Katika maisha yangu sijawahi kuona mtu amepona na kutolewa majini akiwa fresha and comfortable na kupona kabisa na majini yasirudi tena.
Nimeona tu Kuna Namna nyingi za kutoa majini na Mashetwani.. mosi ni kwa maombi ya wachungaji au manabii wa makanisa nimeona kwenye TV wakiwashika watu na watu wakipagawa na mapepo kuikubali yanaondoka.
Pili ni kwa Tiba za kiasili lakini yote kwa yote sijawahi kukutana na mtu aliepona kabisa matatizo haya ya Mashetwani. Sasa basi Kama Kuna mtu alishawahi kupitia hili naomba uzoefu wake.
Maana nahisi Kuna kila dalili kwenye huu mwili wangu Kuna mpangaji mpya na halipi Kodi ananiburuza vibaya nahitaji nijue Kama naweza kumuonyesha mlango wa kutokea? Na Kama mna mapendekezo ya watabibu wa haya mambo nipeni link na connection zao.
Asanteni!
Wewe mwenyewe ndio wa kuamua kupona au kubaki na hali yako
LUKA 11: 24-26
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.
2 PETRO 2: 20-22
Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.