Waliosomea shahada ya mifugo, misitu, kilimo, kuitwa Afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo. Lakini waliosomea shahada ya elimu hawaitwi afisa elimu

Waliosomea shahada ya mifugo, misitu, kilimo, kuitwa Afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo. Lakini waliosomea shahada ya elimu hawaitwi afisa elimu

Walimu hawana posho ndiyo maana wanategemea mishahara 100%, sitaki kuwalaumu CCM imewageuza kuwa tegemezi

Mimi mwenyewe sitaki kusema kwamba CCM inawafanya matoy yao hapana walimu hawana overtime ambapo walio wengi wanatoka shuleni hadi saa 12 jioni, walimu walitakiwa kuwekewa japo posho ya nauli na mawasiliano, walimu wengi wamepanga au wamejenga kwa gharama zao walitakiwa walipwe japo kidogo house allowance halafu ukijumlisha hizo posho wangelipwa katikati ya mwezi ili inapofika mwisho wa mwezi wapewe mishahara yao iwe kama askari wanavifanyiwa
 
Kuna Dea.Reo.Deo.Dao.SLo na Aek.
Dea-wizarani(tamisemi), Reo(Mkoani), Deo,Dao na Slo(wilayani)mwisho Aek(katani)(Wana posho)

Chini

Walimu-wengi(hawana posho)

Lazima watofautishe wakuu na wachini
 
Mleta mada ana hoja,na ni kweli hawaitwi maafisa elimu badala yake hicho ni cheo cha kiutendaji na si kwa ajili ya elimu (shahada).tuliweke sawa hili kwa mwenye uelewa atuweke sawa
Hata waliosomea udaktari hawaitwi afisa daktari.
Labda waitwe afisa mwalimu maana wamesomea ualimu siyo elimu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Na bado kuna wahuni tu mtaani wanaitwa maafisa wa NIDA, mwalimu unapenda sifa wewe khaa!
Siyo sifa bali ni heshima! Napenda heshima maana ni stahili kama ilivyo stahili kwa wengine wenye kiwango sawa cha elimu.
 
Hata waliosomea udaktari hawaitwi afisa daktari.
Labda waitwe afisa mwalimu maana wamesomea ualimu siyo elimu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Ualimu unasomewa ngazi ya cheti na stashahada tu. Hakuna shahada ya ualimu. Shahada inaitwa " Bachelor of Education in Arts, Bachelor of Education in Science nk" Hakuna shahada ya Bachelor of teaching!! Waliosomea udaktari wanaitwa Medical officers!! Labda uamue kuwa mbishi tu lakini ukweli ndio huo.
 
Ualimu unasomewa ngazi ya cheti na stashahada tu. Hakuna shahada ya ualimu. Waliosomea udaktari wanaitwa Medical officers!! I
Yap ni shahada ya elimu

Screenshot_20220504-135124.jpg
 
Na hao maafisa elimu siku hizi wamejaa sana mtaani hawana ajira.
 
Hii imekaaje? Waliosomea nyanja ya mifugo, misitu, kilimo, uuguzi, nk katika ngazi ya shahada na kuendelea hutambuliwa kama maafisa katika nyanja zao kama vile afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo, afisa uuguzi nk, na jamii kukubali kuwa wanastahili kutunukiwa uafisa katika maeneo yao ya utaalamu. Linapokuja suala la waliosomea nyanja ya ELIMU katika ngazi ya shahada ikaonekana HAWASTAHILI KUITWA MAAFISA katika eneo lao la utaalamu!! Waitwe tu waalimu! Hapo awali walikuwa wanaitwa maafisa elimu, lakini WAKAFUTIWA hadhi hiyo ya uafisa!! Sielewi kitu gani kinafanya walimu wabaguliwe hivyo kwa wazi kabisa! Hii ni dharau kubwa kwa wataalamu wetu wa elimu, halafu watu wanashangaa kwa nini elimu yetu inashuka!
Una uhakika kuwa Waalimu hawaajiriwi kama Maafisa Elimu?

Kafanye research upy
 
Una uhakika kuwa Waalimu hawaajiriwi kama Maafisa Elimu?

Kafanye research upy
Walikuwa wanaajiriwa kama maafisa elimu hapo awali. Lakini baadaye wakafuta hiyo na wakawa wanaajiriwa kama waliimu. Hata ajira zilizotangazwa hivi karibuni na TAMISEMI wataajiriwa kama waalimu. Sehemu ya tangazo hili hapa:

Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry na Biology; v. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu wa somo la English Language, English Literature, Chinese Language, French Language na Kiswahili; vi. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Commerce, Accountancy na Economics;

Ingia tovuti ya Tamisemi uhakiki hilo. Haihitaji utafiti, inahitaji kuingia tovuti ya Tamisemi na kuhakiki hilo. Scheme of service ilishabadilika miaka mingi iliyopita. Wakanyang'anywa uafisa Elimu na kupewa ualimu.
 
Walimu hawana posho ndiyo maana wanategemea mishahara 100%, sitaki kuwalaumu CCM imewageuza kuwa tegemezi
Hizi kazi mbili za ualimu na upolisi sidhani kama mtu wa idara hiyo angetamani mwanae aje kusoma kuwa mtumishi wa idara hizo kama yeye. Serikali huwatumia kama vikaragosi vyao.
 
Hii imekaaje? Waliosomea nyanja ya mifugo, misitu, kilimo, uuguzi, nk katika ngazi ya shahada na kuendelea hutambuliwa kama maafisa katika nyanja zao kama vile afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo, afisa uuguzi nk, na jamii kukubali kuwa wanastahili kutunukiwa uafisa katika maeneo yao ya utaalamu. Linapokuja suala la waliosomea nyanja ya ELIMU katika ngazi ya shahada ikaonekana HAWASTAHILI KUITWA MAAFISA katika eneo lao la utaalamu!! Waitwe tu waalimu! Hapo awali walikuwa wanaitwa maafisa elimu, lakini WAKAFUTIWA hadhi hiyo ya uafisa!! Sielewi kitu gani kinafanya walimu wabaguliwe hivyo kwa wazi kabisa! Hii ni dharau kubwa kwa wataalamu wetu wa elimu, halafu watu wanashangaa kwa nini elimu yetu inashuka!
Mbona Yesu aliitwa mwalimu na hakuitwa Afisa Elimu?
 
Hii imekaaje? Waliosomea nyanja ya mifugo, misitu, kilimo, uuguzi, nk katika ngazi ya shahada na kuendelea hutambuliwa kama maafisa katika nyanja zao kama vile afisa mifugo, afisa misitu, afisa kilimo, afisa uuguzi nk, na jamii kukubali kuwa wanastahili kutunukiwa uafisa katika maeneo yao ya utaalamu. Linapokuja suala la waliosomea nyanja ya ELIMU katika ngazi ya shahada ikaonekana HAWASTAHILI KUITWA MAAFISA katika eneo lao la utaalamu!! Waitwe tu waalimu! Hapo awali walikuwa wanaitwa maafisa elimu, lakini WAKAFUTIWA hadhi hiyo ya uafisa!! Sielewi kitu gani kinafanya walimu wabaguliwe hivyo kwa wazi kabisa! Hii ni dharau kubwa kwa wataalamu wet wa elimu, halafu watu wanashangaa kwa nini elimu yetu inashuka!
Tatizo hixo kada zingne wapo Wachache tu, halmashaur nzima unakuta una afisa misitu mmoja,Kwa upande wa elimu walipo wapo elfu Moja, so utakuta una maafisa elimu elfu Moja hpo Ndo shida Ilianza.
 
Back
Top Bottom