Waliotengeneza invoice kubwa siyo watumishi WA umma, NI kampuni iliyopewa dhamana yakutengeneza ndege ya mzigo. Kwanini tunawaogopa kusema ukweli?

Nijuavyo Mimi,tatizo lipo kwenye mkataba maana huenda kuna kipengele kinachoruhusu kuongezeka kwa bei bila mteja kupewa taarifa.Kama hicho kipengele kipo nadhani tatizo mnajua linaanzia wapi.Elimu yetu bado haijatusaidia kwani watu kujizima data na kujidai hawaoni vifungu kama hivyo ni kawaida sana ili wafanikishe mambo yao.

Hii yote imetokana na msingi tuliojengewa kupitia janja janja ya siasa kuanzia kwenye katiba.Inakupa haki kwa mkono huu,kisha inainyang'anya kwa mkono mwingine

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Rais mwenyewe amesema kuwa kuna watu wamemuambia haya mambo yameanzia huku ndani. Sasa huku ndani kuna watumishi wa babu yako na sio watumishi wa umma? Kama hauna hoja si lazima kujaza kurasa za JF na maandishi kanjanja kama haya.
 
Unaelewa kidogo sana....

Unaongelea invoice na delivery notes vitu vidogodogo sana hivyo...

Kwenye biashara kubwa kama hii, kitu cha kwanza kabisa kabla ya vitu vidogo dogo kama invoice, quatation au BOQ nk huwa kunaingiwa mkataba wa makubaliano (business legal contract/agreement)

Kwenye mkataba wa makubaliano ndiyo Kila kitu kimewekwa humo ikiwemo;

1. Bei ya bidhaa au huduma inayotolewa na mtoa huduma..

2. Muda wa mkataba...

3. Wajibu wa kila upande wa serikali ya TZ (mteja wa ndege) na kampuni iliyouza ndege..

4. Terms and conditions zingine zinazopaswa kuzingatiwa na Kila upande..

MASWALI YA KUJIBIWA NI HAYA na kamwe siyo issues za invoice wala delivery notes;

✓ Je, mkataba wa mauziano unademaje kuhusu bei..?

✓. Kuna kipengere kinachoruhusu validation ya bei..?

✓ Kama Kuna kipengere cha namna hiyo, Je ni ktk mazingira gani, na kwa kiwango gani? Na yalikuwepo kweli mazingira hayo? Na kwanini iwe ni kuongeza bei na sio kupunguza?

KWA HIYO:

Ishu hapa sio invoice au delivery note. Ishu siyo nani amelipa au hakulipa.

Ishu hapa ni mkataba wa mapatano ya mauziano ya ndege hiyo tangu awali unasemaje.

Na kama unasema tulipatana tuuziane ndege Kwa bilioni 47 ni kwanini malipo yamekuwa ni zaidi ya mapatano? Nani ka - inflate bei kinyume na mapatano?
 
Mpaka ije kuidhinishwa hapo inapita kwenye mikono mingi sana.
 
Ndio nimekuelewa sana tu variation haiwezi kuzidi 10% variation ya kwetu imeenda hadi 90% ni maajanu sana kwa kweli sijawahi kuyaona duniani
Hiyo variation ni zaidi ya 100% mkuu, yaani variation inazidi order ya ndege nyingine mpya kama hiyo.
 
Mbona kama tunazunguka wakati suala lipo wazi.

Utalipaje invoice kubwa, wewe kipofu? Mbumbu au?

Unafikiri pesa za serikali zinatoka kimchezo mchezo? Ina maana kama imetoka wameamua wengi kuna chain iliyohidhinisha kwa upande wa serikali, hamna cha kukwepa rais analijua
 
Ujue aliyetoa taarifa ya mabadiliko ya invoice ni Rais Samia. Tena akilalamika hadi akaita watu wapumbavu.
Watu / hadi wabunge ni kama hawamwelewi Rais na wanataka kumsaidia achukue hatua.
Kama Rais kafunga aseme bana tufahamu yupo kwenye mfungo
Alichosema yeye kataarifiwa kuna over-invoice. Na akaeleza ongezeko la bei ni inflation adjustments zilizopo kwenye mkataba.

Baada ya hapo akaanza kulalamika inakuwaje watu awapambani mpaka wanaruhusu ongezeko linakuwa kubwa ivyo au awasomi vizuri mikataba.

Ndio maana ‘communication skills’ ni muhimu, sikiliza mtu anachokusudia kusema; badala ya kukimbilia kuweka tafsiri zako na maana tofauti.

Hakuna mahala raisi aliposema hiyo invoice imetengenezwa Tanzania; alicholalamikia wamekubali vipi kirahisi na kuingia mikataba bila ya kusoma details vizuri.

Mwigulu kaenda mbali zaidi na kuelezea walichofanya wao kuhakikisha uhalali wa hayo malipo kupitia ofisi ya mwanasheria.

