Waliozaliwa 1984 tukutane hapa tuzungumze...

Waliozaliwa 1984 tukutane hapa tuzungumze...

Nimemenunua BMW X5, X3 na X1 za kuendea shambani, nimejenga ghorofa 10 Dar, Nairobi, Paris na US, Nimenunua shamba dogo lenye ukubwa wa ekari elfu hamsini Texas Marekani na kijishamba cha ekari elfu ishirini Morogoro.

Kwakifupi bado najitafuta, wewe je?
Hiyo stimu acha mkuu.
 
Mlichelewa sana kuguna guna...tulianza guna guna tukiwa na umri wa miaka 25....na mpaka sasa guna lipo
 
Haya maisha ukiyafikiria sana utakata tamaa. Kimsingi kama unamudu basic needs furahia tu maisha kwasababu sisi wote lazima tufe. Kitu kikubwa nadhani kwa binadamu ni kama ukijaliwa kupata ndoa na watoto. Kuhusu pesa wala usijali. Unaweza ukazipata na zikapotea vilevile.

Mimi nakimbilia 39 na nilichojifunza ni kuwa sisi binadamu hatuna ujanja wowote kujua kesho zetu. Unaweza ukasoma sana ukadunda. Unaweza ukafanya sana biashara ila matokeo yasiwe mazuri. Kama uko na afya njema na hauko jela mshukuru Mungu na furahia kila dakika yako kwenye haya maisha. Waliosoma Moshi Tech form IV ya 2002 mtamkumbuka dogo moja wa Chuga alikuwa na akili za kutisha ila leo mambo yameenda kinyume na matarajio. Kuna Patrick Sosopi alikuwa dogo ambaye hakuwa na uwezo mkubwa darasani ila leo ni miongoni mwa watu wazito kwenye genge la Mbowe.
 
Karibuni mliofika 40 mshukuruni sana Mungu kwa neema alizokupa hakuna mtaji mkubwa kama Mungu akikupa afya njema...Stev Jobs alikiri hili akiwa kitandani..
 
They say 'life begins at forty!'

Sasa kama wewe umeshafikisha miaka 40 au umebakiza siku au miezi kadhaa, hebu tujuzane ni nini umejifunza? Ni mangapi umefanikisha? Changamoto ni zipi za kusaidia wengine kupambana zaidi?

Karibuni sana legend.
Bibi shkamoo
 
Back
Top Bottom