Kwanza kabisa kulingana wa Tanzania National Bureau of Statistics wame project kufikia mwaka 2010 kutakuwa na Watanzania 43,187,823.
National Bureau of Statistics
Kulingana na data hizo, ambao watakuwa hawajafikikisha miaka 18 siku ya kupiga kura 2010 wamekadiriwa kuwa ni 22,807,252. Watu wenye umri 80+ wako 287,758. Hivyo eligible and able voters ni 20,092,813. Haiwezekani kwamba NEC wameandikisha 100% ya watu wanaoweza kupiga kura. Ukichukulia 90% unapata 18,083,532. Ukiondoa wazee wengine wasiojiweza above 75 na vichaa au wenye mtindio wa ubongo tuweza ku conclude tuna maximum ya wapiga kura waliojiandikisha 18M Tanzania 2010, sio 19M na definately sio 20M.
Pili, Kwa mtazamo wangu kuna mambo mengi yaliyofanyika kuzuia wapiga kura "kujitokeza" uchaguzi huu:
1) Kwanza kuna uchakachuaji uliofanywa kwenye daftari la wapiga kura na NEC ama kwa NEC yenyewe kujua ama kutokujua (infiltration by Usalama). Watu zaidi ya 1.1M walihamishwa vituo vyao na hivyo kutoweza kupiga kura. Kwa mfano mtu umejiandikisha kituo Songea lakini huonekani huko bali unaonekana kituo Mafia. (Data hizi nimepewa na mtu anayelifanyia analysis daftari).
2) Kuna propaganda iliyofanywa kwa ufanisi sana na CCM nationwide ya kuwaogopesha watu kwamba kutakuwa na umwagaji damu siku ya kupiga kura. Aidha walitawanya habari tofauti na nyingi sana kwamba ukipiga kura upinzani "itayeyuka" one way or another na kuishia CCM au mawakala watanunuliwa kwa sh milioni moja etc. Stori za namna hii zilikuwa zimezagaa kila kona ya Tanzania (hata hapa JF) na hivyo kufanya watu kuogopa kwenda kupiga kura au kukata tamaa. Hapa wanawake walikuwa wengi nahisi idadi yao inaweza kuwa 2.5M.
3) Kuna uchakachuaji uliofanywa kitaalam wakati majumuisho au wakati wa kutangaza matokeo na Wasamamizi wa vituo (NEC/CID?). Waliweza kupunguza kura za wapinzani angalau 3,000 kila jimbo, hii inafanya idadi kuwa 600,000.
4) Kuna ambao walikuwa hawana kadi. Wale waliouza kadi zao, au kadi kukusanywa na mabalozi wa nyumba kumikumi au kubadilishana kadi na mtendaji kwa ajili ya vocha ya mbolea au simply kadi kupotea. Hawa ni kama 1M (BTW kuna watu walikamatwa wakinunua kadi au walikamatwa wamekusanywa kadi lakini pindi wanapofikishwa polisi wanatolewa mlango wa nyuma kabla hata maelezo hayajakamilishwa kutolewa. cases ziko nyingi tu). Kazi hii ya kukusanya kadi imefanyika kwa muda mrefu sasa zaidi ya miaka mitatu.
5) Kuna wale wanooishi mbali na vituo. Huko vijijini katika kila kituo kuna watu angalau 20 ambao wanaishi mbali sana na kituo, wengine hata umbali wa zaidi ya kilomita 15. Hivyo ukikadiria vituo 40,000 Tanzania bara, vijijini, unaongelea watu wapatao 800,000 walishindwa kupiga kura kutokana na umbali.
6) Kuna wale waliotaka kupiga kura lakini walirubuniwa. Wako waliohongwa wakati wa kampeni wasiende kupiga kura na kwa ujinga wao wakakubali. Wako walionyeshwa pombe wakashindwa kuamka siku ya uchaguzi. Wako waliorubuniwa barabarani wakienda kituoni. Au waliokuta vituo vimehamishwa bila wao kujua. Hawa nakadiria kuwa 500,000.
7) Wako walioshindwa kwenda kwa kuwa walikuwa safari au dharura ilitokea au ugonjwa. Hawa ni pamoja na wale wanafunzi waliojiandikisha shule nakujikuta shule bado zimefungwa wakati wa uchaguzi. Hawa wanaweza kuwa 500,000.
8) Wako wasio na elimu ya uraia. Kuna Watanzania wengi bado hawaoni umuhimu wa kupiga kura. Aidha hawaelewi, hawajali, ama ni wavivu kwenda kupanga mstari au mabishoo, au wanaona tu wanajidhalilisha au kujishusha hadhi kupanga mstari na watu wa kawaida. Hawa ni kama 2M.
Ukijumlisha jumla ya hivyo vipengele hapo juu 9M na kura zilizopigwa 8.6M unapata 17.6M. Tofauti ya Hii 17.6 na 18 (maximum) ni idadi ya majina yaliyojirudia kwenye daftari la wapiga kura pamoja na wale waliofariki lakini hawajaondolewa.
Sasa Tufanye nini?
Tujipange kuanzia sasa kwa chaguzi zijazo. Kuna mambo manne ya muhimu:
1) Daftari la wapiga kura lisiwe siri ya NEC. Wadau wote wa uchaguzi tudai daftari kabla ya chaguzi tuweze kulihakiki sisi wenyewe.
2) Tuhakikishe tuna mawakala waelewa kwenye vituo. Kutokuwa na uchaguzi uliokuwa wa haki kunamathiri kila Mtazania na sio to vyama vya siasa tu. Hakuna maana ya kuwa na uchaguzi wakati hatupati viongozi tunaowataka. Mwaka huu kulikuwa na vituo 55,000 (probably 65,000 by 2015), hili ni jukumu zito kwa chama chochote cha siasa hata CCM kupata mawakala waelewa. Tusiachie vyama vya siasa jukumu la kuhakikisha kwamba chaguzi zetu ni huru na haki. Serikali na NEC vimeshindwa kwa makusudi au kwa uzembe. Watanzania tuanzishe mikakati ya kuhakikisha kura unayoipiga inaenda kwa mgombea uliyemchagua. Tu campaign kuanzia sasa mpaka 2015 hili tatizo liundiwe mkakati liweze kutatuliwa localy.
3) TUsaidiane na vyama vya siasa, pamoja na NGOs husika kutoa elimu ya uraia. Tu mobilize wapiga kura waende kupiga kura siku ya uchaguzi kama wanavyofanya wenzetu majuu.
4) Tudai Tume huru na tuwe na sheria za uchaguzi zisizopendelea chama tawala. Bungeni lifanyike lakini sio hivyo tu bali tuwabane mabalozi/wahisani/wafadhili wailazimishe serikali yetu ibadili mfumo kama walivyoweza kutulazimisha kuingia kwenye siasa ya vyama vingi.