Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Inawezekana hakua na umaarufu kweli na hakuchorwa kipindi akiwepo. Ila wafuasi wake inawezekana waliagiza achorwe ili kuweka kumbukizi zake sahihi.


Aisee... Yesu alipewa prom???
Labda useme alipewa promo na wafuasi/wanafunzi wake. Na hilo ndio waliloagizwa kulifanya.

"Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa kua wanafunzi wangu"

Ndio hivyo sasa kuwa Yesu hakuwa maarufu mpaka anaondoka, hivyo hakuwa anajulikana,
Watu walikuwa hawamjui, hata Watawala wa Enzi hizo hawakuwa wanamjua, ni mpaka siku anasulubishwa kama wahalifu wengine walivyokuwa wanasulubishwa ndio Watawala wakamjua.

Hivyo haikuwezekana Picha au Sura ya Yesu kuhifadhiwa Kwa namna yoyote Ile.

Zingatia, Baada ya Yesu kuondoka, lilikuwepo vuguvugu la kuwauwa wafuasi wake, Jambo hilo lilipelekea Wanafunzi wake wote kuuawa kasoro Yohana.
Kwa mazingira hayo na mengine, ni vigumu Kupata picha na sanamu yenye taswira ya Yesu.

Mwisho, utamaduni WA kiyahudi Kwa kipindi kile haukuruhusu sanamu za MTU kuchongwa.
Zingatia pia hata kama Wayahudi wangeruhusiwa kuchonga sanamu. Yesu hakuwa na Sifa na vigezo hivyo
 
Ndio hivyo sasa kuwa Yesu hakuwa maarufu mpaka anaondoka, hivyo hakuwa anajulikana,
Watu walikuwa hawamjui, hata Watawala wa Enzi hizo hawakuwa wanamjua, ni mpaka siku anasulubishwa kama wahalifu wengine walivyokuwa wanasulubishwa ndio Watawala wakamjua.

Hivyo haikuwezekana Picha au Sura ya Yesu kuhifadhiwa Kwa namna yoyote Ile.

Zingatia, Baada ya Yesu kuondoka, lilikuwepo vuguvugu la kuwauwa wafuasi wake, Jambo hilo lilipelekea Wanafunzi wake wote kuuawa kasoro Yohana.
Kwa mazingira hayo na mengine, ni vigumu Kupata picha na sanamu yenye taswira ya Yesu.

Mwisho, utamaduni WA kiyahudi Kwa kipindi kile haukuruhusu sanamu za MTU kuchongwa.
Zingatia pia hata kama Wayahudi wangeruhusiwa kuchonga sanamu. Yesu hakuwa na Sifa na vigezo hivyo
Tatizo lako unapenda ubishi....?
 
Huwezi kuamini uwepo wa Mungu halafu usiukubali Utatu mtakatifu. Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu. Toka miaka miaka watu waliomuamini Mungu walikua na dini.
Nakijua nachokisema.

Utatu ni masonry,

Catolicano ni Juzi tu ndo wameweka Roho MTAKATIFU kwenye utatu,

Mwanzo ilikuwa utatu wa BABA,MWANA na mungu mke aliyejificha nyuma ya bikra mariem,

Kilichofanywa na warumi ni kuchukua miungu Yao na kuichanganya na mapokeo ya INJILI na kuiita dini.

Acheni IBADA za sanamu,

Mungu ni MMOJA, Hana NAFSI tatu.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Kama Mwamposa na Kuhan Mussa ni maarufu ambao wanafanya vimiujiza vidogo vidogo kwa kutumia jina la Yesu, sembuse Yesu mwenye jina lake ambaye alikuwa anafanya Miracle kubwa zaidi zilizoshindikana vipofu wanaona, viziwi wanasikia, viwete wanatembea na wafu wanafufuka.

Mtu ambaye alichukiwa na kupingwa na wazee wa kanisa, viongozi wakubwa, pamoja na wafalme wakubwa wa zama hizo. Unathubutu kusema hakuwa maarufu.

