Waliomuua mwalimu walimuibia Mil 9.5

Waliomuua mwalimu walimuibia Mil 9.5

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu watano waliokuwa wanajifanya waganga wa kienyeji kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu Monica Patrick (31) mkazi wa Itilima mkoani Simiyu baada ya kumuibia fedha shilingi milioni 9.5 na kisha kumnyonga.

Imeelezwa marehemu alifika mkoani mara kwa madai ya kumfanyiwa maombi ya kumsaidia katika biashara yake ya madini.

FpkeE_0WAAEr-TK
 
Walimdanganya apeleke hizo pesa zikaombewe ili ziongezeke kishirikina. RIP mwalimu.
Kuna dogo mmoja naye aliwahi kufilisika kupitia utapeli wa aina hii hii. Kuna mwenzake alimdanganya eti Tunduma kuna waganga wa aina hiyo!

Akachukua milioni 10 ya mtaji na kuipeleka kwa mganga, akiamini itaongezeka! Matokeo yake dogo aliishia tu kutapeliwa, na mpaka leo hajafanikiwa kurudi katika kile kiwango chake cha biashara.

Binafsi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini eti mtu hawezi kufanya biashara, bila ya uchawi.
 
Pumzika kwa amani mwalimu Monica Patrick. Haki itapatikana tu kwa hao wauaji wako.

By the way, biashara wala haihitaji uchawi! Hivyo watu wasikubali kutapeliwa kirahisi na wazee wa mjini. Tena wengine wapo mpaka humu jukwaani.
Wamo aisee. Kuna watu wanaitwa Tindo na Sexless; kila nikisoma comments zao nywele zinanisisimka!! Ndo hawa Waganga matapeli
 
Kuna dogo mmoja naye aliwahi kufilisika kupitia utapeli wa aina hii hii. Kuna mwenzake alimdanganya eti Tunduma kuna waganga wa aina hiyo!

Akachukua milioni 10 ya mtaji na kuipeleka kwa mganga, akiamini itaongezeka! Matokeo yake dogo aliishia tu kutapeliwa, na mpaka leo hajafanikiwa kurudi katika kile kiwango chake cha biashara.

Binafsi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini eti mtu hawezi kufanya biashara, bila ya uchawi.
Mbona Zito anafanikiwa?
 
Back
Top Bottom