Waliopanda ndege ya Mama kwenda Algeria ni mashabaiki wa Yanga SC au wavaa suti tu wanaokwenda kutalii na kupiga selfie?

Waliopanda ndege ya Mama kwenda Algeria ni mashabaiki wa Yanga SC au wavaa suti tu wanaokwenda kutalii na kupiga selfie?

Kuna watanzania wengi wanasoma huko Algeria, hili zoezi la kwenda na ndege ya Air Tanzania wala kupeleka mashabiki halikuwa na umuhimu, ni ubadhilifu tu wa mali za umma.

Serikali kama ilitaka kusaidia ingelipia baadhi ya gharama za usafiri wakaenda na mashirika mengine kama kawaida, gharama zingekuwa chini zaidi kuliko kurusha ndege halafu ikapaki siku 4 pale Algiers (na hata hili halina ulazima maana CAF wanatoa mafungu ya kutosha kulipia gharama hizi za usafiri).

Kule Misri mechi na Uganda hatukupeleka mashabiki, waliopo kule wakaja kushangilia tukashinda. Tulivyorudiana hapa Dar, tukapitisha zoezi la kununua tiketi, uwanja ukajaa tukafungwa. Akili kumkichwa.
Kwa sababu ni suala la Yanga umejifanya mwanaharakati sana na kubana bajeti.
 
Wawe mashabiki ama wavaa suti,ukweli ni kwmb muhimu ni bench la ufundi na utayar wa wachezaji kupambana ndo kitakacholeta matokeo chanya
 
Nitangulize kutoa baraka na kila la heri kwa Yanga SC katika mpambano wa marudiano huko Algeria.

Kongole kwa Mh. Raisi kwa kutoa ndege ya mashabiki na wadau wa mpira kwenda kuisapoti Yanga SC.

NALIA NGWENA najiuliza hao mashabiki waliopanda ndege ni mashabiki wa kuleta morali/kushangilia muda wote au ni mashabiki wa kuvaa suti na kupiga selfii (watalii)?

Nitasikitika sana kama mashabiki lialia/wenye morali ya kushangilia endapo watakua wameachwa.

Nawasilisha hoja.
Nendeni mkachapwe nchi itukie 😎
 
Ingepewa Simba hiyo ndege ungesemaje??
Mbona mataifa ya wenzetu wanasapotiwa na viongozi wao.

Acha kisokolokwinyo we mzee.
Haya mambo utayakuta huku kwa Waswahili tu wasiojitambua. Serikali inatoa ndege kusapoti safari ya KLABU, umeona wapi? Tena sapoti inatolewa kipindi haihitajiki, kipindi hizi klabu zinayumba kifedha umewahi kuona serikali inatoa hiyo sapoti?
 
Huwezi kwenda wakati huwezi kununua hata maji ya wachezaji, asilimia kubwa wameenda watu ambao wanaweza kuongeza motivation kwa Timu na siyo unaenda huko na hela yako ya kodi ya nyumba Kwa Mnyamani ukirudi unatimuliwa
 
Back
Top Bottom