BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Kwa sababu wewe ni nyumbu.Basi kaa kwa kutulia,
Binafsi siwezi poteza muda kwa visivyo nihusu
Mkuu vijana wa enzi ya Nyerere na Mwinyi walikuwa jasiri, waliandamana hata watoto wa shule walikuwa wanaandamana; lakini hawa wa leo wala chips, wengine waoga, wanafiki, chawa hawawezi kuandamana, wengine kazi yao ni kuwachongea wenzao tu.Tukiondoa uoga, kujipendekeza na unafiki,tunaweza kuionesha serikali kuwa Tanzania hii siyo ile ya Nyerere.
Hii ni Tanzania iliyochangamka, ni Tanzania inayojua nini inahitaji.
Cha msingi ni kuwa na umoja,
(Unit is power) na dhamira ya kweli.
Nguvu ya umma ni zaidi ya risasi na mabomu.
Maanda ya watu hawazidi watano ni maandamano gani hayo?Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.
Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.
========
WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI
Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.
yuko Masaki hapa anakula bia, anasema amechelewa kuamka na alisahau kuwa ni leoYule huenda walimkamata kabla
Basi tuyaite matembezi ya hiari.Maanda ya watu hawazidi watano ni maandamano gani hayo?
Kibaya zaidi huyu Deus Soka ni kutoka familia maskini kabisa na anadanganywa na hawa wahuni ambao wamekula na kushiba kama mzee mbowe,lissu na LemaDeus Soka kijana ambaye amekubali kutumika na wanaharakati na wanasiasa bila kujua athari zake kwa kuhamasisha maandamano leo jumatatu hajaonekana kwenye maandamano hayo na matokeo yake walioingia mkenge wamenaswa na sasa familia na ndugu wanakaa vikao vya kwenda kuwanasua.
Kibaya zaidi wanaowatuma wamekaa maofisin wanaandika maandiko ya kuomba hela kwa wazungu ili kuendelea kuhamasisha ujinga nchini ilhali wao na familia zao maisha yanaenda.
Watanzania tubadilike, hamtamuona mtoto wa Mbowe wala Tundu lissu wala Maria Sarungi.
Sasa hela ya kula na familia mnakwenda kuitumia kama nauli ya kwenda na kurudi polisi kila siku.
Hiyo ndio concept ya Poverty Circle.
Kwaninwatakiona cha mtema kuni huko lokapu
Thubutu!!Umeenda andamana?
Alikuwa nyumbani kwa mzee Mbowe akisubiria kupata ujira waleYule huenda walimkamata kabla
Eeh ila nyie kazi yenu ni kuandamana nyuma ya keyboard wakikamatwa watu wanatudi hapa kuwapongezaMungu awabariki walioandamana.
Wamedhihirisha kwa vitendo Uzalendo kwa nchi yao.
Huyo askari aliyemkamata muandamanaji naomba anikamate na mimi, nipo Tegeta.Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.
Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.
========
WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI
Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.
MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI
Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.
Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.
Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.
Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.
Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.
Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.
Mwananchi
Nahisi hivyoYule huenda walimkamata kabla
Ila sio wewe, waumie wengineHuwezi kuletewa uhuru kwenye sahani lazima baadhi yetu waumie.