Mbona inahitaji uelewa wa kawaida sana mtu kuelewa sijui nyie mataikon mnafeli wapi?

Kasome hapa
Mathayo 26:
48 Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” 49 Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.

Kama Yesu angekuwa maarufu na anayejulikana Yuda asingewaambia hao maaskari maneno hayo.

Kama Yesu angekuwa mashuhuri na maarufu wala asingewapa Wanafunzi wake Misheni ya kumtangaza yeye na habari zake.

Vinginevyo haujui maana ya MTU maarufu na mashuhuri
 
Kasome hapa
Mathayo 26:
48 Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” 49 Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.

Kama Yesu angekuwa maarufu na anayejulikana Yuda asingewaambia hao maaskari maneno hayo.

Kama Yesu angekuwa mashuhuri na maarufu wala asingewapa Wanafunzi wake Misheni ya kumtangaza yeye na habari zake.

Vinginevyo haujui maana ya MTU maarufu na mashuhuri
Nipe kwanza maana ya neno maarufu?

Sipo hapa kubishana.
 
I hope y'all are doing just fine, It has been long time since I was here[JF Inteligence]
View attachment 2545863
Kuna mtu alileta mada humu akiuliza kwamba picha inayotumiwa na wakristo hasa wakatoliki ya mtu mmoja mzungu kua “ndie” yesu, je hiyo picha ni ya Yesu kweli? Akaongeza kwa kusema kwamba wakati yesu akiwepo kulikua hakuna teknolojia ya Photography wala Motion Picture…So wao waliitoa wapi picha hiyo na wana ushashidi upi kwamba yule ndio Yesu mwenyewe??

I’m glad you asked coz I would like to use this moment to Splendid Explain these stuffs to you!


Toka dunia kuumbwa, dunia imeshuhudia kuzaliwa kwa watu wawili wenye akili zaidi.watu hao walikua wenye uwezo wa kujifunza mambo wao wenyewe yaani Autodidacts na walikua wana uelewa na uwezo wa kufanya mambo meengi kwa wakati mmoja yaani Polymaths…watu hao si wengine bali ni Imhotep kutoka Misri ya zamani (Ancient Egypt) na Leonardo Da’Vinci kutoka Sicily Rome.

Imhotep alikuwepo duniani Zaidi ya miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Da’Vinci, Da’Vinci kazaliwa miaka 600 iliyopita yaani 1400s.Imhotep alikua kuhani mkuu wa mungu mkuu wa wamisri aitwaye mungu jua Ra, mbali na hayo jamaa alikua mbobevu katika hesabu,fizikia na biology hivyo alijikita sana katika usanifu wa majengo na tiba mbalimbali. Ukiziona Pyramids zilizopo misri wala usidanganyike kua alien ndio wamejenga bali ni huyu Inhotep ndio alizisanifu.

Wagiriki walimuabudu huyu mtu kama mungu wao wa tiba kutokana na mchango wake mkubwa katika tafiti zake zi kitabibu.

Kwa waliosoma mada zangu kadhaa zilizopita nilielezea jinsi utawala wa Ugiriki ulivyotokea na kuanguka na matokeo yaliyotokea baada ya ugiriki kuanguka. Kwa ambao hawajasoma nitaelezea kwa ufupi sana nini kilitokea.
Miaka ya nyuma ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo 100 na kila mji na ulikua na utawala wake japo walikua wakiungana na kusaidiana pindi uvamizi unapotokea, enzi hizo superpower wa dunia alikua Persia yaani Iran ya sasa. Iran ilikua inajitanua kwa kuvamia maeneo na kuyachukua hapo ndio alipoikaribia Ugiriki akitaka aanze kuchukua mji baaada ya mji, hapo ndio unakutana kisa cha mfalme Leonidas wa jiji la Sparta.

