Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
WALIOSHINDWA KUMSHAURI VIZURI HAYATTI MAGUFULI WAONDOLEWE KWENYE UONGOZI
Na, Robert Heriel.
Katika makala yangu niliyoandika mwaka juzi, niliyoipa kichwa kisemacho "Njama za Ikulu, hata Rais anaweza kudanganywa" nilieleza namna kiongozi anavyoweza ingizwa mkenge au kujiingiza mkenge pasipo yeye kujua, na mwishowe akaja kushtuka mambo yakimuendea mrama. Nilitoa mifano mingi, baadhi ikiwa kwenye Biblia, kama vile kisa cha Mfalme Nebukadreza na Daniel ambapo kisa hicho mfalme anaingizwa mkenge na washauri wake zaidi ya mara tatu pasipo yeye kujua, akija kushtuka picha limeisha. Kisa cha Mfalme Herode na Yohana Mbatizaji, ambapo Mfalme anaingizwa mkenge na Herodia(mke wa kaka yake herode, aitwaye filipo) Mfalme anagundua ameingizwa mkenge lakini hana cha kufanya zaidi ya kumungamiza Yohana. Kisa cha Pilato na kumsulubisha Yesu, Pilato anajiingiza mkenge kwa uchu wa madaraka kwa kuhofia kutochaguliwa tena kwani ulikuwa mwaka wa uchaguzi, hivyo akamsulubisha Yesu kwa ushawishi wa wazee wa baraza waliotafuta vijana wamshinikize Pilato amhukumu Yesu.
Rais anaweza kuwa mzuri kiuongozi lakini akajikuta kwenye taabu kutokana na kuchagua madubwasha yenye nia Ovu. Rais hata awe mzuri vipi kama wanaomzunguka ni madubwasha lazima waboronge. Pia, Rais anaweza kuwa mbaya kiuongozi lakini kama wanaomzunguka ni watu bora basi lazima afanye vizuri. Ndugu yangu Ole Mushi katika makala zake aliwahi kuandika Rais lazima azungukwe na watu wenye maarifa, hekima, ujuzi, na watu wema. Ole Mushi akaongeza kuwa watu bora ni mali ya Rais/ Mfalme. Naungana na Mushi kwa 100%.
Hayati Magufuli pengine alikuwa na nia nzuri na yapo mambo mengi mazuri ambayo aliyafanya, lakini hatuwezi kuwa wanafiki kuwa yapo mabaya makubwa ambayo yalifanyika, ndio maana sishangai kuona baadhi ya viongozi wakijitokeza kipindi hiki na kujifanya kuomba radhi kwa mambo yaliyopita.
Huu sio wakati wa kulaumiana, lakini hatuwezi puuzia uzembe uliofanyika, kwa maana kwa mambo bora tutapongeza na kuwapa sifa walioyafanya, na kwa mambo mabaya tutayalaani na kuwawajibisha wote waliohusika.
Wale wote walioshindwa kusema ukweli hawatufai katika uongozi, wale wote walioshindwa kukemea maovu yaliofanyika mathalani mauaji, utekaji, kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, hao wote hawatufai katika kutuongoza.
Ikiwa mtu alikuwa kiongozi akashindwa kushauri kwa kuogopa kusema ukweli, huyo hana sifa ya Uongozi.
Viongozi wote walioshindwa kumshauri vizuri Hayati Magufuli wanafahamika, na wanajijua, waondolewe haraka kwenye nafasi zao kwa kushindwa kuongoza.
Uongozi sio kuongea ongea kwenye media, kuongoza sio kutisha watu, sio kujifanya mtabe, kujifanya wewe ndio unahaki zaidi kuliko unaowaongoza.
Tunahitaji viongozi wenye mfano wa kina Mhe. Antony Mtaka, sio viongozi kucha kuchwa kwenye vyombo vya habari, na mitandao ya kijamii. Viongozi wa show off waondolewe kwani wana mambo kama wanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza, kila kitu media, kamera, na instagram.
Hatutaki viongozi wanaotaka kujigeuza miungu watu, badala watake kuheshimiwa wao wanataka kuogopwa, uogopwe kwa kipi hasa, kwa cheo au kwa hizo milioni 100, au kwa kipi hasa. Kila siku naandikaga hapa kuwa, anayeogopwa ni MUNGU na watu wote wacha Mungu, ukitaka kuogopwa basi tenda wema, haki na kuwa na upendo. Sio ulete ushamba wako na ulimbukeni wako wa madaraka, cheo kidogo unatak watu wakusujudie, vipesa kidogo unataka kujifanya nawe umo kumbe haupo na unajijua haupo. Hatutaki viongozi wanaojihadaa wao wenyewe.
Viongozi wote waliokuwa wanataka Hayati Magufuli atawale milele waondolewe, kwani walionyesha upumbavu usioelezeka, mtu anajua kabisa Katiba inasema Rais ataongoza miaka mitano katika awamu ya kwanza, kisha kama atachaguliwa tena ataongoza miaka mingine mitano katika awamu ya pili na ya mwisho, jitu halielewi, linakazana na aongezewe miaka, haya licha ya Mhusika mwenyewe kukataa kuwa hataongeza na hataki kuongezewa miaka bado baadhi ya viongozi wanajitoa akili.
Napendekeza viongozi wote waliotaka Hayati Magufuli aongezewe muda, wachunguzwe, kwa maana sio kawaida kabisa, japo ni maoni yao lakini uchunguzi ufanyike.
Kama walishindwa kumshauri Hayati Magufuli basi hawataweza kumshauri Rais Samia Suluhu zaidi ya kumletea unafiki.
Kiongozi yeyote asiyeweza kushauri vizuri ni lazima atakuwa ni mnafiki.
Kushauri vizuri ni nini?
Kushauri vizuri ni kumpa mtu mawazo mazuri, kumpongeza, na kumkosoa pale anapotekeleza jambo fulani. Mtu anayepongeza tuu pasipo kukosoa huyo sio mshauri mzuri, ni MNAFIKI.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Mlali, Morogoro