Waliopata chanjo ya Uviko-19 Dar yafikia milioni 3.4

Waliopata chanjo ya Uviko-19 Dar yafikia milioni 3.4

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema hadi sasa idadi ya waliochanja chanjo ya Uviko-19 katika mkoa huo ni milioni 3.4.

Makalla ameyaeleza hayo leo Jumamosi Novemba 27, 2022 baada ya matembezi ya hiari yaliyoandaliwa na Huduma za Afya Aga Khan Tanzania (AKHS, T) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na Mtandao wa Mashirika ya Kimataifa ya Maendeleo ya Aga Khan (AKDN) na kufanyika jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kukuza uelewa na mwitikio wa chanjo ya Uviko- 19 kwa umma.

Amesema kiwango hicho ni zaidi ya lengo lililowekwa kwa mkoa wa Dar es Salaam la kuchanja watu milioni 3.3.

"Sensa ya watu na makazi ya 2022 inaonyesha Dar es Salaam ina watu milioni 5.3 hivyo hali ni nzuri na naamini elimu hii ikiendelea kufika kwa wananchi watu wataendelea zaidi kwenda kupata chanjo,"amesema.

Pia ametoa wito kwa wananchi kuachana na dhana potofu juu ya chanjo ya Uviko-19 na kujitokeza kupata chanjo hiyo ili jamii iendelee kuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema pamoja na kuchanja ni muhimu kufanya mazoezi ili kuimarisha zaidi kinga dhidi ya maradhi mengine na kuweka sawa afya zao.

Naye Mkurugenzi wa Tiba, Hiduma za Aga Khan Tanzania, Dk Harrison Chuwa amesema matembezi hayo ni sehemu ya programu ambayo EU na AKDN imeingia makubaliano ya mradi wa dola za kimarekani milioni 9.5 unaolenga kuboresha miitikio ya kimfumo na ambayo inazingatia jinsia ili kushinda madhara ya kiafya na kiuchumi yaliyosababishwa na janga la Uviko -19 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji.

Amesema kwa Tanzania mradi huo umetengewa kiasi cha bilioni 3.8 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Mwanza na inatarajiwa kuwafikia zaidi ya watu 700,000.
 
Back
Top Bottom