Vumbi ilitimka kweli kwa wapenzi wa muvi waliotazama muvi ya 300 na 300 Rise of Empire wanaelewa.
Baada ya vamizi kadhaa zilizokua zinafanywa na nchi kubwakubwa wagiriki wakaamua kuungana na kutengeneza nchi moja ya Greece. Mikaka ikaenda akatokea alexander the great akaikuza sana Greek, akaanzisha mji wake ulioitwa Alexandria katika nchi ya Misri. Kipindi hicho misri ilikua ndio hazina na kitovu cha Elimu dunia nzima.
View attachment 2545869
[Mwigizaji Gerald Butler aliyeigiza kama mfalam Leonidas wa sparta kutoka muvi ya ]

Wanafalsafa wengi na walienda hapo kusomea, hata mwandishi wa injili Luka alisomea hapo. Miaka ikaenda baada ya Ugiriki kuanguka Superpower aliyeibuka akawa Rome, Rome ilienda kuchukua kila kitu kilichokua misri wakakihamishia kwao. Maarifa yote yaliyokua Misri kwenye Maktaba ya kwanza kuanzishwa duniani yalihamishiwa Rumi.

Wakati nchi ya Israel ikitawaliwa na Rumi anazaliwa Yesu anafanya kilichomleta duniani kisha anafariki miaka 33 baadae, wafuasi wa Yesu wanaongenzeka na kupata ushawishi mkubwa katika serikali na maeneo mengi duniani.

Kwa wanaopenda Conspiracy, inasemaekana baada ya utawala wa Rumi duniani kuanza kuanguka watu wenye kufikiria mbali (futurist) wakiongozwa na mfalme Nero walikabidhi madaraka kwa wafuasi wa Yesu Kristo wa kipindi hicho ili Rumi iendelee kutawala dunia kupitia mlango wa nyuma (indirectly) ndipo ukristo ukatambuliko rasmi duniani kama Roman Catholic na wakapafanya Rumi kama ndio makao makuu ya Ukristo badala ya Yesrusalemu. (Sina uhakika kama nadharia hii ina ukweli ndani yake ila ina make sense sana maana wote twafahamu nguvu na ushawishi iliyonayo RC katika mataifa mbalimbali)

Miaka kadhaa tawala ya Rumi inaanguka, Ukatoliki ukawa umeenea maeneo mengi na ushawishi mkubwa ulimwenguni anazaliwa Leonardo Da’Vinci 1452, kutokana na uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali kila alichokifanya kiliweza kua Perfecto. Davinci aliweza kuifanya tasnia ya uchoraji kua kubwa na yenye thamani sana kutokana na kazi zake bora na zenye kufikirisha za uchoraji.

Ni moja kat ya wachoraji wakubwa kuwahi ktokea hapa duniani kuna vitu kachora hakuna mwingine anayeweza kuchora labda urumie Powerful software…kama utanibishia jaribu kuchora duara na pembe nne vikiwa pamoja kama alivyochora mchoro wake wa Vitruvian man… Jamaa alikua anaweza kujichora yeye mwenyewe sura yake…Baadae anazaliwa Michelangelo ambae na kwa kiasi Fulani alijitahidi sana katika uchoroja unaweza kujionea michoro yake ya Sistine Chapel iliyopo hapo Vatican, lakini pia nae alibobea katika uchonganji (sculptures)
View attachment 2545902
[Sistine Chapel]
Inahusiana vipi na Picha ya Yesu…?

Kama nilivyoeleza huko juu Baada ya Ugiriki na Misri kuanguka na Rumi kuibuka kama Superpower alibeba maarifa yote yaliyokua Rumi na Ugiriki na kuyahamishia Roma, hivyo baada ya rumi kuanguka kanisa katoliki likabaki limeshikilia maarifa kutoka pande zote za dunia hasa misri,ugiriki na Israel. Leo hii hakuna taarifa au maarifa ambayo hayapo Vatican…Vatican inamiliki moja kati ya eneo lenye kulindwa Zaidi duniani ambalo hua haiingii huko mtu bila ruhusu maalumu…Hata Pope inabidi apate kibali kutoka kwa kiongozi wa Jesuists ndio anaweza kwenda huko.

