OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Habari ni kama mlivyozisikia,Simba SC tumeingia robo fainali na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania. Tumepitia katika wakati mgumu sana,dhihaka,dharau na kebehi kwa kipindi chote cha mapambano.
Asanteni sana mliotubeza kwani mlitupa changamoto. Tunawasamehe tunawataka msijisikie vibaya,tufurahi wote kama nchi. Mashabiki wa Yanga baadhi tunawasemehe, Shaffi Dauda ulikiuka ethics za mchambuzi ukitubeza,tunakusamehe. Mwinyi Zahera uliyeacha nyumba yako ikiteketea kwa moto ukaenda kuzima moto wa jirani,na wengine tunawasamehe.
WanaJF wooooote kina Sibonike demigod Nifah Shadeeya Joseverest gungele kisiki kibichi astrologist hazard cfc nk tunasema msijisikie vibaya,ushindi ni wenu pia. Furahini pamoja na kina sembo MTAZAMO Shunie Viol Ghazwat Louis II nk
Shukrani ziwaendee makamanda wetu wote kikosi kizima. Clautus Chota Chama umekuwa unatuokoa dakika mbaya kwa hatua zote,umefanya hivyo dhidi ya Nkana FC,umefanya jana pia.
Shukrani zimwendee Mwalimu Patrick Aussems, Denis Kitambi, Boss Mo Dewji na Board of Directors yote, mashabiki wa Simba kwa hamasa ya maana kokote duniani.
Shukrani za kipekee kwa De La Boss Haji Sunday Manala,umekuwa nguzo muhimu kwetu nje ya pitch. Asante sana
This iz Simbaaaaaaaaaaaaaaaaaaa