Elections 2010 Waliotoka mjengoni ni hawa tu?

Hivi hamuoni kwamba hii itakuwa ngumu kwa upinzani sasa?
Naona CCM wametumia ujanja ili waondoe makapi yaliyokuwa hayapendwi na wananchi ..ili uchaguzi utakapofika wote watakaoshindania Kinyang'anyilo ni wale waliochaguliwa na wananchi wenyewe??

La sivyo kungekuwa na hatari huo msululu woooote uliotoka ungechukuliwa na wapinzani kama bado ungekuwa kwenye kinyang'anyilo.
 
Kama Jimbo lina wapiga kura 40,000 na wanachama wa CCM waliopiga kura ni 10,000 tu then kuna watu kama 30,000 ivi ambao ni wananchi wenye uwezo wa kupiga kura..kwa hiyo mi sioni sababu yoyote ile ya upinzani kushindwa kuwawawishi hao walio baki. cha muhimu ni upinzani kusimamisha mtu anekubalika tu wawe makini katika hili!!
 
waweza shangaa NEC(hahaaaa shingo) wakawarusha mjengoni baadhi yao kwani wao ndio wenye kisu
 
Hao walio toka ndio mafisadi wenyewe au ndi magumashi tu. maana tulitaka mafisadi wooote wasirudi mjengoni,, sisi kwetu fisadi tumemtoaa
 
Omari Babati Mjini???

Ila Bado siunajua tena Mzee wa fadhila!! anaweza kuwarudisha wengi mjengoni akidhani anatoafadhila kumbe! anawapa upinzani Majimbo?
 
Omari Babati Mjini???

Ila Bado siunajua tena Mzee wa fadhila!! anaweza kuwarudisha wengi mjengoni akidhani anatoafadhila kumbe! anawapa upinzani Majimbo?
Mwalimu wangu Omar Kwaang' kaangushwa na Kisyeri Werema Chambiri yule jamaa aliyesababisha CCM ikang'olewa Tarime hadi kesho!
 
Hawa nao vipi?

Abdulkarim Shah (Mafia).

Mkuu huyu muheshimiwa alitangazwa mshindi lakini Mpinzani wake mkuu alikata rufaa kwani Kituo kimoja kinasemekana aliweka MAMLUKI wengi sana. Hivyo rufaa itasikilizwa Alhamisi.
 
63. Lotto (Morogoro Mashariki)
64. Malima Lubeleje (Mpwapwa)
65. Prof. Mwalyosi (Ludewa)
 
Mbona hii thread inakufa hivi hivi?au wadau hamna interest na analysis ya hii kitu?
 
Mwalimu wangu Omar Kwaang' kaangushwa na Kisyeri Werema Chambiri yule jamaa aliyesababisha CCM ikang'olewa Tarime hadi kesho!
Imekuwaje Kisyeri Chambiri akagombea tena Babati huku maskani yake yakiwa Tarime? Huyu jamaa namkumbuka sana wakati akiwa mwanafunzi wa engineering huko Lagos nadhani mwaka 1974 alipata ajali ya basi akiwa njiani na baba yake Mzee Werema Chambiri aliyekuwa akimsindikiza Nairobi kukamata ndege ya kwenda Lagos. Mzee Chambiri alifariki katika ajali ile naye Kisery alipata majeraha sana ila sina uhakika kama aliendelea na safari au aliahirisha. Watu wengi pale Tarime walilia sana kwa vile Mzee Chambiri alikuwa mtu mzuri sana, alikuwa anasidia watu wengi sana hasa waliokuwa na matatizo ya madeni ya namna moja au nyingine.
 
Mbona hii thread inakufa hivi hivi?au wadau hamna interest na analysis ya hii kitu?

wacha wafu wazike wafu wao, tunaingiza CHADEMA ikulu na wabunge 200. CCM walikufa na sasa wanafanya maigizo. Huwezi kupitia kozi ya rushwa halafu ukahubiri utakatifu.
 

Kichunguu;

Mzee Chambiri aliposhindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2005 kule TARIME basi yeye akawa kiguu na njia kuhamia Babati;inawezekana alifanya uchunguzi na kugundua kuwa Mbunge Omary Kwaang ni mbunge rahisi kumshinda,na kweli juzi kamuangusha kwenye kura za maoni kwa kura nyingi tu!

ONYO;Babati wajiandae kwa mgogoro mkubwa wa uongozi ndani ya CCM maana uzoefu unaonyesha kuwa Mzee Chambiri ni bingwa wa kutengeneza makundi na ndicho hasa kilichomtoa TARIME baada ya kundi lake kuzidiwa nguvu na kundi la mfanyabiashara Gachuma.

CHADEMA hili linaweza likawa jimbo rahisi kabisa kulichukua,Mzee Chambiri ni rahisi sana kumshambulia jukwaani kwa madudu yake toka alipokuwa Mbunge wa jimbo kule mkoa wa Mara!Kwa nini hakubaliki jimbo alilokulia hadi kuzeekea la Tarime na sasa akubalike kwenye jimbo jipya wa Babati?
 
Kwa wachambuzi wa siasa inaashiria nini hii?
Utafiti wa Redet ulishasema kila kitu, najisikitikia mimi ni mmoja wa walioubeza utafiti ule.
Nadhani Redet wataibuka na utafiti mwingine hivi karibuni ili kuendelea kumpandisha JK dhidi ya tufani ya Dr.Slaa.
Thw wind of change is sweeping accross Tanzania, wana CCM wameanza, wananchi watamalizia.
 
Hawa vijana wa Mzee Werema Chambiri( Kisyeri na Enock) wamekua wakakuta jina zuri sana la baba yao kwenye siasa za Tarime. Mwanzoni walilitumia vizuri tu. Wakaanza kulewa sifa na umaarufu. Wakaanza kuonyesha dharau kwa watu wa Tarime. Wamejikuta wanachukiwa kwelikweli. Ile "political dynasty" alooianzisha baba yao wameibomoa kisawasawa. Bado ni wafanyabiashara wazuri tu. Wanapata tenda nyingi kubwa tu kwenye Halmashauri na serikali kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…