Hivyo basi sidhani kwamba kanisa katopliki wanaweza kua wameshindwa kupata piacha ya yesu wakati wameweza kumiliki taaroifa za kutoka kila pande ya dunia. Kama Plato,Socrate, nk picha zao zipo na waliishi miaka mingikabla ya yesu haiwezekani yeye picha yake isiweze kupatikana.

Nimesema kipindi hicho taaluma ya uchoraji na uchongaji ilitumika Zaidi katika kuweka kumbukumbu za watu mbalimbali ndio maana leo ukiitaka picha ya Plato unaipata, kuna watu wamejaliwa uwezo mkubwa wa uchoraji unaweza kumuelezea kwamba Fulani sura yake ipo hivi na hivi na akaichora kama ilivyo. Njia hii hutumiwa sana na mashirika ya usalama hususan FBI na polisi. Tena sasa hivi kuna msaada wa softwares yaani ukimuelezea mtu anakutulea mchoro kama picha halisi…hivyo basi natumaini hata picha ya yesu watu wa zamani walitumia njia hiyo kuhifadhi taswira ya Kristo.

Ndio maana utakuta picha hiyo inayotumika sura yake ipo mahali pote sio tofauti. Hata miaka ya 1970s wakati wanaandaa filamu ya yesu walijaribu watu Zaidi ya waigizaji 200 ambao watafanana na Sura hiyohiyo ni Brian Deacon pekee ndio alifanikiwa kufit kwenye role hiyo kutokana na sura yake kufanana na sura inayotumika kuwasilisha taswira ya Kristo.
Ndio maana wasiojua wanapoona hiyo taswira ya yesu hua wanasema kwamba ni sura ya mwigizaji Brian Deacon…Si kweli, kwa maarifa waliyonayo RC hawawezi ruhusu hilo.

So kwa kuhitimisha ni kwamba Wakatoliki kukubali kuruhusu picha hiyo ya Yesu kutumika sio wajinga hata kidogo kwamba hawafahamu taswira halisi ya Kristo.
Kuna kitu kinaitwa Sanda la torino imebeba vitu VINGI sana ni kama negative ya picha ya MTU lakini ina umri mkubwa sana ili fanyika mbinu nyingi za kuteketeza ikashindikana
 
Nipe kwanza maana ya neno maarufu?

Sipo hapa kubishana.

KiswahiliEdit. NominoEdit. maarufu. ni kujulikana hasa katika sanaa au kisiasa; umaarufu pia kuwa unajulikana kitaifa na hata kimataifa.

Huyo Yesu hata Askari wenyewe walikuwa hawamjui.
Rejea Yuda akiwaambia hao maaskari.

MTU maarufu au mashuhuri Kwa mfano kama Mwamposa, Askari au Watu wa kawaida wa Hapa Dar es karibu wote wanamjua.

Yesu alikuwa mgeni katika jiji la Jerusalem
 
Labda angejadiliwa Imhotep ningeridhika zaidi,,da Vinci tabia yake ya ushoga ilimfanya credibility yake kuwa tarnished maana anaweza kuwa pia alikuwa na kichaa,, na watu wengi wachonga vinyago wanasema hizo taswira wanazochonga Huwa wanazipata kwa zenyewe kuwajia ndotoni.Kwa hio hizo picha za da Vinci atakuwa pia aliletewa ndotoni na Pengine hao viumbe waliomletea ndio watakuwa ndio walioanza kumpakua....

NB..Tumeshauriwa tusinunue vinyago na kuviweka ndani,,,,nadhani pia ni hatari kwa mtu asie na uhusiano na Siri za dada Vinci kuweka mapicha yake ndani fate yake haikuwa nzuri.
 
