Waliopigania uhuru wa Tanganyika Walipigana na nani?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Hi Great thinkers.

Nafikiri kuna jambo haliko sawa hasa tunaposema tulipigania uhuru. Tulipigana na nani.?

Mi navojua ule ulikuwa ni mchakato wa kupata uhuru wa Tanganyika, Na hakuna mtu aliyegoma kutupatia uhuru eti hadi tuanze kupigania.

Ni bora isemwe tu kwamba walioongoza harakati za kupata uhuru wa Tanganyika na siyo kupigana .

Labda kama ni sielewo kiwahili vizuri kati ya harakati/Kupigana.
 
Imagine miaka 60 sasa tuna taifa la majoga ....hakuna elimu wala kujitambua...hatuwezi kusimamia haki yetu kama Taifa....sembuse miaka hiyo.....walijitahidi sana wale wazee sasa tuna key boardworriors
 
Labda mwingereza alitaka kukwepesha makubaliano ili aendelee kututawala hivyo ikabidi kitembezwe kichapo (kupigania) ili atoe uhuru kama ilivyopangwa hapo awali πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Acha ujuaji dogo janja wewe tu hapo kijitokeza hadharani kupambana dhidi ya mafisadi ya CCM unajificha nyuma ya keyboard Tena kwa fake ID hutaki hata ujulikane
 
kwa akili yako kupigania ni mpaka kupigana vita? Elimu yako ni kiwango gani maana ujinga ni mzigo mzito sana kuubeba.
 
Kulikuwa na mapigano sababu mikutano ya kisiasa ilikuwa hairuhusiwi na polisi wa kikoloni walikuwa wakipiga hata kuua wananchi waliofika kwenye mikutano, harakati za kisiasa zilikuwa ngumu sana
Mbona hapa tanzania Kuna kipindi mikutano ya kisiasa ilikuwa haipo na Hadi Daud mwangosi alifia kwenye mkutano wa siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…