Walisema DP World itashusha gharama na siku za mizigo kukaa Bandarini. Leo gharama za kuingiza mzigo zitapanda kwa 360%

MLETA MADA AMEKUJA KAMA KATUMWA KUWATIA WATU MASHAKA NA KUPANDIKIZA CHUKI.

MTOA MADA KWANN HUKUTOA SABABU YA BANDARI KUONGEZA BEI YA CONTAINER. ?? NA BADALA YAKE UMEPELEKA LAWAMA MOJA KWA MOJA KWA RAIS NA VIONGOZI KWA UJUMLA ?? ULIKUWA HUJUI KAMA KUNA SHIDA REDSEA.?? AU HUNA INFO KAMILI ?? ALAFU KWANN USIANDIKE KAWAIDA WATU WAKAKUELEWA NA KUANZA KUCHAMBUA KULIKO UMEANDIKA HARAKA HARAKA ALAFU UMEKIMBIA ?? HUKU UNAWATIA WATU KAZI.??? KWAHIYO UNATAKA KUWAAMINISHA WATANZANIA KUWA KAMA SIO DP WORLD KUWA PALE BEI ZA CONTAINER ZISINGEPANDA.??????????????
 
WaTZ wengi ni kama kupe.
 
Hao Mombassa mizigo yao inapitishiwa wapi?
 
Bahati mbaya kwetu na nzuri kwao Rais wa tanzania haamriwi na Kura za wananchi.
Hii nchi ukiwa na akili ya kuona mambo kabla hayajatokea utateseka sana.
Basically hii nchi ina hasira sana na watu wenye akili.
Mkuu nimeipenda sana hii para "Basically hii nchi ina hasara sana na watu wenye akili" Ahsante.
 
Safi sana , ni hbri njema hii.Gharama zipande za kutoa mizigo zipande , bidhaa madukani zipande, wananchi washike adabu ili ikifika 2025 wawe na akili za kulitoa madarakani hili dubwana liitwalo CCM
Haya ukimtoa madarakani utakipa chama gani dhamana?
 
Tatizo akili za wajinga wengi zimehodhiwa na ccm,suala nyeti kama hili wakaingiza udini kweli tumepatikana MUNGU tu ndiye atatuepusha na hatari iliyo mbele huko.
Hii nchi hii 😔
Sijui mchawi aliyeturoga ni wa nchi gani. Mtu anashiriki kudanganya na anajua kabisa anadanganya.
Ilimradi maslahi yake yanatimizwa anasahau ya wengine.
 
Inawezekana umesoma ukiwa tayari una majibu. Mtoa mada hajatumwa na wala hakuwahi kutumwa. Rudia kusoma tena. Tatizo la baadhi ya watanzania kila hoja ya msingi tunaipeleka kisiasa. Mtoa mada hajamtaja Mh Raisi labda wewe utuambie wapi ametajwa; ila mtoa mada ametaja kuna baadhi ya viongozi , wapambe na waandishi wa habari walipewa rushwa za aina mbalimbali;hata kupelekwa Dubai kwenye 5 stars hotel ni rushwa ya ushawishi na baada ya safari hizo wote waliifagilia DP -World as if ndiyo mkombozi kinyume na kabla ya kupelekwa huko, kinyume na misimamo yao mikali tuliyokuwa tunaifahamu. Swali ni kitu gani kiliwalainisha mpaka wakakosa objectivity kwenye kudiscuss na kupambanua faida na hasara ya kumilikisha Bandari kwa DP world.

Suala la Red-sea ni global issue na imeaffect all countries almost equally na kila mtu analijua hilo.Swali la kujiuliza ambalo na wewe ulitakiwa ujiulize mbona kuna almost three fold (thrice) increase ya kodi ukilinganisha na nchi nyingine. Yes hata nchi nyingine kodi imepanda lakini ni average na reasonable; at least 20-50% sisi tuko kwenye 360% wewe bado unaona ni sawa tu.

Kwetu sisi ukiacha suala la red sea unafikiri ni kitu gani kingine kimesababisha three fold increase ya ghalama. Hapo ndipo tunakuja kwenye suala la DP world, huwezi kuwatenganisha na huu mkwamo kwani wao ndio wanaoendesha Bandari kwa sasa na hawaingiliwi na mtu yeyote na wala usifikiri watakuwa na machungu na madhara yatakayowapata wananchi kwa maamuzi yao. Kumbuka wao wako kibiashara na ndio maana tunarudi kulekule ,kwamba kuna strategic economic sectors zinazodetermine major sources of country revenues na well being ya wananchi, hizo sector lazima zilindwe na lazima kuwa makini kama ikibidi kubinafsisha hasa kwenye kipengere cha kuvunja mkataba. Hivi wewe eneo hili unaona lilikuwa sawa kabisa, mtu unasign mkataba wa miaka 30 ambao ni ngumu kuuvunja., kwa Bandari nachelea kusema hatukuwa makini kwa hapa na hiki kinachotokea kilitegemewa ila wachache walibisha na kujihapiza.

