NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
- Thread starter
-
- #21
Kwa sababu ni suala la Yanga umejifanya mwanaharakati sana na kubana bajeti.Kuna watanzania wengi wanasoma huko Algeria, hili zoezi la kwenda na ndege ya Air Tanzania wala kupeleka mashabiki halikuwa na umuhimu, ni ubadhilifu tu wa mali za umma.
Serikali kama ilitaka kusaidia ingelipia baadhi ya gharama za usafiri wakaenda na mashirika mengine kama kawaida, gharama zingekuwa chini zaidi kuliko kurusha ndege halafu ikapaki siku 4 pale Algiers (na hata hili halina ulazima maana CAF wanatoa mafungu ya kutosha kulipia gharama hizi za usafiri).
Kule Misri mechi na Uganda hatukupeleka mashabiki, waliopo kule wakaja kushangilia tukashinda. Tulivyorudiana hapa Dar, tukapitisha zoezi la kununua tiketi, uwanja ukajaa tukafungwa. Akili kumkichwa.