿ˜œ
Mimi sio mzaliwa wa huku mkuu, nasaka ugali tu...๐Ÿ˜‹
 
Nawasalimu wote wakubwa kwa wadogo,

Ni usiku wa kuamkia leo nimepokea taarifa kutoka kwa watu wangu wa karibu kua kuna dakitari ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga katika mji wa Nyamongo wilaya ya Tarime.

Dakitari huyo kijana mdogo kabisa aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Afya Nyamongo(Nyamongo HC) amekutwa na umauti huo wakati akiwa anaendesha pikipiki yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika mji huo.

Bado chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana, na wala sina taarifa yoyote kuhusiana na kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Ni aibu kubwa Kwa mji huo kumuua mtumishi tena kwa kumkata kata kwa mapanga wakati huu ambao kumekua na uhaba wa watumishi hasa kada ya afya katika maeneo ya pembezoni ya nchi, je ni nani atakubali kwenda kufanya kazi katika eneo kama hilo ambalo linaonekana si salama tena kwa watumishi na ukizingatia ajira za TAMISEMI zimetangazwa juzi,

Haijalishi sababu ya kifo itakuwa nini lakini huu ni ukatili wa hali ya juu

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Dr Isack Sima Mahala pema peponi, Amina

Poleni sana, ila mauaji kama hayo mostly huwakuta wala vitu vya watu, sijasema kala vitu vya watu, ila mapenzi huleta chuki sana.
 
Kanda ya ziwa hasa Mara,musoma.,kagera ni watu wa ajabu Sana,Hawa jamaa kukata mtu mapanga imekuwa Kama Hadi Sasa,ni maeneo hatari Sana haya,Kuna classmate wangu tulipotezana miaka kadhaa baada ya kumaliza chuo ,majuz hivi tukakutana kwenye event moja hivi ya mh.rais jijini Dodoma ,kumchek jamaa usoni ana lialama la mkato wa panga Ila limepona so kabaki na lialama la kukatwa,sikutaka kumuuliza kulikoni mkuu li ngeu panga usoni ,maana tulikuwa serious kidogo na event ,yeye alikuwa huko Mara kikazi bt baadae alifanya transfer kutoka kule.
Bukoba sio makatili kama haya mashezi!
 
Lindi kuko shwari hata usiku wa manage unatembea
Ila kanda ya ziwa ni balaa

Ova
Hatari sana kuna madogo walipigwa jembe za kichwa.Kuja kupata habari kumbe walikuwa wameenda kufatilia mchongo kwa mturuki-Tabora.Wakakutana na Mangosha na vijinzi vyao vya kubana ,jamaa wakawaungia kuwa watakua wezi wa ng'ombe tu.Watu wakanda ya ziwa wakiwa town kama mafala wakute chaka sasa.
 
Duh,inasikitisha sana

Ova
 
We fikiria uhaba wa wataalam wa afya nchini hasa vijijin unapata uhodari wa kumpiga dr jembe la kichwa sasa unatofauti gani na mtu anayeweka aumu kwa siri kwenye kisima cha kijiji????
Unyama huo,huko wanaamini sana kwenye kutumia maguvu,ubabe
Kama hapo wamemuaa dr mtu ambaye alikuwa msaada kwao.
Hiyo kanda imenikalia shoti sana
Mimi napenda sehemu kuwe na uhuru,amani
Haya mambo ya kuishi roho mkononi
Na mashaka ya nini

Ova
 
Nawasalimu wote wakubwa kwa wadogo,

Ni usiku wa kuamkia leo nimepokea taarifa kutoka kwa watu wangu wa karibu kua kuna dakitari ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga katika mji wa Nyamongo wilaya ya Tarime.

Dakitari huyo kijana mdogo kabisa aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Afya Nyamongo(Nyamongo HC) amekutwa na umauti huo wakati akiwa anaendesha pikipiki yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika mji huo.

Bado chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana, na wala sina taarifa yoyote kuhusiana na kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Ni aibu kubwa Kwa mji huo kumuua mtumishi tena kwa kumkata kata kwa mapanga wakati huu ambao kumekua na uhaba wa watumishi hasa kada ya afya katika maeneo ya pembezoni ya nchi, je ni nani atakubali kwenda kufanya kazi katika eneo kama hilo ambalo linaonekana si salama tena kwa watumishi na ukizingatia ajira za TAMISEMI zimetangazwa juzi,

Haijalishi sababu ya kifo itakuwa nini lakini huu ni ukatili wa hali ya juu

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Dr Isack Sima Mahala pema peponi, Amina
Huyu kijana nilimfahamu toka 2020.
Anaitwa ISACK DANIEL SIMA.
Ni Mnyaturu kwa kabila, mzaliwa wa Kijiji cha Kaselya wilaya ya Iramba.
Alizaliwa 1993 akasomea Shahada ya udaktari katika chuo cha st. Francis.
Ameacha Mke na mtoto mmoja.

Alikua ndo mtoto tegemezi katika familia yao.

Tukio limetokea Jana saa 5 usiku akiwa kwenye pikipiki na Mdada mmoja ambaye amebakwa na kulazwa hospital.

Waharifu wakaamua kumcharanga mapanga kijana wetu.

Mungu wangu tunaomba uoneshe hasira yako juu ya hawa shetani.

FB_IMG_1683174991258.jpg
FB_IMG_1683175050026.jpg
FB_IMG_1683195466168.jpg
 
Attachments

  • 20230504_184907.jpg
    20230504_184907.jpg
    45.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom