Hakika sikio la kufa halisikii dawa. Wabunge wakishirikiana na mawaziri, machawa na wapambe e.g. baadhi ya waandishi walituaminisha pitisha hiyo sheria ya kubinafsisha bandari zetu kwa DP world.
Tuliaminishwa, ulimwengu unaenda kasi lazima tuende na wakati, tuende na utandawazi, pitisha hiyo sheria ya kubinafsisha bandari zote baharini na nchi kavu na misitu yetu mikubwa kwa DP world, mwanzo ilikuwa kwa miaka 100, baada ya kilio ikashushwa kwa miaka kama 30, miaka ambayo karibu viongozi na wabunge wote waliopitisha hii sheria watakuwa wamekwisha kufia mbali na kuwaachia vizazi vyetu umasikini wa kutupwa chini ya utumwa mamboleo kwenye rasilimali zao.
"Sikieni nyie watanzania msiotaka maendeleo, hawa DP world wanauzoefu wa kuendesha mabandari makubwa kimataifa; India na Marekani (just to mention a few). Hawa jamaa sio tu tukiwapatia bandari watapunguza siku za mzigo kukaa bandarini mwezi mzima bali itakuwa wiki moja au mbili na ghalama za kuingiza mzigo zitashushwa zaidi ya nusu ya gharama za sasa"
"Watakuja na vifaa state of arts, watacomputerize process nzima za kutoa mzigo kuongeza quality na tija. Nchi itapata mapato matrililioni (ile figure siwezi kuiweka hapa kwani ni kituko) , mapato ya mwaka yatakuwa zaidi ya jumla ya mapato ya miaka kumi iliyopita" NDIVYO WATANZANIA TULIVYOHAMINISHWA NA WAWAKILISHI WETU BUNGENI, wakipewa support na machawa na wapambe waandishi waliolipwa rushwa ya kupelekwa DubaI few days kwenye five stars Hotel na kulipwa mamilioni na magari ya kifahari juu. Hivi wanajisikiaje sasa wakiona wotetunasuffer; Ila wabongo bwana hatuna aibu, tunajua kumute, macho makavuuuu, ndindindi! as if nothing happened.
Sasa tunaambiwa tukae mkao wa kula, kwa kupanda kwa gharama ya kwa asilimia 360% kuingiza na kutoa mzigo bandarini; haijawahi kutokea tangia bandari zetu zianze kufanya kazi, tutegemee mfumuko wa bei ya vifaa vyote tunavyotumia (vipuli na vifaa vya magari, magari yenyewe, ujenzi, kilimo, umwagiliaji, mafuta n.k) kwani hata hivyo vinavyotengenezwa nchini mali ghafi inatoka nje, tutegemee mfumuko wa bei ya vyakula na mafuta, tutegemee ghalama zote za maisha kupanda. Kibaya zaidi serikali itakosa mapato makubwa, sitakiwi kuweka takwimu hapa na contribution ya bandari zetu kwenye budget nzima ya nchi; Kwishnei! Nakwambia kama wangekuwa na tija tayari leo tungeambiwa mapato yalivyoongezeka, huduma ilivyoboreshwa, Jiulize kwa nini kimya kikali sana.?
Tunaambiwa copper ya Congo iliyokuwa ikipitishwa hapa kwetu, sasa inapitia bandari ya Mombasa, Wafanyabiashara wa nchi zote jirani na wa ndani wamehama/watahamia bandari ya Mombasa. Hivi jiulize yale malori lukuki ya Mizigo kutoka na kwenda Uganda, Burundi, Kongo, Malawi, Rwanda , Zambia, Malori uliyokuwa ukipishana nayo wakati wote yameunga tela kutokea Dodoma mpaka Dar es salaam to and fro yamepotelea wapi?. what is the implication of that? Ni kiasi gani cha mabillioni walikuwa wakilipa kwa mwezi na sasa yanapotea. Hakika huhitaji akili ya PhD ya uchumi kujua kitakachotokea kesho kwenye maisha ya watu wa kawaida.
Rushwa ni mbaya sana, kwani mpokea rushwa hajali madhara yatakayotokea kwa wenzake na kizazi kijacho, yeye anaangalia masilahi yake na familia yake kwa wakati huo, ndio umesikia. Ni kweli hakuna ubishi kuna watu wamekuwa mabilionea kupitia ishu hii ya DP world. Ila wapambe koko, wengine utawasikia hata humu jamii forum kupitia comments zao huku hata wao ni njaa kali na shida kwelikweli ila bado wanatetea dhuluma hii ya rasilimali yetu, wanatetea ubakaji na utekaji wa mali ya umma tuliyokuwa tunamiliki tangia uhuru na kujipangia kulingana na kipato chetu
Na hii unaambiwa ni bado, hizi ni mvua za rasharasha, cha mtoto (this is just a pre-amble) labda tuvunje mkataba, mkataba ambao hatuwezi hata thubutu.
Nafikiri bado hatujasahahu vifungu toa damu, vifungu kata roho walivyotuwekea ili tusithubutu hata kufikiria kuvunja huu mkataba, achana na independent tribunal ya nje itakayotakiwa kibaya eti lazima wao kwanza wakubali na kulidhia ndipo waturuhusu kuvunja mkataba. Ebu msomaji fikiria eti ili uvunje mkataba unaambiwa itabidi huyo anayefaidi akubali kwanza. Hivi wasomi wetu, wanasheria, viongozi wetu kuna wakati mnakuwa na mapepo wakati mnasign mikataba hii, au akili zenu zinakuwa zimehamishwa seheme nyingine na kubaki vichwa tupu, eti inabidi adui, dhulumati , anayefaidi alidhie kwanza ndipo kukuruhusu uanze mchakato wa kuchukua kile anachofaidi,ili umnyang'anye tonge nono mdomoni. Hivi kwa akili ya kawaida inawezekana kweli. Hata Malaika hawezi kufanya upuuzi huo.
Ngoja sasa msumari wa moto uingie vizuri, sisi wabongo tunajifanyaga wajuaji sana, hatujifunzi hata kwa wenzetu Malysia waliovunja mkataba na hawa DP-world, kizuri wao hawakuwa na masharti magumu sisi vipofu tukajifanya wajanja kama kawaida yetuna kukubali masharti kata roho, masharti vujisha damu. Sasa tusubili kuendelea kubleed till we are dried -up. Na hili liwe somo kwa watunga sheria wetu, sio kila ukipewa kadola, ukipelekwa Dubai for 5 days night in 5 starts hotel unasahau ndugu zako, wazazi wako, wajukuu zako, kizazi chako, mbaya zaidi hata wale waliokuweka hapo.