Waliowahi kutolewa majini/Mashetwani

Hilo siyo jini,Kuna ugonjwa niliosoma,dalili zake ni hizo kasoro ndoto
 
Mtu wangu wa karibu ana hali hii.
 
we huna mapepo ni stress tu ya maisha.
 
Pata dosage ya kitimoto, kutwa mara tatu, uone kama hayo mambo yataendelea.
 
Tatizo linaanza majini ni ugonjwa wakili...Baadala ya kupelekwa hospitali unapelekwa kwa waganga...Ubovu hata hospitali unakuta madaktari wasomi kabisa bado wanaamini hizo primitive concepts
 
Naomba kuuliza...hivi wachungaji ambao wako bara la amerika ya kaskazini na ulaya nao waumini wao wanapandisha na kutolewa mapepo na majini kama huku kwetu afrika??
 
 
Yeah hizo ni miongoni mwa dalili kuwa una shaytwaan ndani ya mwili wako na anahitaji kutolewa kwa visomo vya Ruqya (Quran na Dua alizofundisha Mtume Muhammad ) na dawa za kisunnah.

Hivi vitu kwa mtu ambaye havijamkumba anaweza kusema ni uongo ila vipo. Mashaytwaan huwakumba matajiri na masikini. Mimi nlikuwa muhanga wa haya mambo , dalili ulizozitaja ndio nlikuwa nazo ,moja wapo ni hizo extreem anxiety ( wasiwasi uliopitiliza) yaani moyo unaenda race huku nikiwa na wasiwasi mithili ya muhalifu anayetafutwa na polisi. Ukosefu wa usingizi usiku, hasira na ghadhabu zilizopitiliza, isolation ,kichwa kuuma n.k ila nilipata mwalimu akanisomea na kulitoa hilo shaytwaan lililokuwa linanisumbua
 
Hv majini yanawaogopea nn matajiri na kuwaonea masikini tu. Sijawahi sikia hizo swaga za majini kwa matajiri Wala nn
Sasa tajiri utamjuaje kama ana hayo makitu? Nani atakuambia? Mtakutana wapi.akueleze kuwa ananyo?
 
I agree. It must be hell. Anyone with anger is possessed too.
 

Wewe mwenyewe ndio wa kuamua kupona au kubaki na hali yako

LUKA 11: 24-26
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.

2 PETRO 2: 20-22
Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…