Labda mimi sielewi maana ya maarufu?

Tukubaliane kwanza maana ya neno "maarufu"?

Dadavua nami nipate kuelewa?

Then turudi kwenye majadiliano.

Ndio maana tukapishana,

Maarufu na mashuhuri ni MTU anayefahamika/julikana iwe kitaifa au kimataifa.

Sasa Yesu bado hakuwa katika hiyo stage katika Wakati wake.

Umaarufu wa Yesu umeanza Baada ya Dola la Rumi kuichukua dini ya Ukristo kama dini ya kirumi, kisha kuisambaza Kwa UPANGA,
Kisha wakaja Wazungu.
Vinginevyo huyo Yesu wala usingemjua hata Wewe Kwa sababu kimsingi Hana maajabu bila ya Promo
 
KiswahiliEdit. NominoEdit. maarufu. ni kujulikana hasa katika sanaa au kisiasa; umaarufu pia kuwa unajulikana kitaifa na hata kimataifa.

Huyo Yesu hata Askari wenyewe walikuwa hawamjui.
Rejea Yuda akiwaambia hao maaskari.

MTU maarufu au mashuhuri Kwa mfano kama Mwamposa, Askari au Watu wa kawaida wa Hapa Dar es karibu wote wanamjua.

Yesu alikuwa mgeni katika jiji la Jerusalem
Hadithi zako dhaifu Huwa unazipata kutoka kitabu Gani?
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa, Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Hawa wasabato wakiacha unafiki mbingu ipo wazi direct kwa ajili yao. Waache unafki tuuuuu
 
Muhammad alikuwepo miaka 600 baada ya kristo sitaki kuamini warabu hawakutunza kumbukumbu yake maana nao walikua vizuri kiteknolojia

Mimi huwa nataka kujua. Kama Muhammad SAW alikuwepo miaka 600 baada ya Kristo Yesu na Muhammad ndio alishushiwa Quran ma tunaamini ilishushwa na haikuandikwa kama Biblia ilivyo. Iweje Quran ina Hadithi/ Story ambazo ni Copy and paste kutoka kwenye Biblia??


Inakuaje Mungu anamshushia Muhammad Mambo ambayo watu walisha andika yapo documented tayari?

Hii napenda kujua [mention]Da'Vinci [/mention]
 
Kwanza nikukanushe dunia haijawai kuwa na watu wenye akili kama mnavyodangwanywa.

Pili uwepo wa wachoraji wenye akili na uwezo mkubwa wako wengi sana hata mitaani wapo, njoo uwaone watoto wanaoweza kukuchora mpka maungo yako ya sirini.

Tatu historia ya dunia imepindishwa kwa faida ya mzungu Tu, je vipi kuhusu Kemet iliyoongoza dunia nzima kwa zaid ya miaka 6000? Vip kuhusu utawala wa South afrika ya kale kabla ya ukolon, naongelea zaid ya miaka 5000bc sio hizo falme zenu za juzi hizo walizoongoza wafalme vibaraka, na je vip kuhusu ufalme wa Ethiopia ama kush ya kale ambayo ilikuwepo zaid ya miaka 6000 bc, siongelei hiyo ethiopia ya leo ya vibaraka wa kidini waliopewa Biblia za mchongo kuupa nguvu ukristo feki.

Dunia na historia mnayofundishwa ni kama 10% ya historia mnayotakiwa kujifunza, maana mashulen mnaanzia kusoma hivyo vijifalme vya waajem sjui warumi na takataka za kizungu, kumbe waliwai kuwepo wahindu, wachina na Waafrika kabla ya hizo dola za karibuni.

Kama dunia imepita maelfu ya miaka kwann mjifunze kuhusu historia inayogusa miaka maximum 7000 tu je miaka 30000 b.c nini kilikuwepo? Ni nani alitawala? Na wakina nani waliounda misingi ya dunia hii?

