Walisema DP World itashusha gharama na siku za mizigo kukaa Bandarini. Leo gharama za kuingiza mzigo zitapanda kwa 360%

LEO WAKO WAPI WALIOLOPOKA
MBONA SIWASIKII.
Mtujuze leo wanaongeleaje hili swala? au ndio kama kawaida vichwa vyao havitunzi kumbukumbu ya vinywa vyao.
 
Hizo ni kiasi kikubwa zinaendana na local imports. Transit imports ambayo ni kubwa mno ndiyo mtoa mada anasema wamehama bandari yetu. Je huko wanakoenda maharamia wako excluded?
 
LEO WAKO WAPI WALIOLOPOKA
MBONA SIWASIKII.
Mtujuze leo wanaongeleaje hili swala? au ndio kama kawaida vichwa vyao havitunzi kumbukumbu ya vinywa vyao.
Tatizo akili za wajinga wengi zimehodhiwa na ccm,suala nyeti kama hili wakaingiza udini kweli tumepatikana MUNGU tu ndiye atatuepusha na hatari iliyo mbele huko.
 
Naona vizuri watu tukijadiliana kwa hoja na nimependa kwa maandiko mazuri. Mimi siwezi kusema direct kama kuna DP wamechangia pia sababu sina data breakdown hizo cost pia zimechangiwa na kuongeza charges port au ni shipping lines tu wakija na breakdown ndio tunaweza kujua shida ipo wapi. Lakini kuhusu Mombasa kuwa watu wanakimbilia kule hili limeanza kabla hata ya DP kuja Tz ni miaka na miaka tunasikia hayo na hatujawahi kujuwa sababu ni nini, sasa kusema kwenda Mombasa ni sababu DP inakuwa sio haki.

Ila ni muhimi kwa hawa wakala wa shipping waweke wazi hizo gharama zimetoka wapi? je hakuna regulators nchi hii? mbona mengine tunayaweza. Unajuwa meli zikiwa kubwa zinaleta mizigo gharama zinakuwa chini kidogo shida huku kwetu vimeli vidogo vinakuja. Nakubaliana na wewe kabla hatujaanza kunyosheana vidole tupate breakdown wapi gharama zimezidi sababu ni wapi.
 
Hapana mimi sababu sijaona wakala statement sababu zao za kuhamia Mombasa nashindwa kuongelea. Lakini kama una statement yoyote ya wakala kuhusu hilo please tuwekee hapa ili tunufaike na kujuwa ukweli na tukijuwa ni DP basi tutalisemea hili kwa nguvu. Hoja ya kuhamia Mombasa kabla ya DP wanasema Mombasa ni rahisi haijaanza leo. Ila unakubali dunia nzima shipping imepanda mpaka 50%.
 
Mm ntakua wa mwisho kukubari, mpaka ntakapoona rasmi waraka kutoka kwao, wenye ufafanusi wa bei mpya za kuagiza mizigo.
 
Global supply chains are no longer tight and goods consumption today is rising only moderately. Shipping costs have increased by more than 150% since December 2023 as a result of disruptions to maritime traffic in the Red Sea.
 
Jibu zuri mkuu, una hoja, swali sasa

Je kama gharama zimepanda kote, kwanini, watu wakimbilie mombasa na hali jambo hili la kidunia?
Hili suala la Mombasa versus Dar halijaanza leo tumeambiwa Mombasa cheap kuliko Tz kwa miaka mingi tu kabla ya DP. Lakini nakubaliana na wewe kunahitajika cost breakdown. Mombasa inaweza kuwa cheap lakini kwa % ngapi? kama kabla ya rate mpya tuseme Mombasa ilikuwa cheap kwa 5% kwa mfano tu je leo ni same gap au tunaongelea 360% wanayosema watu humu. naweka habari za Kenya hapa kuonyesha wali walitoa angalizo bei zinapanda.

Kenya Ships Agents Association (KSAA) on Wednesday said importers should expect higher charges from this week as stakeholders assess the increasing insecurity from Yemen Houthis’ claim of fresh Red Sea attacks on British and American ships.

KSAA Chief Executive Officer Juma Ali Tellah said shippers are concerned about the escalating conflict along the Red Sea route, and its potential repercussions on the business community and consumers in East Africa.

The worry was always expected to bring a new burden. But the actual cost increment wasn’t known since December when Houthis first fired the first missile.
 
Msoma matokeo 2025.

Idadi ya wapiga kura M35.
Waliopo mjini M15.
Waliopo vijijini, umasaini, porini kusipo na internet wala duka la kijiji wala bandari 20M.
Du, umemaliza.
 
Acha story za vijiweni.
 
LEO WAKO WAPI WALIOLOPOKA
MBONA SIWASIKII.
Mtujuze leo wanaongeleaje hili swala? au ndio kama kawaida vichwa vyao havitunzi kumbukumbu ya vinywa vyao.
Mwandishi pia ameulizia swali hilo, kwamba wale waliotuhaminisha na kujihapiza kwamba Tanzania itakuwa kahanani punde tu tukiwakubali hawa DP world. Wengine wakafanya mahesabu ya matrillioni tutakayopata ilikuwa zaidi ya asilimia 50% ya budget ya nchi kwa mwaka. Hivi hawa watu hawaoni haibu, wako wapi? sura zao wamezificah wapi? hata kutoka hadharani na kusema mtusamehe hawawezi? wameuchuna kama vile sio wao. Na hilo ndilo tatizo la watanzania, tunasahau mapema sana. Sehemu nyingine wangeandamwa mmoja baada ya mwingien watwambie kwa nini baada ya kupelekwa dubai, wakakaa 5 stars hotel, wakala bata , walikuja kutudanganya.
 
Una hoja nzuri lakini uswahili ndio shida, umeandika kama mtu mwelewa lakini ukianza tu na "acha usanii dogo" mtu anakushusha unajuwa mtu wa aina gani. twende kwenye hoja yako. andika gharama na before kwa kutumia breakdown uliyoandika. Ili tujuwe gharama zimepanda ziko ndani ya uwezo wetu au hapana. Kama ni number 3, 4, 5, 6 ni ya sera za kikodi lakini najuwa budget mpya bado sasa uhakika hakuna ongezeko hapo. 1, 2, 7, 8 na 9 haziko kwenye mikono yetu hasa CIF sasa tupe comparison kabla na baada.
 
wewe pita uandishi wako tu najuwa naongea na mtu ni kama hajielewi au uhuni fulani wa kizamani.
Mkuu wewe panic tu ila the fact is ulichoandika ni story za vijiweni.
 
Akili za CCM hizo,,hawezi kuelewa hilo andiko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…