Waliowahi kuchukua mkopo kwenye taasisi yoyote na kufanikiwa kukuza biashara bila tatizo tushirikishane

Waliowahi kuchukua mkopo kwenye taasisi yoyote na kufanikiwa kukuza biashara bila tatizo tushirikishane

Fernando Wolle

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
387
Reaction score
770
Binafsi niliwahi kuchukua mkopo wa milioni 5 kwenye bank moja hivi. Marejesho nakumbuka yalikuwa 516,666TZS kila mwezi kwa miezi 12.

Hakukuwa na manufaa sana ila tu mkopo ulisaidia kuinusuru biashara ambayo ilikuwa inayumba. Wakati nachukua mkopo tayari nilikuwa na biashara ambayo kwa mwezi ilikuwa inaingiza faida ya 350,000 kwa mwezi.

Nilipochukua mkopo faida ilipanda mpaka 600,000 kwa mwezi. Lakini kumbuka kuna rejesho. Marejesho hayakusumbua sana lakini baada ya kumaliza mkopo biashara ilirudi kule kule tu faida ya 350,000. Kwahiyo sikuona faida ya mkopo zaidi yankupata stress na roho kuniuma tu yani biashara nilikuwa nawafanyia Bank.

Tushirikishane namna bora ya kunufaika na mkopo wa biashara.
 
Kukopa ni jambo jema kama unakopa kwa lengo la kuongeza faida kwenye biashara yako na kweli umeona huo uhitaji na hesabu inakupa majibu kuwa unahitaji kiwango fulani ili uweze kutengeneza faida zaidi.
Usikope tu kwakuwa unakopesheka na wakati biashara yako haihitaji ongezeko la mtaji, mwisho pesa iliyo kopwa haiendi kwenye jukumu lililokusudiwa.
Pia tujue wakati sahihi wa kukopa kulingana na nature ya biashara unayo ifanya,
Wengi hawapeleki pesa iliyo kopwa kwenye biashara iliyo ombewa mkopo.
 
Back
Top Bottom