Jibu mnalipata kuwa mtu wa mwisho kupata dola kuongoza dunia kwa ujanja yaan mrumi ndie aliyeharibu historia hii ya dunia.

Dunia inanza ambapo maelfu ya miaka iliyopita kabla ya mgawanyo wa mabala, then inakuja historia ya chanzo cha Races dunian na mgawanyo wa makabila na matabaka ya rangi za watu+wanadamu, then inakuja historia ya falme 5 kubwa zilizotawala dunia miaka mingi iliyopita.

Ndipo zinakuja nyakati za giza ambapo warumi waliiba historia za watu wa kale na Jemedari wa kale wa jamii ya kiafrika ambaye babu za mama yake waliishi afrika mashariki ama babilon ya kale ama pia Edeni ya kale na baadae kuhamia central afrika ama Yerusalem ya kweli ya kale, na huko jemedari huyo alizaliwa kimiujiza yaan alizaliwa na Mama pasipo mimba yake kutungwa kwa muingiliano wa Me+Ke na hiyo zamani ilikuwa jambo la kawaida kwa mababu waliojua siri ya nguvu za Nuru Rohoni.

Mtu huyo alizaliwa afrika kwa mission maalumu na alikuwa mweusi kwakuwa Africa ni ya watu weusi, na mtu huyu alifanyiwa janja janja na wanadamu wa ngozi nyeupe kuuwawa, lkn alifufuka kimiujiza baada ya mission yake kukamilika aliondoka dunian kimazingara na kurudi Makao yake ambako ni nje ya mbingu za viumbe wa Roho za Nuru.

Mtu huyu ndiye habari zake wazungu wa kirumi waliiba na kukitengeneza kiumbe kiitwacho yesu kwa kukipa historia ya mtu huyo, na yesu huyo kibinadamu ni ufanano wa mwana wa mfalme wa rumi ya miaka ya 320, ivyo basi Yesu kama yesu hajawai kuwepo, Viongozi wenu wanayajua haya mambo.

Ubapozungumzia yesu unakuwa unamzungumzia JINI azazel/Zeus ambaye kiroho ni Jini/pepo lkn kibinadamu alipewa uhusika wa mtu mwenye ufanano na mwana wa mfalme wa rumi, ambaye ndie wakina Leonard da vinch walimchora, na Jini hili ndilo hucontrol tabia za ushoga&usagaji ndiomaana viongoz weng wa kidini wakipagawa na pepo hili huishia kuwalawiti watoto mfano mapadri&mashekhe wote wanatumia nguvu za hiki kiumbe.

Rumi hiyo ndio inatawala dunia leo hii kupitia mashirika mbalimbal dunian kama UN, WHO, UNHCR, mashirika ya muvi kama Hollywood, mashirika ya technolojia kama NASA, mashirika ya usambazwaji habari na media zote kubwa na mitandao mikubwa ya kijamii kama Fb, whatsApp, instagram, jamii za siri kama freemason&illuminat, mifumo ya siasa kama ubepari, ujamaa, mifumo ya kidemokrasia, pia Taasisi za Dini zote za ukristo&uislam ni mali yao hawa jamaa, hata lile taifa pendwa la israel ya mchongo ni wao walilitengeneza kwa kuakisi maisha ya wayahudi wa kwel ambao waliishi afrika na ambao ni watu weusi, na Taifa teule la kweli lilikuwepo hapa Africa central afrika katikati mwa afrika kutokea Eden ya kweli ambayo ni East Africa.

Jua kuwa picha ya yesu iliundwa kwa makusudi na lengo kubwa na Target ni mtu mweusi Tu, huko kwingine dunian hawahangaik nako bali Africa,

Ndioamaana ilitumika nguvu kubwa kueneza filam ya yesu kupitia mashirika ya kidini mikutanon na masemina mliyokuwa mkioneshwa Projection ya sinema ya yesu then majarida na vipeperushi mpaka leo wanagawa mashulen kwa watoto wanawaharibu akili mapema ili wasije kuujua ukweli.