Baada ya kuambiwa na mwanasheria deni ni halali wakamtaarifu boss wao kuna budgetary expenses variance kwa sababu ya ongezeko la malipo kama taratibu za control procedures za matumizi zilivyo serikali. Ndipo Bi Tozo alipojua.

Swala lipo wazi kuna uzembe wa kuingia mikataba serikalini; lakini hakuna wizi wowote.
 
Mwigulu ameeleza inavyopasa kufanyika sio alivyofanya, angetekeleza ipasavyo CAG asingepata hojanya kuandika wala neno stupid lisingetikea, pamoja na wizara kuongozwa na doc
Hilo swala halipo kwenye report ya CAG ya mwaka huu speaker ameshaeleza.

Raisi alikuwa akilalamikia uzembe uliotokea hivi karibuni, na taarifa zake kazipata kutoka wizara ya fedha kabla awajalipa.

Embu tujenge tabia ya kusikiliza watu wanakusudia kusema nini, badala ya hizi tabia za ‘bias listening’ kukimbilia yale tunayotaka kusikia.
 
Waziri wa fedha na waziri anayehusika na uchukuzi wasingoje kufutwa kazi wajiondoe kwa kuwajibika kwa masilahi mapana ya TAIFA hapo hakuna kumumunya maneno.
 
Tukiongelea alichokisema mwigulu na alichokiuliza olesendeka , ripoti ya CAG inahusika kwenye malipo ya riba kwa uchelewasheji malipo, na wizara inayohusika na kuwajibishwa ni watendaji wa wizara, na report ya CAG sio hii tu mpina alikuwa anaongelea ripoti ya CAG na kushindwa kufanya kazi ipasavyo wizara ya fedha
 
Hayo ya Mpina ungeyaweka pembeni kwanza tujadili contexts za mada husika.

Back to the topic.

Let’s recap kilichotokea bungeni siku hiyo alianza ‘Ester Matiko’ kubwabwaja shutuma za invoice ya hiyo ndege ya mizigo kwa jinsi alivyotafsiri yeye na kumlaumu waziri wa fedha kumkwamisha raisi. Waziri akaomba mwongozo na kumwelezea control process za matumizi ya serikali kuu raisi lazima ajuzwe kwanza.

Baada ya kauli ya waziri, Olesendeka kwa kuamini kuna ufisadi kwenye invoice akataka waziri kutomuingiza raisi katika hilo genge.

Ndipo Mwigulu alipofafanua zaidi taratibu zao za matumizi huko juu serikalini.

Alichozungumza Mwigulu kwa watu wa finance ni uelewa wa kawaida achilia serikalini kwenye taasisi yeyote yenye control procedures makini monthly budgets ya matumizi lazima boss mkuu ajue na large budgetary expenses variation kabla ya kulipa lazima boss ajue hayo mabadiliko. If anything that’s a strong control system ya matumizi sio watu wajiamulie tu kama huko kwenye serikali za mitaa na taasisi za kibiashara ambapo watu wanapiga hela wakurugenzi hawajui.

Swala lenyewe uwezekano wa invoice kuongezeka ni hivi kwenye mkataba wa matengenezo kuna kuna kitu kinaitwa ‘transaction price’ (google kwa maelezo zaidi kama uelewi hiyo concept) hii inalipwa kila baada ya hatua za kazi. Na mara nyingi ‘transaction price’ sio fixed huwa ni ‘variable consideration’ (again google the concept for more details) kwa kifupi kuna sababu kadhaa invoice inaweza ongezeka, sababu ambazo raisi kazigusia material inflation price after covid.

Ni hivi sisemi hakuna uzembe kwenye kuingia mkataba ila ukisikiliza kinachosemwa na serikali ni wazi hilo deni ni halali shida ni uelewa tu. Kumalizia Boeing awawezi toa invoice halafu wakarikodi kitu tofauti kwenye ledgers those things are usually numbered and traceable hadi bank na external auditor.

Swala hapo ni kuajiri watu wenye skills sahihi serikalini ndio shida, watu wengi hawana uwezo na Phd zao za Magumashi ndio shida ilipo na kupelekea nchi kupigwa kirahisi hasa kwenye mikataba.
 
nmesoma mpaka uliposema tuweke pembeni , kwa kuwa hyo sentensi haina tija kwa taifa., haitapendeza kuendeleza mjadala na ww , kwa kuwa wa kuwajibishwa kutokana na report za CAG za. Mwaka uliopita na repoti ya mwaka ambayo haijawa public, waziri wa fedha naye inaswa awemo
 
Mbona unajichanganya ktk maelezo yako?hapo kinachogomba ni mikataba/mkata ulioingiwa pande zote mbili,kwa maana nyingine invoice/madai yalikuwa ni makubwa tofauti kubwa sana na mkataba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…