Waliotunga na kupitisha vitabu hivi kwa ajili ya watoto wetu wachukuliwe hatua gani?

Waliotunga na kupitisha vitabu hivi kwa ajili ya watoto wetu wachukuliwe hatua gani?

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,204
Reaction score
3,277
Ukijiuliza kuwa hii nchi ina Serilkali (CCM), lakini bado kuna vitabu vinatungwa na kupitishwa kwa ajili ya kufundishia watoto wetu mashuleni. Mfano kuna "kitabu kimeandikwa namba yoyote ukigawa kwa sifuri ni sawa na sifuri", yaani 2/0=0, lakini jibu sahihi ni kwamba hakuna namba inayogawika kwa sifuri. Kuna vitabu kadhaa vimekosea mwaka wa vita vya majimaji.Pia kuna vitabu vimeandika kuwa reli ya TAZARA imejengwa mwaka 1993, wakati reli hii ilijengwa kati ya mwaka 1970 hadi 1975.
Sasa najiuliza, Tanzania tunakwenda wapi? walioandika na kupitisha vitabu hivi wachukuliwe hatua gani?

Kuna siku niliandika kuwa Tanzania ni kama gari la mkaa, maana gari la mkaa mara nyingi utakuta breki au taa hazifanyi kazi. Hivyo ni rahisi kuacha njia.

Hivi serikali ya CCM mnatupeleka wapi?:rockon:
 
umenikumbusha biology hepatic vein is the vein which pours blood from the liver to the stomach. nikajiuliza mara 3 hivi kuna vein inayomwaga damu toka kwenye ini kuja tumboni?? ama kwa muandishi na mhariri neno connect na neno pour ni synonymous??

kimsingi vitabu vya kiada vilivyotungwa na kuchapwa na nyamabari nyangwine vinafunza uongo watoto.
 
Taja majina ya vitabu husika, mwandishi, na publisher....acha porojo
 
Ngoja aje mtu siku moja asimulie kuwa Vita Vya Kagera vilikuwa kati ya Rwanda na Burundi...
 
Serikali ya China ingeshawanyonga watu hawa!
 
Ni upepo tu wa kielimu utapita!
 
Baraza la Mitihani katika muongozo wake wa kuonyesha makosa ya watahiniwa, limesahihisha jibu la swali linalouliza matatizo ya serikali kutoa huduma za afya Tanzania kwa kuandika "Tanzania is spacily populated".

Hilo ndilo baraza la freaking mitihani. Chochote kinawezekana bongo.
 
Taja waharibifu wa elimu ya bongo wanaoandika porojo km NYAMBARI NYANGWINE na maboya wengine

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Si kila kitabu kilichoko sokoni kimepitishwa kaka. Walimu wengi na hata wadau mbalimbali wa elimu hawalijui hili jambo. Ndo maana mleta hoja anatakiwa ataje title, author na publisher ili tujiridhishe kama kimepitishwa.
 
mharibifu mwingine anaitwa adamson educational publishers.
 
Nyambari Nyangwine ana mkono wake hapo

Nashukuru Mungu sana nilikuwa mmoja wa wanafunzi waliokataa kuvikubali vitabu vya Nyangwine.Havimfundishi mwanafunzi kuelewa bali vimekaa kujibu mtihani tu.Waandishi wa Nyangwine wengi wao wanaandika kwa mtindo wa kudonoa ili mwanafunzi apate kujibu mtihani.Na wala vitabu vyake si vitabu bali ni mkusanyiko wa materials tu ili kumrahisishia mwanafunzi kujibu mtihani.Mimi kamwe hawezi kunishawishi mwanafunzi nimnunulie kitabu et kimeandikwa na waandishi wa Nyangwine kama kina Msabila na Kinunda James.Na kwa mantiki hii pia kuna wanafunzi ambao wanamaliza kidato cha nne hawajawahi kusoma kitabu kama Things Fall Apart.Wao wanategemea uchambuzi uliofanywa na kina Kinunda tu.Hii ni hatari sana.Na hapa ndipo unaona hata huku vyuoni watu wanategemea notes za mhadhiri zaidi kuliko kutaka kusoma kitabu.

Mimi nilikisoma kitabu hicho tena version kubwa si ile simplified kabala hata hatujaanza kusoma rasmi darasani na bado naweza kukusimulia matukio mazima ndani ya kitabu hicho. Mimi binafsi sikushangazwa na kufeli kwa wanafunzi na wala sitoshtuka kamwe kwani hayo ni matokeo halali kabisa.
Labda ninachoweza kukubaliana na malalmiko ya wadau wengine ni kile kilichoonekana kuwa kuna wanafunzi hawakufanya baadhi ya masomo lakini wameonekana wamefaulu.Hapo tatizo sasa lipo NECTA.

Pia kuna wadau wanasema mtihani ulikuwa mgumu sana.Hii si hoja.Mlitaka mtihani uwe laini ili kiwe nini sasa?Kwanza hakuna mtihani mgumu wala mrahisi.Kama watu wanataka mtihani rahisi ili matokeo yaonekane ni mazuri ili wajipongeze basi hakuna haja ya kufanya mtihani huo.Maana hii ni sawa na mwanafunzi anayefanya maswali ya hesabu yale yale anayoyajua halafu anajipongeza.Mwalimu wangu mmoja alipata kusema mtindo kama huo ni kudumaza akili.Unakuwa huna maarifa mapya.

Kuhusu vitabu anavyo vilalamikia James Mbatia ni sahihi.Vipo kabisa vinataka kupotosha wanafunzi.Hivi hesabu zimebadilika lini kuwa namba yoyote ikigawiwa kwa sifuri jibu ni sifuri?Wizara ipo na taasisi ya elimu ipo lakini hawafuatilii sula la hili. Kisa hoja ya kisiasa kasema Mbatia.Tunaendekeza siasa hata kwenye mambo ya msingi.Jana kwenye kipindi cha kipima joto cha ITV alionesha ushahidi wa kitabu kinachosema any number divided by zero is zero page 46.Wahusika hapa wako wapi jamani?

Leo hii ukikutana na mwanafunzi aliyemaliza chuo kikuu ukimwambia aandike hata barua ya kuomba msaada wa kupata sponsor ya masters hawezi.Atakuambia niandikie mimi nitakopi.Hii maana yake nini? Huyu alikuwa na msingi mbovu huko nyuma.Mchezo wa mwanafunzi kukariri maswali umetamalaki hata vyuo vikuu.Si ajabu pia ukakuta mhitimu anashindwa kusoma makala ndefu kwenye gazeti.Siku moja rafiki yangu alinishangaza kwa kauli hii kuwa yeye akisoma gazeti kama Raia Mwema makala ndefu anapofika mwishoni hakumbuki nyuma amesoma nini.Yaani anashindwa kukumbuka alichokwisha soma paragraphy ya kwanza na ya pili.Haya ni matokeo ya twisheni mashuleni.

Jamii nzima inahitaji mabadiliko.
 
KAMA TUNAADHIMISHA CKUKU YA UHURU waTANZANIA, IWEJE HLO LA VTABU. du cku 1 nlikuwa tempo shule fulan, akaja madam kufanya tp, akaingia form 1 kufundisha historia ya lugha, secod master akamuulza kwan we syllabus yako inaelezaje? akasema haijui sylbs
 
Back
Top Bottom