Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Bara la Afrika ndiyo bara tajiri sana kuliko mabara yote duniani, kuanzia kwenye rasilimali watu (human resources) hadi kwenye rasilimali asili (natural resources).
Ni bara kubwa lenye majitu yenye nguvu yanayo stahimili dhoruba mbali mbali kuliko watu wengine duniani. Ndiyo maana utaona mabingwa wa dondi duniani ni watu toka bara hili, wachezaji wazuri wa soka na ridhaa wengi wanatoka bara hili. Ni mijitu highly naturally selected yanayo stahimili magonjwa na taabu za duniani kuliko watu wengine duniani.
Ni bara lenye rasimali nyingi na za aina zote za hapa duniani. Ardhi yenye rutuba ya asili, misitu minene, viumbe vya aina zote - both micro and macro organisms, madini ya aina zote, maji mengi ya mabahari, maziwa mengi makubwa makubwa, mito mingi mikubwa mikubwa na kadhalika. Bara hili ni kama ile bustani ya Adeni kule paradiso inayosimuliwa na vitabu vitakatifu.
Ndiyo maana jamaa walipoliona bara hili, walilivamia. Walianza na kutuchukua utumwa na kutupeleka huko kwao kuwajengea nchi zao. Ndiyo maana utatukuta tuko huko, America tunaitwa maniga na kadhalika. Wakaona hiyo haitoshi wakatufanya makoloni yao ili waweze kuzichota vizuri maliasili zetu. Walipoona tunataka kuwa wajanja, wakaamua kutuwekeza (neocolonize). Lengo lao ni hilo hilo la kuendelea kuchota na kumiliki maliasili zetu hususani madini yetu, bandari zetu, rasilimali watu yetu na kadhalika.
Hiyo janja janja ya mikataba yao ya uwekezaji ndiyo mikakati yao ya neocolonization. Tunahitaji kuwa makini sana na hawa jamaa. Uwekezaji salama tunapaswa kuufanya wenyewe. Makampuni yetu ya wazalendo yanaweza. Hata hayo makampuni ya nje mitaji yao wanaipata kwa kukopa mabenki. Mikopo hiyo ndiyo inawawezesha kununua vifaa vya miradi na kuajili watalaam wa kutekeleza hiyo miradi. Hata kampuni zetu za ndani za wazalendo zinaweza sana kufanya mambo hayo. Hao siyo wajomba zetu. Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe. Tuzinduke.