Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Mimi ni Mwanafunzi wa degree, nipo Mwaka wa Pili katika chuo Cha Abdurahman Al-Sumait kilichoko Zanzibar.
Mimi na wenzangu tulipata ufadhili wa masomo (Scholarship) kutoka Taasisi ya Direct Aid Society ambayo zamani ilijulikana kama African Muslim Agency (AMA) ambayo ndio wamiliki wa Chuo cha Sumait pamoja na MUM cha Morogoro.
Tuliahidiwa kufadhiliwa ndani ya kipindi chote cha masomo yetu yaani miaka mitatu ya degree, huku tukilipiwa kila kitu ikiwemo full tuition fee, accommodations, stationary na transport hadi mwisho wa mwaka.
Ajabu baadhi ya watu tumepigwa simu kutoka chuoni kwamba hatuna ufadhili tena kwa hiyo tuanze kujilipia la sivo tuache chuo bila ya kuzingatia kwamba hatuna makubaliano ya kimkataba ya kumuondoa mtu yeyote kwenye ufadhili huo.
Serikali yetu zitusaidie maana sasa hivi hatujui hatma yetu ya kimasomo ikoje na chuo kimefunguliwa tangu 28/10/2024.
Wengi wetu ni maskini na yatima ndio kilikuwa kigezo cha kupata ufadhili. Maana tungepewa maelekezo ya kimkataba awali tungeamua tukubali au tukatae ufadhili wao. Sasa wanatuacha sasa hivi hatuna pa kukimbilia na huu ndo mwaka wetu wa mwisho masomo.
Rais wa Wanafunzi wa SUMAIT, Salim Abass amesema:
JamiiForums imewasiliana na Kiongozi huyo wa Wanafunzi, anaelezea: Mimi pia ni mmoja wa wanufaika wa ufadhili huo, kilichotokea ni kuwa kila baada ya semester kulikuwa kuna vikao vinafanyika vya maboresho na mazungumzo ya mikataba ya ufadhili.
Baadhi ya Wanafunzi walikuwa hawashiriki, hivyo inawezekana kuna baadhi ya mambo yamewapita, kwa kuwa baada ya mazungumzo kila mtu alikuwa anasaini mkataba wake pekee, huwezi jua mwenzako amesaini mkataba wa aina gani.
Moja ya maelekezo ya mkataba ni kuwa Mwanafunzi alitakiwa kuwa na wastani wa ufaulu wa GPA ya 3.0, ambaye hafikishi inamaanisha anatolewa katika ufadhili.
Fedha wanazotupa ni nyingi na inawezekana zinaweza kuwachanganya wanufaika wakajisahau kufuatilia mambo kama hayo ya maboresho ya mikataba.