Nyambari Nyangwine ana mkono wake hapo
Nashukuru Mungu sana nilikuwa mmoja wa wanafunzi waliokataa kuvikubali vitabu vya Nyangwine.Havimfundishi mwanafunzi kuelewa bali vimekaa kujibu mtihani tu.Waandishi wa Nyangwine wengi wao wanaandika kwa mtindo wa kudonoa ili mwanafunzi apate kujibu mtihani.Na wala vitabu vyake si vitabu bali ni mkusanyiko wa materials tu ili kumrahisishia mwanafunzi kujibu mtihani.Mimi kamwe hawezi kunishawishi mwanafunzi nimnunulie kitabu et kimeandikwa na waandishi wa Nyangwine kama kina Msabila na Kinunda James.Na kwa mantiki hii pia kuna wanafunzi ambao wanamaliza kidato cha nne hawajawahi kusoma kitabu kama Things Fall Apart.Wao wanategemea uchambuzi uliofanywa na kina Kinunda tu.Hii ni hatari sana.Na hapa ndipo unaona hata huku vyuoni watu wanategemea notes za mhadhiri zaidi kuliko kutaka kusoma kitabu.
Mimi nilikisoma kitabu hicho tena version kubwa si ile simplified kabala hata hatujaanza kusoma rasmi darasani na bado naweza kukusimulia matukio mazima ndani ya kitabu hicho. Mimi binafsi sikushangazwa na kufeli kwa wanafunzi na wala sitoshtuka kamwe kwani hayo ni matokeo halali kabisa.
Labda ninachoweza kukubaliana na malalmiko ya wadau wengine ni kile kilichoonekana kuwa kuna wanafunzi hawakufanya baadhi ya masomo lakini wameonekana wamefaulu.Hapo tatizo sasa lipo NECTA.
Pia kuna wadau wanasema mtihani ulikuwa mgumu sana.Hii si hoja.Mlitaka mtihani uwe laini ili kiwe nini sasa?Kwanza hakuna mtihani mgumu wala mrahisi.Kama watu wanataka mtihani rahisi ili matokeo yaonekane ni mazuri ili wajipongeze basi hakuna haja ya kufanya mtihani huo.Maana hii ni sawa na mwanafunzi anayefanya maswali ya hesabu yale yale anayoyajua halafu anajipongeza.Mwalimu wangu mmoja alipata kusema mtindo kama huo ni kudumaza akili.Unakuwa huna maarifa mapya.
Kuhusu vitabu anavyo vilalamikia James Mbatia ni sahihi.Vipo kabisa vinataka kupotosha wanafunzi.
Hivi hesabu zimebadilika lini kuwa namba yoyote ikigawiwa kwa sifuri jibu ni sifuri?Wizara ipo na taasisi ya elimu ipo lakini hawafuatilii sula la hili. Kisa hoja ya kisiasa kasema Mbatia.Tunaendekeza siasa hata kwenye mambo ya msingi.Jana kwenye kipindi cha kipima joto cha ITV alionesha ushahidi wa kitabu kinachosema any number divided by zero is zero page 46.Wahusika hapa wako wapi jamani?
Leo hii ukikutana na mwanafunzi aliyemaliza chuo kikuu ukimwambia aandike hata barua ya kuomba msaada wa kupata sponsor ya masters hawezi.Atakuambia niandikie mimi nitakopi.Hii maana yake nini? Huyu alikuwa na msingi mbovu huko nyuma.Mchezo wa mwanafunzi kukariri maswali umetamalaki hata vyuo vikuu.Si ajabu pia ukakuta mhitimu anashindwa kusoma makala ndefu kwenye gazeti.Siku moja rafiki yangu alinishangaza kwa kauli hii kuwa yeye akisoma gazeti kama Raia Mwema makala ndefu anapofika mwishoni hakumbuki nyuma amesoma nini.Yaani anashindwa kukumbuka alichokwisha soma paragraphy ya kwanza na ya pili.Haya ni matokeo ya twisheni mashuleni.
Jamii nzima inahitaji mabadiliko.