Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Maandamano uchwara ,angalia huko Tripoli ,Cairo na Benghaz watu wamechafukwa wameshawahi kutoa mpaka marais madarakani.

#KataaMaandamano #MaandamanoNiUhalifu
Adriz,tupe maoni kama haya siku wazanzibar wakiandamana kujitoa ktk muungano.
Nitakukumbusha.
 
Wapumbavu mpo wengi sana bongoland
one of direct qualification ya kua mwanachadema ni kuamini kwamba kuropoka matusi, kujiona unajua sana kuliko wengine na kuamini unachofikiria ndio sahihi ndio AKILI..... Kwahiyo sikushangai huo ni utamaduni wenu.
 
kwahiyo hadi watu wa Nangurukuru, Ileje na Itipingi Njombe nao waende wakaandamane ?
 
Yamefanikiwa sana kwani yamevunja propaganda ya udini, Kuna watu mpaka viongozi wa dini walikuwa wanasema rais anapingwa sababu ya udini lakini miongoni mwa walioandamana ni kutoka dini yake
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.

========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.

MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Mwananchi

PIA, SOMA:
- Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai
- Polisi yapiga marufuku maandamano ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, Jumatatu Juni 19, 2023
Kuwategemea watanganyika kwenye maandamanonyankudai haki ni sawa na kusubiri mbuzi atage yai!

Naamini wao waliamini wakiingia barabarani wataungwa mkono na watanganyika wengine ili maandamano yashike hatamu lakini mambo yamekuwa tofauti sana wakajikuta kama walikuwa 10 walio toka na maandamano wamebaki 10 hao hao hakuna mtu aliye ongezeka hata mmoja.
 
Chile the social, economic, and political laboratory of the world

2023 Tanzania imeingia katika maabara ya dunia ikionesha kuwa ni mwanzo mzuri kisiasa kwa vijana wake wameweza kuingia barabarani kuonesha kutokubaliana na siasa za kuifanya Tanzania iwe eneo la mabeberu kuingia na kuichezea mali za taifa milele.

Hali hii mpya ya kisiasa itaendelea kuwa endelevu hadi watawala watapotambua kuwa wamefanya makosa kuingia katika mikataba ya kibeberu na ukoloni mkongwe.

Jambo la kutia moyo ni kuona upingaji wa sera hizi za serikali sio tu umeingia barabarani kupitia maandamano lakini pia sauti zinapazwa kutoka kila kona huku wazee wasomi kama Profesa Haruna Lipumba, Profesa Anna Tibaijuka, wachambuzi waandishi wasomi kina Jenerali Ulimwengu, wazee kina Stephen Wassira na great thinkers wa JF vijana wote wanaendelea kupaza sauti kwa kupitia radio, televisheni, mijadala na mitandao hii inaonesha upinzani dhidi wa kugawiwa eneo la nchi yetu ni endelevu

Raia wote wakubwa kwa wadogo, kina mama kwa kina baba wamejitokeza kuonesha vuguvugu hili litaendelea kuchemka na kutokota kwa muda mrefu hadi kuwachoma watawala na bunge lao pia serikali hadi wasitishe hili jambo na kuutupilia mbali kaa hili la moto linalounguza la mkataba mbovu

Aluta Continua !

Gabriel Boric won Chile's presidential election in December 2021

1687243938919.png
 
Maandamano yeyote ni upuuzi na uhalifu hata Waislamu wakiandama bado nitafbakia katika kauli hiyo.

#KataaMaandano#NiUhalifu
Niliongelea wazanzibari. Ila nitakukumbusha kauli yako hii.
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.

========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.

MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Mwananchi

PIA, SOMA:
- Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai
- Polisi yapiga marufuku maandamano ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, Jumatatu Juni 19, 2023
pole zao
 
Back
Top Bottom