Wewe unataka kuipeleka mada kisiasa wakati hii mada inatakiwa iwe open kama eneo linaloelekea kupeleka maisha ya wananchi kuwa ya shida. Acha watu wajadiliane bila kuingiza siasa, acha watu wawe huru. Wewe kama huoni hatari kwenye maisha yako acha wengine waongee ambao wao, watoto wao, wazazi wao, wajukuu zao, jamaa zao wamekwisha anza kuathilika na mkwamo huu. Hivi unajua recently watu wamehifadhi na kuficha bidhaa adimu (hasa maagent wakubwa wa vifaa ya ujenzi, kupikia, gas, vipuli nk.) , maagent wote wanasema hawana vifaa, unajua kwa nini. Wanasubiri sasa hili ongezeko lianze kufanya kazi ili na wao wapandishe ghalama wakisingizia hilli ongezeko wakati bidhaa hizo waliziingiza mapema. Kwa wafanya bisahara watakuwa wamenielewa.

Husiwazibe watu midomo, husiwafumbe watu macho, husiwapumbaze watu akili. Sasa watanzania wengi wamefunguka wanajua upi ni ukweli na upi ni si ukweli. Subiri baada ya miezi sita nitarudisha uzi huu, ila nitakuwa ninataja machungu tutakayokuwa tunapitia, halafu nitakuomba uendelee kubisha.
 
Mchakato wa majadiliano ulipitishwa je hivi vifungu vya upandishaji wa gharama wa kutopandisha kiholele haukujadiliwa maana ni ilikua ni muhumi sana, atavaa silaha zote za ki monopolistic tutakosa pakupumilia
 
Daaah
 
Mkuu nimeipenda sana hii para "Basically hii nchi ina hasara sana na watu wenye akili" Ahsante.
Sawa kabisa kama jamaa mmoja hapo anaongelea suala la Redsea as if issue hii inahusu Tanzania tu. Yaani suala la kujenga hoja (making a case) kwa watanzania wengi ni shida. Huwezi kuongelea effect ya Red sea conflict huku wenzetu Kenya na Bandari nyingine mambo ya mswano, wamejiadjust kidogo tu lakini sisi tumepandisha kodi three-fold, sasa hiyo ni hoja gani. Wengine wakishindwa kujenga hoja wata-attack personality yako au watakuingiza kwenye siasa. Kwa kweli inasikitisha sana

Kwa mfano tu wa jinsi tusivyojua kujenga hoja na tulivyo watu wa ajabu. Unaweza ukamwambia mtu mzima kabisa hiki ni kinyesi, ni mavi.Jinsi tulivyowabishi utasikia hapana hiki si Kinyesi, si mavi ni mabaki ya chakula baada ya kupita tumboni na kwenye utumbo mpana na mdogo. Sasa unajiuliza huyu lengo lake ni kubisha tu, huoni sababu ya kukataa hiki si Kinyesi. kwani hatukuwa tunaongelea process ya kutengenza Kinyesi tunaongelea jina la end product ambayo ni Kinyesi.Ndivyo ninavyoona kwa baadhi yetu tunavyomake a case, hata humu tuko wengi wa namna hiyo
 
Mchakato wa majadiliano ulipitishwa je hivi vifungu vya upandishaji wa gharama wa kutopandisha kiholele haukujadiliwa maana ni ilikua ni muhumi sana, atavaa silaha zote za ki monopolistic tutakosa pakupumilia
Bora umeuliza swali gumu ambalo hutapata jibu. Swali gumu lingine ni je zile mutlibillions investment tulizoambiwa zitakuwa invested Bandarini na hawa mabwana zililetwa au wamechukua kilichokuwepo na zile kubenefits geti mpya tulizokuwa tumekamilisha zile za mkopo wa trillion 2 , wao wakaanza kuendesha tu. Yaani ukisikia mtelemko ndio huu. Hivi kweli hawa ni waharabu wa Dubai kweli, hisije ni wabongo wajanja wamejivisha U-DP world. Ukiangalia hili suala kwa umakini sana, mchakato wenyewe, contracts zilivyoandikwa, sula la kuvunja mkataba, kiasi wao watakachoinvest na namna walivyopwewa Bandari. Mh kama ni mtu aliyekuwa najua kila kitu cha ndani hasa our weakness na weakness ya kisystem.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…