Elections 2010 Waliopiga kura Oktoba 31, milioni 12 walienda wapi Jumapili ile?

Elections 2010 Waliopiga kura Oktoba 31, milioni 12 walienda wapi Jumapili ile?

Haya kwa sehemu kubwa yalichangia hali hiyo:

1. Miaka mingine tulikuwa tunaandikisha kila uchaguzi unapofika na kupiga kura siku chache baada ya hapo, hili lilisaidia vilevile kuhamasisha watu wajitokeze.

2. Tangia mizengwe ya daftari la kudumu, waliojiandikisha 2005 na kuhama maeneo waliyokuwa wanaishi, kwa sababu mbalimbali hawakujitokeza kubadilisha taarifa zao [hili ndio kundi kubwa]
Ilipotolewa fursa ya ku-update daftari la wapiga kura, waliopoteza vitambulisho, waliohama maeneo yao na wale ambao hawakuwemo kabla wote walijiandikisha. Kwa uwezo mdogo wa NEC, hawakuwa na mfumo wa kuchuja taarifa za zamani na kuziondoa kwenye database yao. Ndio maana tunaambiwa eti kuna wapiga kura 19,600,000 jambo ambalo katika hali halisi lisingewezekana.

3. Kuna mazoea ya kufikiri kuwa hata tusipopiga kura walioko madarakani wangeshinda kwa njia yoyote ile na watu wengi wakadharau kujitokeza siku ile.
 
Back
Top Bottom