Nguvu hii inayotumika kumdanganya mtu mweusi kupitia mafunzo ya kidini, ndio ile ktk dini zenu mnaita Chapa ya 666 yaan kumfanya mtu halisi wa dunia(mtu mweusi) asahau utambulisho wake kwa kutaka ama kutotaka ndiomaana mafunzo haya ama uongo huu haukwepeki kirahisi na ukiukwepa ni vigumu kusurvive dunian maana utatengwa na nchi zote kuwekewa vikwazo vya kila namna ama kuuwawa,

Na ukiukubali uongo huo ndio pale unakuwa umekufa kiroho kwa kukubali chapa ya mafundisho ya uongo, hivyo sahau kuhusu Ufalme wa mbingu, labda kwa Neema sana kulingana na matendo yako dunian.

Narudia tena, huyo yesu hajawai kuwepo, stori zoote za dini zote ni uongo, mitume wote na manabii waliishi Africa na walikuwa watu weusi, hamuwezi kuambiwa haya na wachungaji wenu maana watauwa soko la makanisa, jarbu kupeleleza utatajua haya.

Dunia inaongozwa na shetan mwenyewe by 100% dunian wanamuabudu shetan uwe unapenda ama hupendi ukweli ndio huu ama vip urudie asili ya kumuabudu muumba wa kweli ambaye wazungu na waarabu walichakachua mafundisho yake.

Niishie hapa msijekuchanganyikiwa.

Tawala za nyuma na za kati zimepuuzwa. Dunia ya leo ipo related na Kristo ndio maana tunatumia Tarehe inayohusiana na Kristo
 
Mimi huwa nataka kujua. Kama Muhammad SAW alikuwepo miaka 600 baada ya Kristo Yesu na Muhammad ndio alishushiwa Quran ma tunaamini ilishushwa na haikuandikwa kama Biblia ilivyo. Iweje Quran ina Hadithi/ Story ambazo ni Copy and paste kutoka kwenye Biblia??


Inakuaje Mungu anamshushia Muhammad Mambo ambayo watu walisha andika yapo documented tayari?

Hii napenda kujua [mention]Da'Vinci [/mention]
Mkuu swali lako nalipeleke kwa maustadhi adriz Kisai FaizaFoxy
 
U
Mimi huwa nataka kujua. Kama Muhammad SAW alikuwepo miaka 600 baada ya Kristo Yesu na Muhammad ndio alishushiwa Quran ma tunaamini ilishushwa na haikuandikwa kama Biblia ilivyo. Iweje Quran ina Hadithi/ Story ambazo ni Copy and paste kutoka kwenye Biblia??


Inakuaje Mungu anamshushia Muhammad Mambo ambayo watu walisha andika yapo documented tayari?

Hii napenda kujua [mention]Da'Vinci [/mention]
Usiandikie mate na wino upo, weka japo aya (verse) moja ya biblia ambayo unaiona wewe kuwa ni original na weka verse ya Qur'an ambayo unaidhania wewe kuwa ni "copy" ya hiyo original.

Tunasubiri.

Ukishindwa kuleta ina maana umezusha tu. Uje kutuomba msamaha wana jamvi kwa uzushi wako
 
U

Usiandikie mate na wino upo, weka japo aya (verse) moja ya biblia ambayo unaiona wewe kuwa ni original na weka verse ya Qur'an ambayo unaidhania wewe kuwa ni "copy" ya hiyo original.

Tunasubiri.

Ukishindwa kuleta ina maana umezusha tu. Uje kutuomba msamaha wana jamvi kwa uzushi wako

Kwamba hujui kuna habari kwenye Quran na Biblia zinafanana? kwa kuanzia kisa mpaka majina ya watu hujui hilo au unajitoa ufahamu.

nakuja na facts soon
 
Back
Top Bottom